Mjue Jelly Fish Samaki hatari baharini, ni haja wavuvi kuwa nae makini

Mjue Jelly Fish Samaki hatari baharini, ni haja wavuvi kuwa nae makini

ROJA MIRO

Member
Joined
Jul 19, 2021
Posts
52
Reaction score
56
Box Jelly fish (Sea wasp), ni samaki anaepatikana baharini,hasa katika bahari ya Pacific (Indo-Pacific) pia katika bahari ya Atlantic.Hupatikana kwa wingi katika nchi za Australia,New Zealand,Philippenes na mji wa Hawaii ulioko USA.

Samaki huyu hujulikana kama 'the most deadliest fish in the world', 'the world most venomous creature', na 'the most notoriously dangerous specie in the world' yaani kiumbe hatari kuliko vyote duniani,yote hii katika kumsifia kutokana na uwezo wake wa kuua kwa sumu kali na kwa haraka kuliko kiumbe chochote duniani.

MAISHA YAKE.
Box Jelly fish ukubwa wake unakuwa na urefu wa cm 20, na 'miguu' yake inakuwa na urefu wa kufikia mita 3, ana uzito wa kg 2.Ana jumla ya macho 24,ambayo huwa yamekaa yamekusanyika sita na yakiwa katika kona nne za mwili wake.Wanaishi muda wa mwaka mmoja tu toka wazaliwe.

MUONEKANO.
Ukimuangalia kwa umbo unaweza kusema ni kiumbe kidhaifu na hata cha kufuga ili uchezee,maana yupo kama maua.Kwa wale walioangalia movie ya Seven Pound ya Willy Smith watakuwa wamemuona pale mwishoni.


Kwa viumbe wa ardhini na majini tunaweza kupima ukali wake wa kuua kwa sumu kwa kuangalia vigezo viwili.

(a) Sumu yake anayotoa kwa kipimo cha ounce (ounce 1=28.3 grams),kina uwezo wa kuua watu wangapi?

(b) Hiyo sumu inaweza kuchukua muda gani kuua mtu?



Kwa kutumia vigezo hivyo hapo juu, utaona kuwa Box Jelly fish anawazidi kwa mbali viumbe vingine wote wa baharini na nchi kavu kwa kuwa na sumu kali yenye kuweza kuua watu wengi na kwa haraka.

SUMU YAKE.
Box Jelly fish anaweza kuua kwa kipimo cha ounce moja ya sumu yake inaweza kuua watu 60 kwa mpigo! Na hao watu kwa sumu hiyo lazima wafe chini ya dakika 3 tu! Hapa utaona hata yule nyoka tunayemuogopa zaidi duniani ambae ni Black Mamba au maarufu kwa jina la Koboko..Hafui dafu hata kidogo kwa samaki huyu.


1628487400860.jpeg


SUMU HUNASHAMBULIA NINI MWILINI MWA MTU.
Sumu yake akikupiga inaenda kwa haraka kushambulia moyo na kuua mifumo ya neva kwa haraka hivyo kukuua haraka.

KILICHO HATARI KWAKE
Samaki huyu hazungushi au hafurukuti kwa turtles (kasa), ambao sumu ya jelly fish huyu haimdhuru.

ANAULIWAJE
Mpaka sasa hakuna binadamu aliyefanikiwa kumuuwa samaki huyu kwa kila unapokata miguu yake huchipua ndio maana unashariwa kumuacha maana ni kiumbe kisichokufa kwa kuuliwa hasa na binadamu.

SOURCE:- IUCN Eastern Africa Programme.
 
Hii mada IPO humu kitamb

USSR
 
Hawa Jellyfish kwa lugha ya Kijapani wanajulikana kama "Kurage" or Japanese Jelly Fish.

Kuna documentary fulani walikuwa wanaionyesha National Geograhical jinsi wanavyowavua, kwa sababu ya kuwa wengi katika bahari ya Pacific ukanda wa nchi ya Japan kwa sababu ya kuzaliana sana within a short period of time.

Nakupelekea kuhatarisha Uhai wa Viumbe hai wengine wa majani or other (Marine Organisms).
 
Sasa tukizama Pasific itakuwaje? kina kirefu shida Jely fish nao shida
 
Back
Top Bottom