Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Kamati Kuu ya CHADEMA kupitia ofisi ya Katibu Mkuu imetangaza Majina ya watu wanaoaminika sana miongoni mwa wengi, ambao wameteuliwa kusimamia Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Kumbuka kwamba hawa waliochaguliwa ni watu ambao uadilifu wao hautiliwi mashaka na yeyote.
Miongoni mwao yumo Mzee Kasyupa Lumuli Alipipi, Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kyela na Waziri Mdogo wa Kilimo enzi za Nyerere (siku hizi mnaita Naibu Waziri)
Soma Pia: Mnyika ataja majina ya watakaosimamia mikutano ya kitaifa ya uchaguzi wa CHADEMA
Kasyupa ni Msomi na Muadilifu asiyeogopa kusema Ukweli, ndiye Mbunge aliyekuja kuiweka Kyela kwenye Ramani ya Tanzania kwa kupigania Maendeleo yake, Ni Mcha Mungu wa Kweli.
Nilimfahamu nikiwa mtoto mdogo alipokuja kufanya Kampeni kwenye kijiji alichokuwa anaishi Mjomba wangu Mwaka 1980, Ilikuwa maeneo ya Ipande, Kijiji cha Bukinga mbele kidogo ya Ipinda karibu na kijiji cha Njugiro, zilikuwa enzi za Chama kimoja, ambako alipambana na Mgombea mwingine aliyeitwa Mwakipesile, Kasyupa Alishinda. Kampeni zile zilikuwa kabambe na zilifanyika kwenye eneo maarufu lililoitwa Kwa kinyakyusa (PA MPIKI KIMBWALA) au MTI KIMBWALA kwa kiswahili, Kwenye mti huu paliaminika kuwa na Maajabu mengi hasa kwa waliokuwa wanaamini Ushirikina (Habari ya mti huu itakuja wakati mwingine)
Sina shaka na uadilifu wa mzee huyu ambaye mara ya mwisho alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chadema Kyela kabla ya kustaafu Ni baraka sana kwa Mzee huyu kuwa hai hadi leo.
Zaidi Msikilize hapa