Ila historia ya Miguna Miguna haijakamilika bila kurudi nyuma hadi enzi zile za Moi. Alipokuwa kiongozi wa wanafunzi University of Nairobi, UoN, hapo ilibidi atoroke Kenya kwa sababu ya vijana wa Moi, polisi wa kitengo cha Special Branch. Enzi hizo wakikudaka uhai wako kwishney. Mwili wako unaokotwa Ngong' Forest! Baada ya serikali ya nusu mkate kufanikishwa Miguna alikuwa mshauri wa Raila. Lakini walikosana miaka kadhaa baadaye alipofutwa kazi. Hapo ndo alianza majungu hadi akaandika vitabu viwili vya kumponda na kumtusi Raila. Humo ndani kulikuwa na siri kuhusu Raila, ufisadi, ulaji rushwa, hadi na Raila alivopenda michepuko. Ilibidi atoroke tena Canada kwasababu vijana wa chama cha Raila, ODM karibu wamuue. Vitabu venyewe ni Peeling back the mask na Kidneys for the King.