Mjue Cuckoo, ndege mkwepa majukumu ya ulezi, ndege mwenye roho mbaya

I am Groot

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
3,929
Reaction score
10,747
Cuckoo ni jamii ya ndege wasafiri ambapo husambaa katika kipindi cha kiangazi kwenye bara la ulaya, Asia na Africa.

Jamii hii ni aina ya ndege hukwepa majukumu kwa kupandikizia watoto wao kwa jamii nyingine za ndege ili walelewe tangu yakiwa bado mayai.

Kwa maana kuwa hutaga kwenye viota vya ndege wengine kisha wao huendelea kula maisha ya ujana bila kujali huko nyuma mambo yatakuwaje kwa hao (host) waliosingiziwa.

Pamoja na kuwa mayai yao huwa makubwa kuliko ya host wao, ndege hawa huakikisha sana yanaendana na mayai mengine waliyoyakuta kwenye viota vya mahost wao kwa ukubwa kiasi pamoja na rangi ili host asishtukie.

-mayai ya cuckoo yakiwa na mayai mengine ya host wake.

Chakula cha kawaida cha cuckoo kina jumuisha wadudu, manyungunyungu (caterpillars), ambayo ni chakula cha ndege wengi duniani. Pia muda mwingine hula mayai na vifaranga wengine kwenye viota ili kujikidhi mahitaji yake.

Cuckoo kama jamii ya ndege parasite; hutaga mayai yao kwenye viota vya ndege wengine. Vifaranga vinavyototolewa huwasukuma vifaranga au mayai ya ndege mwingine nje ya kiota. Cuckoo jike hutembelea hadi viota 50 tofauti tofauti kipindi cha utagaji. Kikawaida cuckoo huwanza kutaga baada ya miaka miwili.

Cuckoo majike wamepatiwa uwezo mkubwa wa kuweza kuigilizia miundo na rangi za ndege wengine.
Inaelezwa kuwa madume kuzaa na majike wengi na watoto wao hukuzwa na jamii zaidi ya moja ya mahost.

Kifaranga wa cuckoo kutotolewa baada ya siku 11-13. Njia hii ya utotolewaji haraka hutumiwa na jamii nyingi vamizi. Kifaranga huwa mkubwa kimwili kuliko kifaranga wa ndege host. Na hutaka kuudumiwa chakula pekee yake kutoka kwa wazazi host. Hivyo baada ya kutotolewa , husukuma mayai mengine nje; na endapo kuna kifaranga tofauti na yeye atabahatika kutotolewa mbele ya macho yake, naye hutupwa nje vilevile.
Baada ya siku 14 tangu kutotolewa kifaranga huyu wa cuckoo huwa mkubwa mara 3 zaidi (X3) ya mzazi mlezi.

Sababu haswa za cuckoo hawa makinda kutupa mayai mengine au vifaranga wengine wa mwenyeji wake nje ya nyumba; bado haifahamiki.
 
Attachments

  • 440px-Cuculus_canorus_chick1.jpeg
    66.8 KB · Views: 11
  • Cuculus_canorus_bangsi_MHNT.ZOO.2010.11.149.13.jpg
    9.2 KB · Views: 10
Cuckoo ni jamii ya ndege wasafiri ambapo husambaa katika kipindi cha kiangazi kwenye bara la ulaya, Asia na Africa. View attachment 3009618

Jamii hii ni aina ya ndege hukwepa majukumu kwa kupandikizia watoto wao kwa jamii nyingine za ndege ili walelewe tangu yakiwa bado mayai.

Kwa maana kuwa hutaga kwenye viota vya ndege wengine kisha wao huendelea kula maisha ya ujana bila kujali huko nyuma mambo yatakuwaje kwa hao (host) waliosingiziwa.

Pamoja na kuwa mayai yao huwa makubwa kuliko ya host wao, ndege hawa huakikisha sana yanaendana na mayai mengine waliyoyakuta kwenye viota vya mahost wao kwa ukubwa kiasi pamoja na rangi ili host asishtukie.
View attachment 3009620
View attachment 3009624
-mayai ya cuckoo yakiwa na mayai mengine ya host wake.

Chakula cha kawaida cha cuckoo kina jumuisha wadudu, manyungunyungu (caterpillars), ambayo ni chakula cha ndege wengi duniani. Pia muda mwingine hula mayai na vifaranga wengine kwenye viota ili kujikidhi mahitaji yake.

Cuckoo kama jamii ya ndege parasite; hutaga mayai yao kwenye viota vya ndege wengine. Vifaranga vinavyototolewa huwasukuma vifaranga au mayai ya ndege mwingine nje ya kiota. Cuckoo jike hutembelea hadi viota 50 tofauti tofauti kipindi cha utagaji. Kikawaida cuckoo huwanza kutaga baada ya miaka miwili.

Cuckoo majike wamepatiwa uwezo mkubwa wa kuweza kuigilizia miundo na rangi za ndege wengine.
Inaelezwa kuwa madume kuzaa na majike wengi na watoto wao hukuzwa na jamii zaidi ya moja ya mahost. View attachment 3009623

Kifaranga wa cuckoo kutotolewa baada ya siku 11-13. Njia hii ya utotolewaji haraka hutumiwa na jamii nyingi vamizi. Kifaranga huwa mkubwa kimwili kuliko kifaranga wa ndege host. Na hutaka kuudumiwa chakula pekee yake kutoka kwa wazazi host. Hivyo baada ya kutotolewa , husukuma mayai mengine nje; na endapo kuna kifaranga tofauti na yeye atabahatika kutotolewa mbele ya macho yake, naye hutupwa nje vilevile.
View attachment 3009626Baada ya siku 14 tangu kutotolewa kifaranga huyu wa cuckoo huwa mkubwa mara 3 zaidi (X3) ya mzazi mlezi.

View attachment 3009627
Sababu haswa za cuckoo hawa makinda kutupa mayai mengine au vifaranga wengine wa mwenyeji wake nje ya nyumba; bado haifahamiki.
 
Haya ni maajabu, tunaweza kuita ni ndege wachawi wanaologa ndege wenzao. Wanavamia viota vya wenzao wanataga humo na kulelewa watoto humo, watoto nao wanafanya ukakusi kwa walezi waliowalea. Haya mambo hata kwa binadamu huenda yapo kwa siri sana
 
Kweli kabisa, tena Nat Geo Wild saa 1 hii wametupa hii elimu kidogo.
 
Hii niliiona kwenye documentary flani ya ndege, lkn sikuelewa kbs kwa nini ndege anakuwa na kifaranga kikubwa kuliko wazazi wake, na hawafanani! leo nimepata jibu..asante
 
Aisee hii ni kali....kumbe kuna parasite mpka ndege,......Mungu ana maajabu sana aisee....hii dunia bado yapo mengi sana ambayo hayajulikaniki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…