Solomon David
JF-Expert Member
- Mar 1, 2009
- 1,148
- 17
Hawa watoto wanasemaje?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
shyrose unasemaje?
powa tu .... mwaaa mwaaa mwaaaa
![]()
Mbowe alitetea sana uteuzi huu siku ya uzinduzi wa kampeni za chadema. Mimi nina mashaka CHADEMA kuifanyia majaribio nafasi ya Makamu wa Rais. Wana JF hebu nisadieni kuniondoa mashaka ya Makamu wa Rais huyu endapo haya hapo chini yatatokea.
Sina nia ya kubeza elimu ya mtu lakini naweza kuamini kwamba chadema walikuwa hawajiandaa kwenda kushika dola.
1. Ikitokea Rais akienda safari makamu wa Rais darasa la saba ndiye atakaimu nafasi yake
2. Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu au kupoteza sifa za uchaguzi basi makamu wa rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano.
3. Makamu wa Rais huyu ndiye atakutana na viongozi na wageni wa kimataifa katika majukumu yake na kujadili masula mbalimbali yanayohitaji tafakari ya kina.
4. Endapo itaonekana kuwa Rais hawezi kumudu kazi zake kwa sababu ya maradhi ya mwili na akili basi itahesabika kwamba kiti ya Rais ki wazi, kazi na shughuli za Rais zitatekelezwa na makamu wa rais.
Je, Dr Slaa kamkubali darasa la saba ili kushika hatamu za uongozi peke yake au anahitaji mtu wa ndio mzee.
Je, jambo hili haliwezi kuathiri uchumi wetu?
Je Makamu darasa la saba ana sifa zote za kumudu changamoto za dunia ya utandawazi?
Tuendelee na mada yetu ya mgombea mwenza wa chadema.

Ingawa mimi sitetei kuwapo kwa viwango vya kielimu katika nafasi za kisiasa (a terribly undemocratic way of excluding a huge chunk of our population from leadership positions, racist white americans used this tactic to exclude blacks from voting in the pre-civil rights era) lakini pia nitataka kadiri mtu elimu yake rasmi inapozidi kuwa ndogo, ndipo aweze kusema ana kitu kingine cha kutuonyesha kufidia hilo pengo la elimu rasmi. Kama unataka kutuongoza tuonyeshe mchango wako utatoka wapi.
Inawezekana kabisa kuna watu wana akili kama majini, lakini hawakupata fursa kwenda shule kwa sababu kwa mfano, uongozi waliuanza tangu wadogo katika familia zao, na badala ya kuamua kwenda shule wakaona ni bora wajitoe muhanga kusaidia familia kwa kufanya kazi.Kwangu mimi mtu akiniambia sikuenda shule kwa sababu hii naona kashapasi mtihani wa kwanza wa uongozi. Palipokuwa na haja ya mtu kujitoa muhanga kwa familia yake na kuweka matakwa yake binafsi nyuma, aliweka matakwa ya familia mbele, mtu kama huyu kwangu namuona anajua kujitoa na uongozi ni shughuli ya kujitoa, Kwa hiyo mimi sina tatizo sana na kukosa elimu rasmi, nina tatizo na ujinga.
Kwa kuwa pia naamini kuna tofauti kati ya elimu na elimu rasmi, na kwamba si kila mwenye elimu rasmi ana elimu na si kila mwenye elimu ana elimu rasmi, sitataka kufanya elimu rasmi iwe kigezo cha kumnyima mtu hata urais. Tumeona ma giant wa elimu rasmi kama kina Dr. Fernando Henrique Cardoso, msomi mkubwa tu aliyeheshimika kimataifa, alivyoshindwa kumudu mikiki ya uongozi hususan katika uchumi nchini Brazil, na pia tukaona jinsi gani Luiz Inacio Lula Da Silva mtu ambaye hana elimu rasmi ( aliacha shule kuisaidia familia yake) ambaye kaja kuiinua Brazil sasa imekuwa katika lile kundi la nchi zinazotajwa sana kwa maendeleo ya kiuchumi ( BRIC, Brazil, Russia, India, China). Kwa hiyo elimu rasmi kwangu mimi si kigezo cha kumzuia mtu mwenye upeo na rekodi yenye kuonyesha mafanikio.
Lakini swali linabakia, mgombea wa CHADEMA ana uzoefu gani? Tukiacha suala la elimu rasmi, na kusema tutafute pengine ambapo anaweza kuwa na mchango mkubwa, anaweza kutuambia ana mchango gani aliotoa? Tunajua marehemu Kawawa hakuwa na elimu rasmi ya kutisha sana, hakuwa na shahada ya chuo, lakini alikuwa na uzoefu wa kufanya kazi na kuongoza vyama vya wafanyakazi. Huyu mgombea wa CHADEMA ana uzoefu gani?
Wamarekani wana msemo wao, "What does he bring to the table ?"
Uzoefu ataupata kwa Slaa atakapo kuwa Rais!
itabidi nimuulize huyu mtoto:
![]()
chadema hakikubaliki zanzibar, na ndio maana wamehangaika sana kutafuta mtu wa kuwa makamo wao wamekosa.
hii inaonyesha kuwa chadema ni chama cha upande mmoja na si cha kitaifa