Teko Modise
JF-Expert Member
- May 20, 2017
- 2,331
- 7,733
Wakati wengine wakikimbilia fursa ya mafuta baada ya kugunduliwa, yeye aliiona fulsa kwenye uchafu wa mafuta uliokuwa ukiwakera watu.
Anakumbukwa sana kwa kauli yake maarufu isemayo:
"Innovation doesn’t happen in laboratories; it’s discovered in the field."
Na hii ndiyo hadithi yake.
Mwaka 1859, huko Pennsylvania Marekani, baada ya mafuta kugunduliwa, wachimbaji walikumbana na changamoto moja kubwa. Kulikuwa na ute mzito wenye kunata uliokuwa unaziba mabomba na kusababisha vikwazo vingi kazini.
Ute huo wengi waliuita "Petroleum jelly" (Kwa maana kwamba ni by-product iliyokuwa ikitokana na mchakato wa uchakataji wa mafuta machafu, ili kuipata Petrol) ulionekana kuwa kero kwa wachimbaji wengi hivyo hawakupendezwa nao hata kidogo.
Lakini muda ulivyozidi kwenda, baadhi ya wachimbaji walianza kuwa na tabia ya kupaka jelly hiyo kwenye majeraha yao, wakidai inawasaidia kupona haraka.
(Ni kama vile mchezo wa watoto wa kuweka mchanga kwenye kidonda wakiumia wakidai inawasaidia kupona)
Kijana mmoja anafahamika kwa jina, Robert Chesebrough, aliyekuwa mwanakemia mdogo mwenye miaka 22 baada kusikia tetesi hizi na kuona jinsi wachimbaji walivyokuwa wakiitumia kwa majeraha na mikwaruzo midogo ili kupona haraka, aliamua kuchukua sampuli na kuanza kufanya utafiti zaidi.
Aliporudi nyumbani kwao Brooklyn, New York, Chesebrough hakuwa na wazo la kuanzisha biashara, yeye alikuwa na idea ya kufanya jelly ile iwe salama zaidi kwa wachimbaji na wafanyakazi kule mgodini.
Kwa kutumia elimu yake alisafisha jelly iyo na kugudua kweli kuna uwezekano wachimbaji wake walikuwa sahihi, akaanza kuiboresha kwa kuitenganisha (extracting) jelly hiyo hadi hadi alipoona inafaa kwa matumizi ndipo wazo la biashara likamjia, bidhaa yake akaipa jina Vaseline.
(Jina "Vaseline" lilichukuliwa kutoka kwa neno la Kijerumani "Wasser" linalomaanisha maji na "Eis" linalomaanisha mafuta au solid)
Kijana baada ya kupata final product ya bidhaa yake alikutana changamoto kubwa zaidi, watu walikuwa hawamuamini akisema kwamba bidhaa yake inaponya majeraha na kwamba ni salama kwa matumizi.
Tatizo hili lilimfanya kijana kutembelea nyumba kwa nyumba, ikitokea mtu amembishia, kijana alikuwa akijikata makusudi kwenye mikono yake na kutumia Vaseline kama tiba and then, akirudi siku ya pili kwa watu aliokutana nao ili kuwathibitishia kuwa kidonda kweli kinapona haraka.
Kidogo kidogo watu wakaanza kuamini kwenye bidhaa yake huku uzumi ukisambaa kwa watu wengi zaidi kuhusu bidhaa yake.
Hatimaye, mwaka 1870, Chesebrough alianzisha kampuni yake ya Chesebrough Manufacturing Company na akaanza kuuza Vaseline kama tiba ya ngozi na majeraha madogo.
Bidhaa hiyo ilipata umaarufu haraka sana, na ikawa bidhaa ya nyumbani inayotegemewa kwa madhumuni ya kutunza ngozi na kuponya majeraha.
Baada ya muda mfupi, Vaseline ikaanza kusambazwa kote Marekani na kisha kimataifa. Mafanikio ya kampuni hii yalikua kwa kasi na bidhaa hiyo ikawa maarufu duniani kote kwa karne nzima.
Kampuni ya Chesebrough Manufacturing Company baadaye ilinunuliwa na kampuni kubwa ya Unilever kwa takriban dola bilioni 3.1 mwaka 1986, katika makubaliano ya fedha taslimu ya $72.50 kwa hisa. Ikiwa tunazingatia mabadiliko ya thamani ya pesa kutokana na mfumuko wa bei, thamani hii leo ingekuwa kubwa zaidi.
Kwa sasa, Vaseline inajulikana na kutegemewa katika bidhaa za utunzaji wa ngozi, na Unilever inaendelea kutengeneza na kusambaza Vaseline kwa viwango vikubwa, ikiongeza mafanikio ya bidhaa hii katika soko la kimataifa.