Mjukuu Ukuienda Mbiguni una hela zako ukienda motoni una hela zako

Mtamile

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2011
Posts
2,838
Reaction score
1,275
Babu kaenda kumtembeza mjukuu wake kwenye makaburi ya kijiji;

BABU
: Unaona kaburi hili huyu jamaa alikuwa mtu, nilimkopesha fedha, akajitahidi sana kunilipa, kwa bahati mbaya alikufa huku namdai alfu hamsini. Nina uhakika huyu kaenda mbinguni alikuwa mtu mzuri sana.........wakaenda kaburi jingine
BABU: Sasa huyu alikuwa mshenzi sana alikopa laki yangu hakunilipa makusudi mpaka akafa na deni langu. Huyu lazima yuko motoni
MJUKUU: Dah babu ukifa una bahati kweli
BABU: Una maana gani na wewe?
MJUKUU: Yaani babu ukifa ukienda mbinguni kuna hela zako, ukienda motoni kuna hela zako
BABU: Mjinga mkubwa twende nyumbani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…