yeddy guyy
JF-Expert Member
- Mar 31, 2015
- 627
- 489
Arthur Schopenhauer (22
Februari 1788 - 21 Septemba
1860) alikuwa Mwanafalsafa wa Ujerumani. Yeye anajulikana kwa kazi yake ya
1818 (The World as will and Representation) "Dunia kama wito na Uwakilishi" (kupanuliwa
mwaka wa 1844), ambako
anafafanua ulimwengu wa
matukio kuwa uzao wa dhamira
yakimetafizikia ambayo ni kipofu na isiyotosheka. Kutoka
kwa dhana ngambo ya bara la
uzoefu (Transendental
idealism) ya Immanuel Kant, Schopenhauer alibuni mfumo
wa kimetafizikia na wa kiMaadili ambao unaokana mungu ambao umeelezewa kuwa mfano wa
falsafa za uhasi wa maisha
(philosophical pessimism).
Alikataa falsafa za rika lake za
dhana kwamba ulimwengu
ulitegemea michakato ya kikakili kwa kuwepo kwake;
dhana zilizotawala falsafa za
Ujerumani Karne hio(German
Idealism). Schopenhauer
alikuwa miongoni mwa wasomi
wa kwanza katika falsafa ya Magharibi kushiriki na
kuthibitisha mambo muhimu ya
falsafa ya Mashariki (kwa
mfano, utawa, ulimwengu- kama-kuonekana), baada ya
kufikia hitimisho sawa kama
matokeo ya kazi yake ya
falsafa. Ingawa kasi yake haikupata
umaarufu wakutajika wakati
alikua hai, Schopenhauer
amekua na ushawishi mkubwa
baada ya kifo chake kupitia
kazi zake katika nyanja kadhaa, zikiwemofalsafa, fasihi
na sayansi. Maandishi yake juu ya esthete,
maadili na saikolojia ilikua na
ushawishi wa mkubwa kwa
wasomi na wasanii wengi wa
karne za 19 na 20. Wale
wamemtaja nikama Friedrich Nietzsche, Albert Einstein Richard Wagner, Leo Tolstoy, Ludwig Wittgenstein,
Erwin Schrödinger, Otto
Rank, Gustav Mahler, Joseph
Campbell, Carl Jung, Thomas
Mann, Emile Zola, George
Bernard Shaw, Guy de Maupassant, Jorge Luis
Borges na Samuel Beckett. Fikira Falsafa ya
"wito" Makala kuu: Dunia kama wito,
na Uwakilishi Lengo muhimu la
Schopenhauer ilikuwa
uchunguzi wake wa motisha ya
mtu binafsi. Kabla ya
Schopenhauer, Hegel alikua
amemaarufisha dhana ya Zeitgeist, dhana kwamba jamii ikona fahamu unganifu ya
pamoja ambayo inayosafiri kwa
njia teule, na inatawala vitendo
vya wanachama wake.
Schopenhauer, msomaji wa
Kant na Hegel Wote, alikashifu dhana zao za mantiki chanya
(Logical optimism) na imani
kwamba maadili ya mtu binafsi
inaweza kuongozwa na jamii au
sababu tupu. Schopenhauer
alishikilia imani kuwa binadamu alipata motisha kwa msingi ya
uchu na dhamira zao wenyewe
au witoe zum Leben ( "wito wa
kuishi"), ambayo yote ya
wanadamu huelekezwa. wito,
kwa mujibu wa Schopenhauer, ni kile Kant alichoita "kitu-ndani-
yenyewe". [39] Kwa Schopenhauer, tamaa ya
kibinadamu haikuwa na maana,
haijulikani, haielewi, na, kwa
upanuzi, hivyo hatua zote
zakibinadamu zinaambulia
patupu. Einstein alifalisi maoni haya kama ifuatavyo: "Mtu
anaweza kufanya kile
anachotaka, lakini hawezi wito
kile anachotaka." Kwa maana
hii, alizizingatia kanuni ya Fichte
yaulimwengu akili-tegemezi: "Dunia ni kwa raia." Dhana hii
umewasilishwa jinsi kwamba,
hutumika moja kwa moja kwa
kubuni mtazamo wa kimaadili,
hii ni kinyume na Descartes na
Berkeley waliozingatia masuala ya kiepistemologia pekee yake.
Kwa mujibu wa Schopenhauer,
wito ni nguvu kipofu ambayo
inatawala,sit u matendo ya watu
binasfi, ihali maumbile yote
ulimwenguni – na ni uovu ambao unapasawa kumalizwa na
majukumu ya wanadamu:
utawa na usafi wa moyo [40].
Ametambuliwa na kati moja ya
mistari ya ufunguzi maarufu
zaidi katika falsafa: "Dunia ni uwakilishi wangu." Friedrich
Nietzsche aliathiriwa sana na
wazo hili la wito, ingawa
hatimaye aliukataa. Sanaa na esthete Makala kuu: esthete ya Arthur
Schopenhauer Kwa mujibu wa Schopenhauer,
tamaa ya binadamu, "wito", na
uchu husababisha mateso au
maumivu. Njia ya muda mfupi
ya kuepuka maumivu haya ni
wa utafakari wakiusthete (kwa njia inayofanana na
"Usablimashaji" wa Zapffe). Utafakari huu wakiusthete
unaruhusu mtu kuepuka
maumivu-hata hivyo kwa muda
mfupi-kwa sababu hukomboa
mtu kutokana kuona dunia
kama tu mawasilisho. Badala yake, mtu husita kuangalia
dunia kama kitu cha
maonyesho (kama raia chini ya
katiba ya Kanuni za Misingi
Yakutosha, wakati, nafasi na
usababishi) ambapo mtu hupata kutengwanishwa; bali mtu
anapata kunganishwa na
anakua mmoja na maonyesho: "mtu hataweza tena
kutenganisha mtazamaji
kutoka kwa
mtazamo" (Dunia kama wito, na Uwakilishi, sehemu ya
34). Kutokana na kuzamishwa huku, mtu haijioni tena kibinafsi
kama anayekabiliwa na mateso
duniani kwa sababu ya uchu
wake badala yake, anakua
“raia wa ujuzi” kwa mtazamo ambao ni “safi, huru kutoka wito, na wakati”( kifungu cha 34) ambapo kiini, "mawazo", ya dunia huonyeshwa. Sanaa ni
dhana-tumizi zinazofuta huu
utafakari mfupi wakiusthete
ambapo inajaribu kuonyesha
mtu amezamishwa ndani ya
malimwengu, na hivyo hujaribu kuonyesha kiini / mawazo safi
ya ulimwengu. Muziki, kwa
mujibu wa Schopenhauer,
ulikuwa ni aina safi kabisa ya
sanaa Kwa sababu ilikuwa
inaonyesha taswira ya wito wenyewe bila kuenekana kama
raia chini ya Kanuni ya Misingi
za Kutosha , hivyo kama kitu
kimoja. Kulingana na Daniel
Albright, "Schopenhauer alifikiri
kwamba muziki ndiyo pekee ya sanaa ambayo haikunakili
mawazo, badala yake ililchukua
mfumo wa wito wenyewe." Alizingatia muziki kama huru
kutoka wakati, lugha
yakiulimwengu inayojulikana
kila mahali, ambayo inaweza
kuchanjia mataifa yote na
uchangamfu, ikiwa imechukua mafuatano ya sauti maarufu. Maadili Nadharia ya maadili ya
Schopenhauer ilipendekeza
kwamba kuwa ni huruma tu
ambayo inaweza kuendesha
vitendo vya maadili. Kwa
mujibu wa Schopenhauer, huruma peke yake ndio zuri
katika kitu cha matendo, yaani,
hawawezi kuongozwa na
tumaini la matumizi yakibinafsi
au hisia ya wajibu. Wanadamu
pia wanaweza kuongozwa na ubinafsi , ufisadi na chuki.
Vitendo vya ubinafsi na ufisadi
ni zile ambazo huongozwa na
masilahi binafsi, tamaa ya
taanasa au kujinufaisha.
Schopenhauer aliamini mengi ya matendo yetu ni ya darasa
hili. Matendo ya chuki ni tofauti
na matendo ya kibinafsi. Kama
ilivyo katika matendo ya
huruma, haya haijalenga
matumizi au manufaa ya mtu kibinafsi. Lengo la matendo
haya ni kusababisha uharibifu
kwa wengine, bila kujipatia
faida binafsi. Aliamini, kama
Swami Vivekananda katika
umoja wa wote na nafsi na pia aliamini kwamba ubinafsi ndio
asili ya maumivu na migogoro,
kwamba kupunguza ubinafsi
ndio inaunda mipaka ya kanuni
za maadili. Adhabu Kwa mujibu wa Schopenhauer,
Wakati sisi hufanya uamuzi,
"Sisi hudhani kwamba kama ni
sharti uamuzi huo ulitanguliwa
na jambo fulani ambapo ulipata
kuibuka kutoka, na ni ile tunaitaita ‘msingi’ au ‘sababu’,
au kwa usahihi zaidi ‘nia’, ya
hatua iliyotekelezwa.”
Uchaguzi haufanyiki kwa
uhuru. Matendo yetu hayawezi
banduka na yameshapangwa mapema kwani "kila binadamu,
hata kila kilicho hai, baada ya
nia imeonekana, lazima apate
kufanya hatua ambayo ni ya
kipekee kwa mujibu wa tabia
yake aliyozaliwa nayo na taratibu zisizobadilika." Hatua
ya fulani dhahiri lazima ipate
kutokea wakati ambapo nia
maalum inaathiri tabia ya mtu
ambayo amepewa na
haibadiliki. Serikali, Schopenhauer alidai, huadhibu
wahalifu kuzuia uhalifu wa
baadaye. Inafanya hivyo kwa
Kuweka "kando na kila nia
inaweyozekana ya kufanya
uhalifu nia ya nguvu zaidi ya kutoifanya, katika adhabu
isiyoepukika. Kwa hiyo, kanuni
ya jinai ni kama rejista kamili
iwezekanavyo ya nia-pinganifu
ya vitendo vyote jinai
zinazoweza fikirika..” ... sheria na utimilifu wake,
yaani adhabu, huelekezwa
kimsingi kwa siku zijazo, si
kwa siku za nyuma. Hii
inatofautiana adhabu kwa
kulipiza kisasi, kwani kulipiza kisasi kunahamasishwa na
kilichotokea, na hivyo kwa siku
za nyuma kama vile. Marejeleo
yote ya kujibu mashambulizi
kwa kusababisha maumivu
fulani kwa wengine bila kuzingatia kokote kwa siku za
usoni ni kulipisha kisasi, na
haiwezi kua na lengo zaidi bali
ile faraja kwa yale maumivu
mtu amevumilia kwa kuona
mateso yeye amemsababishia mwenzake. Kitu kama hicho ni
uovu na ukatili, na haiwezi
kuhalalishwa kimaadili ..... Nia
ya adhabu.. ni kuepusha kutoka
kwa uhalifu… Nia na azimio ya
siku za usoni ndio inatenganisha adhabu na
kulipisha kisasi, na kuadhibu
ikona hii maana wakati tu
inaitwa ili kutimiza sheria fulani.
Ni kwa njia hii tu ndio itaweza
kutumika kwa namna isoyoepukika au kukosoleka
kwa kesi zote za usoni; na
hivyo inapea sheria nguvu ya
kukomesha.. Je! Adhabu ya kifo zapaswa
kuhalalishwa? “Ili kulinda
maisha ya raia,”Schopenhauer
alijibu, “adhabu ya kifo lazima
zihitajike”. “Muaji, ambaye
amehukumiwa kifo kwa mujibu wa sheria lazima atumike kama
chombo, na haki kabisa.
Ilikuzingatia usalama wa umma,
ambao ndio wajibu mkuu wa
serikali, na umepata kutishiwa
na mtu huyu; kwa kikweli umepuuliziwa kama hukumu
haijatekelezwa. Muuaji, maisha
yake, utu wake, lazima awe
chombo cha kutekeleza sheria,
na hivyo rejesha usalama wa
umma.” Schopenhauer alikataana na wale waliotaka
adhabu ya kifo itupiliwe mbali.
“Wale ambao wanaopendekeza
ikomeshwe wanapaswa
kupewa jibu:’ Kwanza toa
mauaji kwa dunia, na kisha adhabu ya kifo itafuata” Watu, kulingana na
Schopenhauer, hawawezi
kuimarishwa. Wanaweza
kushawawishika tu na nia
zenye nguzu zinazoshinda nia
za uhalifu. Schopenhauer analitangaza kwamba
“ubadilishaji wa maadili kwa
kikweli haiwezekani kabisa, ila
tu zuia njia kwa tendo..” Alisema kwamba mafunzo haya
hayakuwa na asili nayeye.
Hapo mbeleni ilionekana kwa
maandishi ya Plato, Seneca,
Hobbes, Pufendorf, na Anselm
Feuerbach. Schopenhauer alitangaza ya kwamba maadishi
haya yalichafuliwa na makosa
yaliyofuata na kwa hivyo ilikua
na haja ya ufafanuzi. Dhana ya
kisiasa na ya
kijamii Siasa Siasa za Schopenhauer
zilikuwa, kwa sehemu kubwa,
marejeleo ya mfumo wake wa
maadili (ya jamii ilipata sauti
kwa Die beiden Grundprobleme der Ethik, inayopatikana kwa kiingereza
kwa vitabu viwili, On the Basis of Morality na On the Freedom of the wito ). Maadili pia ilimiliki karibu robo ya kazi
yake kuu, Dunia kama wito na Uwakilishi. Katika maoni ya mara kwa
mara ya siasa katika kazi zake
za Parerga and Paralipomena na Manuscript Remains, Schopenhauer anajieleza mwenyewe kama
mpendekezi wa serikali finyu.
Cha mno, alidhani, ni kuwa
serikali inapaswa “kuwacha kila
mtu huru ajitafutie wokovu
wake mwenyewe”, na ikiwa serikali itasita kudoea au
kuingilia haya, yeye
alipendekeza zaidi “afadhali
kutawaliwa na simba kuliko
panya wenzake”- hiyo
nikumaanisha, na mfalme, kuliko kiongozi wa demokrasia.
Schopenhauer aliunga mkono
maoni ya Thomas Hobbes ya
umuhimu wa serikali, na wa
utendakazi wake, kuchunga
mielekeo yetu ya uharibufu ambayo ni ya undani na
imeambatana na asili ya aina
yetu. Yeye bado alitetea tawi
huru za utunga-sheria,
mahakama, na utekelezaji za
nguvu, na aliona mfalme kama kipengele huru ambacho
kinaweza tekeleza haki
(anamaanisha katika matumizi
ya kila siku, sio kwa maana ya
kikosmologia). Alitangaza
ufalme kama “kile ambacho ni cha hali ya kawaida kwa
binadamu” kwani “uerevu daima
chini ya serikali ya ufalme
umekua ukipata nafasi bora
zaidi kupiku adui wake mkuu,
ujinga” alihujumu ujamhuri kama “yasiyo asili kwani
inasusia hatua za uerevu
wajuu, sanaa na sayansi” Utata wa
nungunungu Utata wa nungunungu, ni
fumbo wa changamoto
zinazoathiri umoja na urafiki wa
watu. Huelezea hali ambayo
jamii ya nungunungu hujaribu
kusongeana karibu pamoja ili kugawana joto katika msimu
wa baridi. Lakini hupata
kwamba zinaumizana na
mishale yao mikali, hivyo
wanapaswa kubaki mbali.
Ingawa zote zilikua na nia ya uhusiano wa karibu
wakusaidiana, hii huenda
isifanyike, kwa sababu
zisizoepukika. Arthur Schopenhauer alitumia
fumbo hili kuelezea dhana yake
kuhusu hali ya mtu binafsi
katika uhusiano wa ujamii na
wengine. Utata wa nungunungu
huonyesha kwamba ingawa nia njema, umoja na urafiki wa
kibinadamu hauwezi fanyika
bila kiasi fulani cha kuumizana,
na huongoza watu kwa tabia
za kujitahadhari na husiano
hafifu. Utata wa nungunungu, unapendekeza kuwa mpole na
kutumia wastani katika
uhusiano na wengine ili
kujichunga, na pia kama njia ya
kuzingatia wengine. Utata wa
nungunungu umetumiwa na mwanasiakologia Sigmund
Freud kueleza upweke na
dhana za kujitenga. Fumbo hii ilitoka kwa Parerga und Paralipomena, Volume II, Sura ya XXXI, Sehemu ya 396 Nungunugu kadhaa
walikaribiana pamoja kutafuta
joto katika siku ya baridi; lakini,
vile walianza kuchomana na
mishale yao, walilazimika
kutawanyika. Lakini baridi iliwafukuza na kuwaleta tena
pamoja, ambapo jambo lile lile
lilifanyika tena. Hatimaye,
baada ya mizunguko mingi ya
kusogeana na kutawanyika,
waligundua ni heri kubakisha nafasi kiasi kati yao. Kwa njia
sawa, mahitaji hufanya
nungunungu za kibinadamu
kuletwa pamoja kwa ujamii,
lakini hujipata wakisukumana
na kuchomana na pembe za sifa mingi tofauti zinazopingana
ambazo ziko kwa asili yao.
Umbali wa wastani ambao
hatimaye wanagundua ndio hali
wanayoezaishi nayo, ni kanuni
za upole na tabia mzuri; na wale wanopita mpaka huu
wanaambiwa –kwa kiingereza-
“keep your distance”. Kwa
mpango huu mahitaji ya joto
inatoshelezwa wastani tu; lakini
pia watu hawadungwi. Mtu ambaye akona joto ndani yake
anapendelea kubaki inje,
ambapo hatadunga mtu wala
hata dungwa yeye mwenyewe.