Mjumbe wa Bunge Maalumula Katiba, Ezekiah Oluoch, ameuchambua Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba nakutaja kitendo cha wajumbe wa Bunge hilo kutokugawiwa hati ya Muungano kuwamoja ya kasoro kubwa zinazoukabili.
Akizungumza katikamahojiano maalumu na gazeti hili jana, Oluoch alihoji mantiki ya wajumbe waKatiba kujadili Muungano, wakati hawana hati ya Muungano iliyosainiwa nawaasisi wake; Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume.
Mimi nililiona hilomapema, nikaenda kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema,nikamuuliza kama atagawa hati ya Muungano kwa wajumbe, lakini inaonekana hakunampango huo. Sasa tunajadilije Muungano wakati hatujui msingi wake, alihoji.
Oluoch alisema nguzo ya Bunge la Katiba niMuungano na kwamba matunda yake yataonekana kama kumewekwa mazingira mazuri yakuujadili.

