Mjue Jelly Fish Samaki hatari baharini, ni haja wavuvi kuwa nae makini

Wavuvi wetu hawafiki huko Pacific kwenda kuvua
 
Mpaka sasa hakuna binadamu aliyefanikiwa kumuuwa samaki huyu kwa kila unapokata miguu yake huchipua ndio maana unashariwa kumuacha maana ni kiumbe kisichokufa kwa kuuliwa hasa na binadamu.
Hakuna specie hatari kupata kutokea ulimwenguni kama binadamu!!

Huyo Jellyfish ni kwavile tu hajaleta uhalifu mkubwa kwa mwanadamu... ngoja nae ajifanye corona wa kuua watu ovyo ovyo ndipo atajua kama watu watakosa mbinu za kumteketeza.

Huyo Mungu mwenyewe tu ndo hivyo tena kwavile kajificha!!
 
Hivi wanaposema mfano sumu ya nyoka kama black mamba inaweza kuua watu wazima 20 wanamaanisha akiuma hao watu 20 ndio sumu inaisha au inakuwaje? Au pengine uwezo wake wa kung'ata ndio unaisha anakuwa amechoka?

Maana yake ni kuwa ujazo wa ile sumu anayoitoa kwa mara moja, kama ukiweza kuiweka kwenye sindano basi inatosha kuwachoma watu 20 na kiwango hicho cha mils/oz kutosha kuwaua wote...
 
Usikute wachina wanamla huyu.
 
Iyo sumu anamdunga vipi binadamu, anaFUNG kama nyoka anakuuma
 
Umesahau hapa.

Anatumia hizo kamba(mikia yake)ya 3m kunasa mvamizi au prey anaowala.
Hiyo kamba moja hata kuiona kwenye maji ni mtihani,lakini ndio ikikugusa moja tu,balaa unalo.

Mungu fundi sana.
Dawa rahisi utomvu wa papai bichi
 
Hawa samaki wapo hapa hapa Tanzania,kwenye bahari ya hindi.Mtoa mada hujatoa credit kuhusu hilo.
 
Hapo Kwenye Jelly Kidogo Iwe KY..........
 
Mara tunaambiwa samaki huyo huwa hazeeki wala hafi.Mbona sasa hizo siyo sifa za kiumbe hai kama Biology ya form 1 ilivyotuambia?

Halafu hayo maviumbe ya baharini mengi huwa ni majini yaliyovaa taswira ya vitu vingine ili tusiyashtukie.I suspect Jelly fishes are Jinnis.
 
Samaki huyu hujulikana kama 'the most deadliest fish in the world', 'the world most venomous creature', na 'the most notoriously dangerous specie in the world'
Mkuu samahani naomba kukusahihisha kidogo hapo kwenye bold, ni kweli jellyfish ni kiumbe mwenyewe sumu Kali sana lakini sio kuzidi viumbe wote duniani.
Huyu anaongoza kwa kuwa na sumu Kali zaidi kwa viumbe wa baharini (the most venomous marine creature) na huyo ni Australian box jellyfish.
Kiumbe anayeongoza kwa kuwa na sumu Kali zaidi duniani pote ni NYOKA ajulikanaye Kama "INLAND TAIPAN"
Anapatikana huko east Australia, sumu anayotoa kwa kung'ata Mara moja tu Inatosha kabisa kuua watu wazima Mia moja!
 
Hivi wanaposema mfano sumu ya nyoka kama black mamba inaweza kuua watu wazima 20 wanamaanisha akiuma hao watu 20 ndio sumu inaisha au inakuwaje? Au pengine uwezo wake wa kung'ata ndio unaisha anakuwa amechoka?
Hapana mkuu; Iko hv. Ule ujazo au wingi(volume) wa sumu iliyopo na anayoweza kuitoa, ikigawiwa kwa vipimo sawa (mls au cc) inatosha kuua watu wazima (kiafya) 20. Lakini kwa kawaida nyoka yoyote anapouma au kung'ata huwa hatoi sumu yake yote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…