Mjue RICHARD SPIKES mgunduzi wa automatic gearbox

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
RICHARD SPIKES: MVUMBUZI WA INJINI ZA GARI ZA KISASA!!

1666146596288.png

Wengi wetu leo tunaendesha gari za kisasa zenye kubadili mwendokasi bila kuhitaji kubadili gea(automated gear transmission systems), na wengi naamini aghalabu wanapofikiri nani aliwezesha hilo' basi taswira ya mzungu fulani inawajia kichwani mwao kama ndiye Mvumbuzi wa mfumo huo wa Injini ya gari!

Injini za gari za mwanzo kabisa zilibuniwa na wavumbuzi wa ulaya magharibi wakitajwa kwa uchache na asiwepo hata mmoja mwenye kubeba sifa yote peke yake, kwa hiyo wanatajwa akina Karl Benz Mvumbuzi wa Injini za Benz na wenzie akina Wilhelm Maybach na Rudolf Diesel ambaye ndiye aliboresha Sana injini za dizeli, uvumbuzi huu ukishamiri Sana katika miaka ya 1800s!

Henry Ford anasifika kwa kuwa binadamu wa kwanza mwanamageuzi wa viwanda kuweza kutengeneza gari zitumiazo mafuta(diesel engine) kwa wingi na hivyo kuleta mapinduzi makubwa katika matumizi ya gari kwa usafiri badala ya magari yakokotwayo na farasi au punda!!

Hivyo mpaka mwaka 1932 magari yaliyokuwepo yalitumia mfumo wa kubadili gea kwa mkono(manual transmission system) lakini ni wakati ambapo Mvumbuzi mwenye asili ya Afrika aitwaye Richard Spikes alipopata wazo la uvumbuzi ingilizi kwa kubuni injini yenye uwezo wa kubadili gea yenyewe akilenga kumpunguzia ugumu dereva wa kudhibiti na kuendesha gari!!

Richard Spikes(pichani) alizaliwa Oktoba 2 mwaka 1878 mjini Dallas Texas kwa familia ya wakulima na hakuna historia inayoelezea kuhusu elimu akisemekana kupata elimu ya ufundi kwa kufanya kazi katika karakana za kukarabati treni mjini Dallas.

Mwaka 1932 Richard Spikes aliweza kutengeneza injini ya kwanza ya gari inayoweza kujibadili gea yenyewe kwa dereva kusukuma pedali ya mafuta pasipo haja ya kubadili gea, akapewa hati ya kutambua uvumbuzi wake namba 1,889,814 mwaka 1933 na shirika la hati miliki la Marekani!

Mwaka 1907 Richard Spikes alivumbua mitungi ya kuuzia mvinyo(beer keg) inayotumika kwenye mabaa na hoteli kubwa duniani hata Sasa! Baadae aliiuza hati miliki ya uvumbuzi huu kwa kampuni la vinywaji la Milwaukee Bottling Company.

Mwaka 1910, Richard Spikes alivumbua meza za kisasa zenye uwezo wa kujifungua na kufunga za mchezo wa biliadi maarufu pool table!
Mwaka 1962 Richard Spikes alivumbua Mfumo salama wa kufunga na kufungua breki za magari maarufu ABS (Automated Braking System)!

Richard Spikes alifariki mnamo January 22,1965 mjini Los Angeles akiwa na miaka 86!
 
JamiiForums, hivi huu uzi kwanini usiwekwe kwenye jukwaa la magari mnauweka kwenye jukwaa la historia? Je huyu mgunduzi ni sawa na kina Rashidi Mfaume Kawawa?
Hebu jaribuni kuwa weledi, hamjautendea huu uzi heshima yake.
This invention is still alive, iweje muiweke kwenye jukwaa la historia?
Msifananishe sayansi na historia please.
 
Historia hutengenezwa kwa kufasri matendo ya binadamu hasa katika uzalishaji na uzalishanaji.Kila tukio kwa wakati wake huwa na historia yake.Matukio ya kihistia huitwa historical facts.Kila tukio lazima lifanyiwe interpretation.Hii ni tafsiri ya matukio ya binadamu na kwakuwa ni historia hapa lipo ni swadakta kabisa.

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
JamiiForums, hivi huu uzi kwanini usiwekwe kwenye jukwaa la magari mnauweka kwenye jukwaa la historia? Je huyu mgunduzi ni sawa na kina Rashidi Mfaume Kawawa?
Hebu jaribuni kuwa weledi, hamjautendea huu uzi heshima yake.
This invention is still alive, iweje muiweke kwenye jukwaa la historia?
Msifananishe sayansi na historia please.
Sayansi Haina historia kumbe

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
JamiiForums, hivi huu uzi kwanini usiwekwe kwenye jukwaa la magari mnauweka kwenye jukwaa la historia? Je huyu mgunduzi ni sawa na kina Rashidi Mfaume Kawawa?
Hebu jaribuni kuwa weledi, hamjautendea huu uzi heshima yake.
This invention is still alive, iweje muiweke kwenye jukwaa la historia?
Msifananishe sayansi na historia please.
Sayansi Haina historia kumbe

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
RICHARD SPIKES: MVUMBUZI WA INJINI ZA GARI ZA KISASA!!

View attachment 2391602

Wengi wetu leo tunaendesha gari za kisasa zenye kubadili mwendokasi bila kuhitaji kubadili gea(automated gear transmission systems), na wengi naamini aghalabu wanapofikiri nani aliwezesha hilo' basi taswira ya mzungu fulani inawajia kichwani mwao kama ndiye Mvumbuzi wa mfumo huo wa Injini ya gari!

Injini za gari za mwanzo kabisa zilibuniwa na wavumbuzi wa ulaya magharibi wakitajwa kwa uchache na asiwepo hata mmoja mwenye kubeba sifa yote peke yake, kwa hiyo wanatajwa akina Karl Benz Mvumbuzi wa Injini za Benz na wenzie akina Wilhelm Maybach na Rudolf Diesel ambaye ndiye aliboresha Sana injini za dizeli, uvumbuzi huu ukishamiri Sana katika miaka ya 1800s!

Henry Ford anasifika kwa kuwa binadamu wa kwanza mwanamageuzi wa viwanda kuweza kutengeneza gari zitumiazo mafuta(diesel engine) kwa wingi na hivyo kuleta mapinduzi makubwa katika matumizi ya gari kwa usafiri badala ya magari yakokotwayo na farasi au punda!!

Hivyo mpaka mwaka 1932 magari yaliyokuwepo yalitumia mfumo wa kubadili gea kwa mkono(manual transmission system) lakini ni wakati ambapo Mvumbuzi mwenye asili ya Afrika aitwaye Richard Spikes alipopata wazo la uvumbuzi ingilizi kwa kubuni injini yenye uwezo wa kubadili gea yenyewe akilenga kumpunguzia ugumu dereva wa kudhibiti na kuendesha gari!!

Richard Spikes(pichani) alizaliwa Oktoba 2 mwaka 1878 mjini Dallas Texas kwa familia ya wakulima na hakuna historia inayoelezea kuhusu elimu akisemekana kupata elimu ya ufundi kwa kufanya kazi katika karakana za kukarabati treni mjini Dallas.

Mwaka 1932 Richard Spikes aliweza kutengeneza injini ya kwanza ya gari inayoweza kujibadili gea yenyewe kwa dereva kusukuma pedali ya mafuta pasipo haja ya kubadili gea, akapewa hati ya kutambua uvumbuzi wake namba 1,889,814 mwaka 1933 na shirika la hati miliki la Marekani!

Mwaka 1907 Richard Spikes alivumbua mitungi ya kuuzia mvinyo(beer keg) inayotumika kwenye mabaa na hoteli kubwa duniani hata Sasa! Baadae aliiuza hati miliki ya uvumbuzi huu kwa kampuni la vinywaji la Milwaukee Bottling Company.

Mwaka 1910, Richard Spikes alivumbua meza za kisasa zenye uwezo wa kujifungua na kufunga za mchezo wa biliadi maarufu pool table!
Mwaka 1962 Richard Spikes alivumbua Mfumo salama wa kufunga na kufungua breki za magari maarufu ABS (Automated Braking System)!

Richard Spikes alifariki mnamo January 22,1965 mjini Los Angeles akiwa na miaka 86!
ABS - Ant-Locking Braking System
 
Back
Top Bottom