Mjue Eugene Maganga mhusika wa njama za kuipindua Serikali ya Rais Julius Nyerere Januari 9, 1982

kwa mimi niliyesoma shule ya Technical, naona nyota tuu hapa (nimemtambua Hans Pope na Baba wa taifa tuu)
 
Imagine wangefanikiwa kumuua Nyerere dah.! Kuna vitu hata kama mtu ni muovu kuna nguvu humkinga.

Sijui tungekua kama kina Burundi na Rwanda huko au Congo D.R. Kupinduana tu.

Sent from my Pro_Max11 using JamiiForums mobile app
 
Mimi nilisoma na Selemani Kamando, wakati tukiwa sekondari skuli alijulikana kama Sulemani Mathusela, hilo la Kamando lilikuja wakati tunamaliza Form Four na kisha kujiunga na JWTZ. Kwa kweli nilishangaa sana niliposikia amejiunga na JWTZ kwani alikuwa mzembe mzembe sana, anapenda sana kula hadi akapachikwa jina la TOP LAYER kwani alikuwa anapenda sana mafuta ya juu hasa kwenye maharage au nyama - kutegemea siku hiyo kuna msosi gani - na alikuwa anapata hiyo "top layer" kwa kuhakikisha kuwa anakuwa wa kwanza kujichotea msosi huo kila siku; na alifanikiwa kwa hilo kwani alikuwa akiwahi kuingia mesini na kuachagua position ulipo "mchuzi" na kuanza nao!

Huyo ndiyo Kapteni Kamando ninaye mfahamu. Pia lile la kumsoma kuwa alikuwa kwenye hicho kikundi cha kutaka kuipindua Serikali ya Mwalimu Nyerere, kilinishangaza sana kutokana na tabia yake ya uzembe uzembe na ukimya! Ila nadhani aliingizwa humo na hao "wanyamwezi" wenzake, akina Maganga, otherwise Kapteni Kamando hakuwa na misimamo mikali politically.
 
Wanajeshi wa zamani walijua strong sana aisee !!! Sidhan hawa wala chips kama wanaweza hii filamu
 
Rubani wa Helikopta nilifanya nae kazi!
 
Nikiwa n Capt.Maganga tulipanda naye basi maeneo ya Magomen Dar,akamkaribisha Maganga Kwan alikuwa anaoa siku hiyo
Simulizi nzuri, lakini kusema Nyerere alikaa nje ya nchi miezi miwili ni uongo.

Nyerere hakuwa nje ya nchi, alikuwa likizo ya kawaida kila mwisho wa mwaka Butiama.

Kilichoshtua ni kuendelea kubaki Butiama hata likizo ilipomalizika. Alikuwa na utaratibu wa kulihutubia taifa kwa kilichoelezwa kama salamu za mwaka mpya akiwa Dar, lakini mwaka ule alihutubia kutokea Butiama.

Jingine, kama kumbukumbu zangu ziko sawa, wakati wanakamatwa, Maganga tayari alikuwa keshafanya mitihani ya mwaka wa mwisho chuoni. Walikamatwa baada ya mwezi Mei.
 
Maganga alikuja kuwa rafiki yangu.Ninachokumbuka alinambia hajuweza kumaliza degree yake.Mauti yalimfika hospital ya Amana Ilala na msiba ulianzia Banana na baadaye kusafirishwa kwenda kwao Tabora.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…