Raia wa Nijeria aliyepata umaarufu kwa kulia
Umaarufu unakuja kwa aina tofauti wengine unakuja kwa kunywa pombe kama ilivyokua kwa Piere, Mwingine unakuja kama huu wa ujugu baada ya kukoment kwenye page za Aston Vila ha ha !
Anaitwa #Oladee kijana mzaliwa wa Nigeria. Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Ilorin nchini Nigeria.
Mwaka 2009 Oladee alipata mkasa mkubwa ambapo baadaye mkasa huo ukamfanya kuwa mtu maarufu. Alipewa Naira 200 sawa na Tsh. 1,200 na bibi yake kununulia mahitaji ya chakula
Aliongozana na rafiki yake aliyemshawishi acheze Kamari. Hela yote aliyopewa ikaliwa kwenye kamari (bet), hapo bwana Oladee alipoanza kulia ili arudishiwe hela yake
Walimpiga picha na kichwa chake kinatumika kwa kupachikwa kwenye picha tofauti tofauti za kuchekesha
Watu wanamwita kichwa kinachotembea bila ‘passport’ kwa sababu picha yake hii imesambaa Dunia nzima na watu wanaihariri ‘edit’ kwa kuifanyia vituko #motratv