Raphael Mtui
Member
- Nov 26, 2024
- 78
- 204
Ilikuwa tarehe 19 July mwaka 64AD. Moto mkubwa ulianza kuwaka karibu na mtaa uitwao Circus Maximus, katika jiji la Rumi. Kwa sababu jiji la Rumi kwa miaka hiyo lilikuwa limejengwa kwa vitu ambavyo vinashika moto haraka, jiji zima likashika moto mkubwa!
Kwa miaka ile, bado hakukuwa na nyenzo bora za kufaa kuzima moto kama ilivyo leo. Ule moto uliwaka kwa fujo siku tisa mfululizo na kuteketeza jiji zima la Rumi!
Mpaka moto unaisha, mitaa minne tu ya jiji la Rumi haikuguswa na moto ule, lakini mitaa kumi na nne iliungua vibaya, wakati mitaa mitatu iliungua kabisa kabisa!
Juu ya nyumba ya makazi ya kifalme, inasemekana alikaa jitu hatari, katili mwenye kupenda kuona taswira za watu wakiuawa mbele yake. Akiwa pale, habari zinasema kuwa alikuwa akicheza chombo cha muziki huku akiimba kwa furaha wakati watu wote mjini wakilia kwa uchungu.
Mtu huyu alikuwa kijana mdogo tu wa miaka 26. Licha ya utoto wake, yeye ndiye aliyekuwa mfalme wa dola kubwa zaidi duniani kwa kipindi hicho, naam, Roman Empire. Dola hii ya Rumi ndiyo ilikuwa ikitawala dunia nzima iliyojulikana kwa kipindi kile, baada ya Dola ya Wagiriki kuvunjika.
Kijana huyu ni maarufu kwa jina moja la Nero. Jina lake baada ya kuasiliwa ni refu, aliitwa Nero Claudius Caesar Augustus Germanicus.
Huyu ndiye alikuwa mfalme wa awamu ya tano ya serikali hii ya ufalme wa Rumi akitawala tangu mwaka 54AD hadi 68AD alipojiua.
Kijana huyu aliukwaa ufalme akiwa na umri wa miaka 16 pekee, na akafariki kwa kujiua akiwa bado mdogo wa umri wa miaka 30, kama tutakavyoona mbeleni katika makala haya.
Tuanze hivi:
Karibu na 'Krismasi' ya mwaka 37AD, tarehe 15 December, kijana mmoja alizaliwa pale Antium nchini Italia. Kijana huyu akapewa jina la Lucius Dominitius Ahenobarbus.
Mama yake mtoto huyu aliitwa Agrippina. Huyu Agrippina alikuwa ni kitukuu cha yule mfalme Augusto tunayemsoma kwenye Luka 2:1.
Wakati kijana huyu akiwa na umri wa miaka miwili, mama yake aliwekwa kizuizini, na hivyo akabaki bila mama.
Mwaka uliofuata, mabalaa yakazidi kumwandama huyu mtoto, baada ya baba yake kufariki. Inasemekana kwamba huyu baba aliuawa kwa kuwekewa sumu na mke wake, yaani yule Agrippina mama yake Lucius aliyewekwa kizuizini.
Kijana Lucius alipofikisha miaka 11, jambo la ajabu likatokea: mama yake aliolewa na mfalme wa Rumi wa wakati huo, mfalme Claudio! Kwa sababu ya tukio hilo, nyota ya kijana Lucius ikaanza kung'aa tena. Tukumbuke huyu mfalme Claudio alikuwa mjomba wa huyu Agrippina, ila kwa zamani zile walioana tu bila kujali 'mjomba ni mama.'
Agrippina alipoolewa na mfalme mtukufu Claudio, Lucius akaletwa na kuanza kuishi ikulu. Ule msemo wa 'ukipenda boga penda na ua lake' ukajidhihirisha. Mfalme Claudio akamchukua kijana Lucius, akamwasili, akawa kama mwanae wa kumzaa, na ili asiingie ikulu na 'nuksi' zake, akabadilishwa jina na kuitwa Nero Claudius Caesar Augustus Germanicus.
Ilikuwa kawaida, na hata leo ni kawaida mtoto anapoasiliwa kubadilishwa jina. Ndivyo mfalme Claudius alivyofanya. Akamfanya Lucius kuwa 'kiumbe kipya' kwa kumpa jina la watu wa heshima, na kumfanya kama mtoto wake wa kumzaa.
Lucius sasa akaitwa Nero, akawa sehemu ya 'ma-home boys' wa pale ikulu ya Rumi. Haikuishia hapo, mama Agrippina akawa akimwomba mume wake jambo kubwa kweli kweli: alimwomba mfalme Claudio amkubali Nero awe mrithi wa kiti chake siku akiondoka madarakani.
Akawa akimwomba Claudio amwandae Nero kuwa mrithi wake. Pia, mama akamwomba Claudio akubali Nero aoe binti yake aliyeitwa Oktavia.
Mfalme Claudio akakubali yote hayo, na akawa akimwandaa Nero kuwa mrithi wake.
Mwaka 54AD Mfalme Claudio alikufa. Nero akiwa bado kijana mdogo kabisa wa miaka 16, kwa kusaidiwa na mama yake, jeshi la pale ikulu pamoja na bunge la seneti, wakampa kijana Nero madaraka.
Maneno yapo mengi yanayodai kuwa ni Agrippina alimwua mfalme Claudio kwa kumpikia uyoga wenye sumu. Hapana shaka huyu mama Agrippina hakuwa mtu mzuri kwa kuangalia tu historia yake.
Madai hayo ya kumwua Claudio yanachagizwa na jinsi huyu mama alivyohangaika kumwingiza mwanae Nero madarakani, lakini pia jinsi 'alivyotawala' Rumi kwa kumtumia mwanae Nero.
Kwa kuwa Nero alikuwa bado kijana mdogo, mshauri mkuu wa masuala ya utawala alikuwa ni mama yake mzazi. Yaani tuseme, kwa kuwa Nero aliingia madarakani akiwa bado mdogo mno, aliyekuwa anaongoza dola ya Rumi ni mama yake.
Wengine waliokuwa wakimshauri na kumwelekeza namna ya kutawala ni pamoja na yule aliyemlea tangu alipoanza kuishi ikulu akimwandaa kuja kutawala, ndugu Seneca the Younger, akishirikiana na mkuu wa ikulu (praitorio) aliyeitwa Sextus Burrus.
Huyu Seneca ndiye aliyemwandikia Nero ile hotuba ya kuingia madarakani, ambayo iliahidi kung'oa mizizi ya rushwa na ukatili wa serikali iliyopita ya Claudio!
Seneca na Burrus walikuwa wakimwongoza kijana Nero chini ya 'mkono wa chuma' wa mama Agrippina. Hawa jamaa hawakupenda kabisa staili ya mama yule.
Waliendelea kumwelekeza Nero kwenye utawala hadi Nero alipoanza kujisikia anapelekeshwa, na moja kwa moja akaanza kutafuta namna ya kutawala bila kupelekeshwa na hasa mama yake.
Alianza kugombana mara kwa mara na mama yake kuhusu mambo ya utawala, mama akiwa anataka kuipeleka Rumi anavyotaka lakini Nero naye akitaka mambo yaende anavyotaka.
Ugomvi huu ulifika pagumu hadi Nero alipoamua kufanya jambo gumu kweli kweli! Aliamua kufanya njama za kumwua mama yake. Kwa kutumia kikosi maalumu, Nero alifanikiwa kuondoa uhai wa mama yake! Ilipangwa auawe kwa kuzamishwa majini, kisha itangazwe ajali ya boti imeua mama mtukufu. Mama akagundua huo mpango, na akajua ni mwanaye Nero amepanga kumwua. Pamoja na kujaribu kuongea maneno mazito, lakini kikosi cha 'wasiojulikana' kilichotumwa na Nero hawakumsikiliza, wakamwua.
Usishangae, ndio hali ya ufalme wa Rumi ulivyokuwa, kuuana tu hapo ikulu, mtu na mama, mtu na baba, mtu na kaka, dada na shemeji, ni mauaji kila siku!
Hata huyu mfalme Claudio aliyeuawa na Aggripina aliingia madarakani baada ya mfalme aliyekuwepo kuuawa Januari mwaka 41AD. Ni yule mfalme Caligula ambaye alimpenda sana farasi wake kiasi ambacho alipanga kumteua huyo farasi akawe gavana au balozi wa nchi fulani, ila kabla hajatekeleza hilo akauawa. Yaani, ungeingia ofisi fulani ya ubalozi, unamkuta mnyama farasi amekalia kiti, huyo ndiye mheshimiwa, unamweleza shida zako, umwombe asaini makaratasi yako, ili 'utoboe' kwenye michakato yako!
Tuache hilo, tuendelee.
Nero alipomwua mama yake, akaanza kutawala anavyotaka. Kwa namna fulani Nero alifanya maendeleo kidogo, ikiwemo kujenga soko jipya zuri pale Rumi. Pia, akaimarisha mishahara ya watumishi wa serikali, akaimarisha jeshi likawa likishinda vita vya kupanua dola ya Rumi, na alipunguza kodi kwa wakulima.
Moja ya vitu ambavyo watu walimpenda navyo ni pamoja jinsi alivyokuwa akisalimiana hadi na wanajeshi wa kawaida kwa kutaja majina yao.
Pia, Nero anajulikana kuwa na tabia ya kupenda sekta ya michezo kupindukia. Kwanza, yeye mwenyewe alijaliwa kipaji cha kuimba, ila shida ni kwamba alipenda kuimba 'wakati ufaao na hata wakati usiofaa'.
Nero aliufanya mji wa Roma ukapambwa na michezo kila mara. Kila mara kulikuwa na matamasha na mashindano mengi ya michezo. Mchezo alioupenda sana ni ule wa mbio za magari. Ilifika kipindi Nero akaona kila kitu kwenye maisha ni michezo!
Nero alituhumiwa kutumia pesa nyingi kuandaa mashindano, na akalalamikiwa kutoa zawadi nyingi mno kwa wale waliokuwa wakishinda michezo mbalimbali. Pesa za maendeleo ya nchi alitumia kugawia washindi wa michezo!
Moja ya mambo mabaya kabisa ambayo Nero anakumbukwa nayo ni pamoja na hilo la kumwua mama yake, kuua mke wake wa kwanza, na pia inasemwa pia ni yeye alimwua mke wake wa pili. Ndoa yake ya kwanza na yule Oktavia haikuwa na furaha. Waliishi kwa vurugu hadi Nero alipoamua kumwua kwa kumpa tuhuma za kwamba 'anatoka' na wanaume wengine.
Mke wa pili inasemwa aliuawa na Nero mwenyewe kwa kumpiga teke la tumbo wakati mke huyo akiwa mjamzito.
Kashfa ingine kubwa iliyomwandama ni ile ya moto niliyoanza nayo. Ni kweli, kuna ubishi kidogo kuhusu Nero alipokuwa wakati moto ulipoanza. Kuna watu wanasema wakati mji unaungua Nero alikuwa safarini Ugiriki, lakini alirudi nchini haraka na inasemekana alitoa misaada ya kutosha kwa watu walioathirika na moto ule.
Lakini, wako wanaosema kwamba Nero alikuwa pale pale mjini na wanaenda mbali na kusema ilifahamika alikuwa wapi na akifanya nini wakati moto ulipoanza. Ndio nikaeleza alikuwa akiutazama moto na kufurahi, huku akiimba kwa sauti yake nzuri aliyojaliwa.
Lakini iwe iwavyo, watu wote wanaungana likija swali la nani alichoma jiji la Rumi kwa moto ule wa kihistoria. Vyanzo vyote hukubali kwamba ni Nero ndiye alifanya njama za kuchoma jiji la Rumi.
Kwa nini afanye hivyo?
Jibu tunalipata kwenye kile alichofanya baada ya tukio lile.
Kwanza kabisa, wananchi walishangaa sana kuona upanuzi wa ajabu alioufanya Nero wa ikulu yake. Nero alifanya upanuzi mkubwa kupindukia wa nyumba ya mfalme, hasa zaidi juu ya kilima cha Oppian kilichopo katikati ya jiji, na hapo akajenga jumba la kifahari lililokuja kuwa maarufu dunia nzima kwa jina la Golden House, yaani Nyumba ya Dhahabu. Walatini waliita Domus Aurea.
Wananchi walidai ilionekana wazi kwamba Nero alitamani kujenga eneo hilo, lakini akakosa namna ya kufanya ili kupata eneo hilo, na ndio akala njama za kuchoma mji mzima.
Hata leo, mara nyingi mioto inayotokea kwenye masoko, majengo na miji inakuwa ina njama za wachache ambao hufaidika maradufu kwa majanga hayo.
Hata hivyo, jumba hilo halikumwacha salama Nero. Fedha nyingi alizotumia kujenga jumba lile, pamoja na pesa nyingi mno alizotumia kujenga upya jiji la Rumi, ziliufanya uchumi wa Dola ya Rumi uyumbe. Akalazimika tena kuongeza kodi mbalimbali kwa wananchi, akazidi kuchukiwa.
Lakini Nero naye akaongeza dhambi ingine ambayo ndiyo inafanya watu wengi wa leo wamjue mfalme Nero.
Nero alijivua lawama ya kuchoma mji moto na kutangaza kuwa moto wa Rumi ulisababishwa na Wakristo! Kwamba, Wakristo ndio walikuwa wamekula njama wakachoma jiji la Rumi! Na hakika Wakristo walikipata!
Sio kwamba Wakristo hawakuwa wakiteswa hapo kabla, bali tukio hili la kusingiziwa lilisababisha mateso makubwa zaidi.
Ni katika kipindi hiki dunia ilishuhudia umwagaji mkubwa wa damu za Wakristo wa lile kanisa la kwanza. Kwa muda mrefu, Nero hakuwahi kuupenda Ukristo.
Tangu ile siku ya Pentekoste Ukristo ulipozaliwa, ilikuwa imeshapita miaka michache sana (kama thelathini hivi) hadi kipindi hiki. Kina Mtume Paulo na Mtume Petro walikuwa wameufikisha Ukristo mitaa ya jiji la Rumi.
Kwa wale waliosoma kitabu changu cha pili, wanajua nimeeleza kwa kirefu jinsi Ukristo ulivyopokelewa na watu wengi pale Rumi, wakiwemo 'watu wazito', mpaka maafisa wa ikulu ya mfalme Nero, na jinsi maafisa hawa walivyokuwa tayari kuacha kazi, ndoa, jeshi ili kujiweka mbali na ibada za kipagani za Rumi.
Katika kitabu kile nikaeleza kwa urefu jinsi mfalme Nero alivyoua watu muhimu sana kuwahi kuikanyaga hii dunia, Mtume Petro na Mtume Paulo.
Lakini nikaeleza kisa chote cha yule mchawi Simon Magus alivyokufa mbele ya mfalme Nero na watu wote wa jiji la Rumi, wakati akitumia uchawi wake kupaa kwenda mbinguni akidai kwamba yeye ndiye masiha.
Mtume Petro akamporomosha kwa maombi akiwa hewani, akaanguka, akafa kifo cha aibu. Kifo hiki kikamwumiza sana Nero, ndipo akaamuru Mtume Petro auawe.
Matukio yote ya kuuawa kina Petro na Paulo nimeyaeleza kwenye kitabu chicho, na miujiza iliyoandamana na kuuawa kwao na baada ya kuuawa kwao. Ukihitaji vitabu vyetu soft copy au hard copy tuwasiliane kwa hiyo namba hapo chini.
Tuache hilo. Ukweli ni kwamba Nero aliua Wakristo wengi akidai ni wao walichoma mji wa Rumi. Wakristo wa pale Rumi hakika waliibeba dhambi ile kwa vifo vya kikatili sana, ikiwemo kuchomwa moto wakiwa hai, na kuvalishwa ngozi za wanyama na kisha kurushwa kwa wanyama wakali kama simba, ambapo waliraruliwa na kuuawa mbele ya watu kama kushuhudia michezo fulani.
Yaani, Wakristo walivalishwa ngozi za wanyama kama mbuzi, kondoo, ng'ombe, kisha wanafungiwa kwenye banda maalum, kisha wanafunguliwa simba wenye njaa wanaokuja kuwararua-rarua na kuwala. Nao ukawa ni mchezo rasmi, watu kukusanyika na kuona Wakristo wanavyoraruliwa na simba!
Wengine waliuawa kwa kupigiliwa misumari msalabani, wakafa kifo cha taratibu kwa mateso makali.
Inasemekana Mtume Paulo naye kesi iliyomfanya akafungwa na kuuawa ni hii hii ya moto. Inaonesha Mtume Petro na Mtume Paulo waliuawa vipindi vya karibu, japo kwa kesi tofauti, Mtume Paulo kwa kusingiziwa kesi ya ule moto, wakati Mtume Petro kwa kumsambaratisha mchawi wa taifa, Simon Magus.
Nero hakuishi muda mrefu.
Iko hivi: Nero aliingia madarakani kipindi ambacho kulikuwa na mabadiliko makubwa ya kisiasa na kiuchumi duniani.
Mataifa mengi yalikuwa yakijiimarisha ili kujitoa kutoka kutawaliwa na Rumi.
Mfano, wakati akiwa safarini Ugiriki utawala wake ulikuwa ukiharibika na alionekana kutokujali.
Usishangae kila saa alienda Ugiriki. Nero alipenda sana tamaduni za Wagiriki. Aliiga michezo yao na kuileta Rumi, na watu wengi hawakupenda. Hata majengo aliyoyajenga pale Rumi baada ya ule moto, aliyajenga kwa kuzingatia staili za Wagiriki.
Wakati huu Gavana wa Hispania Servius Sulpicius alikuwa ameasi serikali ya Rumi na kujitangazia uhuru wake, lakini alikuwa hapati upinzani wowote kutoka kwa majeshi ya Nero.
Pia, gavana wa Ufaransa Gaius Julius naye alikuwa ameasi.
Wakati maafisa wake Nero walipomwambia kuhusu habari hizo, badala ya kuchukua hatua, yeye akacheka na kuendelea kuongea kuhusu michezo na kutaka kuimba.
Tukumbuke, Nero mwenyewe alikuwa akipenda kuimba na alikuwa 'aki-perform' mbele za watu kwenye matamasha kama msanii mwingine yeyote.
Nero aliendelea 'kuchukulia poa' masuala muhimu ya utawala na uendeshaji wa serikali.
Siku yake ikafika. Dawa iliyokuwa ikichemka jikoni kwa muda mrefu iliiva kisawasawa.
Ikafika mahali ambapo baraza lote pale ikulu lilimchoka, wakasema 'kijana asituchezee!'
Wakajadili, wakafikia uamuzi. Wakasema Nero auawe, tena auawe kifo cha aibu kama mtumwa, kwa kusulibiwa msalabani huku akiwa anachapwa viboko. Hawakuwa wanatania hata kidogo.
Kwanza walimtangaza Nero kwamba 'adui wa taifa!' Wananchi wa Rumi wakapokea uamuzi huo kwa furaha, maana walikuwa wanapigwa njaa kali iliyotokana na yule mtawala wa Misri kuasi na hivyo kutopeleka nafaka jijini Rumi. Chakula kutoka Misri kilitegemewa sana pale Rumi. Nero hakujali watu wanakufa njaa, yeye anawaza matamasha ya michezo tu!
Picha likaanza, walinzi wote binafsi wakamwacha! Nero akawa hana 'mabodigadi' tena! Walinzi wote wa ikulu nao wakamwacha. Hali ilikuwa mbaya na hatari kwake, akapanga namna ya kutoroka pale jijini Rumi. Ikashindikana.
Akasema 'hawa watu hawanijui!' Akachukua kisu, akajikata koo, akafa siku ya tarehe 9 June mwaka 68AD akiwa na umri wa miaka 30. Kumbe, licha ya jina la Nero lilivyo kubwa duniani, aliishi miaka 30 pekee!
Raphael Mtui 0762731869