Mjue Rais wa Ethiopia Sahle-Work Zewde atakayeitembea Tanzania 25 January 2020

Mjue Rais wa Ethiopia Sahle-Work Zewde atakayeitembea Tanzania 25 January 2020

Hakuna udhaifu katika kutengua. Usipotekeleza majukumu yako kama kiongozi utatenguliwa tu na wengine watachukua nafasi yako. Tanzania ina watu millioni 66 ikibidi kila mtu ataongoza tu tutabadilishana uongozi mpaka kieleweke.
 
Karudisha sanduku la Agano?
Inasemekana lipo kati ya ngorongoro creator au mlima Kilimanjaro na hii ndiyo baraka ya nchi yetu.

Ndani ya hilo sanduku mna zile mbao mbili Mungu alizoandika amri pia kuna fimbo ya haruni iliyochipuka na kopo au bakuli la dhahabu lenye mana.
 
Inasemekana lipo kati ya ngorongoro creator au mlima Kilimanjaro na hii ndiyo baraka ya nchi yetu.

Ndani ya hilo sanduku mna zile mbao mbili Mungu alizoandika amri pia kuna fimbo ya haruni iliyochipuka na kopo au bakuli la dhahabu lenye mana.
Mshekuu hizo ni story tuu za vijiwen hakuna kitu kama hicho
Kumbuka pia dini ni biashara kama biashara nyingine
 
Malkia wa Shaba alimtembelea mfalme Solomon alimpelekea zawadi za vito vyenye gharama kubwa.

Inasemekana mfalme alimtunuku malkia zawadi ya ujauzito.

Ukisoma maandiko kadhaa huyo kijana mwana wa mfalme miaka fulani alienda kumtembelea babaye, wakati huo Solomon akiwa mzee wa miaka mingi.

Kijana alikwapua lile sanduku la agano la Mungu akarejea kwao Ethiopia, mwisho akafanya utalii Tanzania na lile sanduku akaliacha Tanzania,

Ndiyo hivyo, unabisha nini, niambie wewe

Karibu nyumbani mgeni wetu.
Mmh hili tutalitegemea pia ujio huuu Wa huyu malikia(rais) mwingine Wa Ethiopia
 
Ethiopia wanatumia Mfumo wa uongozi kama wa India, Ujerumani, Israel nk ambapo Rais anakuwa Mkuu wa Nchi tu kwa hiyo cheo chake ni cha heshima (Ceremonial) tu, Serikali inaongozwa na Waziri Mkuu ambaye anaunda Baraza la Mawaziri na anatokana na Chama chenye Wabunge wengi Bungeni.

Mfumo wa kwetu ambao haufai kabisa, Rais ndio kiongozi wa Nchi na Serikali akisaidiwa na Makamu ambaye ni Rais mtarajiwa endapo Mungu atampenda zaidi Rais akiwa madarakani. Rais ndiye anateua Mawaziri na Waziri Mkuu ambao lazima wawe Wabunge na ndio wanaunda Baraza la Mawaziri na Waziri Mkuu akiwa Mkuu wao na kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni.

Rais wa kwetu ndo pia anateua watumishi wote muhimu Serikalini na Mashirika ya Umma ndio maana nchi ikipata Rais dhaifu mambo mengi yanakwama kwa sababu wateule ni wengi mno kwa mtu mmoja kufuatilia utendaji kazi wao. Pamoja na kuwa ni wajibu wa mteuwa kuteua na kutengua (hire & fire), lakini teua/tengua zikizidi unakuwa ni uthitisho wa udhaifu wa mteuwa.
umejtahid kweli kufafanua mwisho umeharibu kuelezea
 
Back
Top Bottom