Alikuwa anazo nguvu na uwezo kama kuliko Tembo? anaweza kupambana na Simba peke yake??, anaweza kuua Nyati kwa mikono mitupu?
Hao wanyama wote, Tembo, Simba na Nyati mbele ya risasi hawakohoi sembuse Mtu mmoja mwenye Sifa kidogo za ajabu (peculiarity) ndiye atambe mbele ya Risasi?
Kuna mnyama mmoja, nadhani ni "honey Badger", huyu ukimpiga mkuki au Panga au kitu chenye ncha kali hakitoboi ngozi yake, huyu ndiye mnyama mwenye ngozi ngumu kupenyezeka kuliko wanyama WOTE,, lakini mbele ya Risasi ngozi yake haifui dafu, Risasi inapenya kama kupenya kwenye karatasi.
Risasi ni habari nyingine, huyo Mbokoo anaweza kutodhuriwa na vitu vingine kama kisu, panga nk, lakini sio Risasi, Risasi inapenya katika mwili wa binadamu yeyote.