Mjumbe hauawi. Mwanamke huwa msafi kabla ya kuolewa, akiolewa mambo hubadilika

Joined
May 23, 2024
Posts
15
Reaction score
43
MJUMBE HAUWAWI.

Nimepitia comment kwenye hii post.

Wanaume wanamalalamiko mengi sana yenye tiija juu ya hoja hii.

Swali likanijia, je anaweza kufika Moshi na asifike kileleni?

Nikaendelea kusoma Comment, nanukuu mbili.

"Mwanamke ukianza naye anakuwa msafi na wa maana sana, muoe sasa utajutraaa. Anaanza kunuka yeye hadi kibuyu cha asali kinatoa shombo la utumbo" mimi haaa!

"Kumuoa tu, azae katoto kamoja, utajuta na kutamani umrudishie mtoto tumboni. Unaweza jikuta unakula ugali una zile chembe za pampasi. Jaribu kusogeza kochi kukiwa na mgeni, utajuta. Hapo muwe mnaishi chumba kimoja, utajikuta kila siku vibanda umiza kuangalia marudio ya mechi hata kama hupendi mpira"

Nikasemaje, shida ni kuwa, mabinti wengi wanasubiri waolewe ndo wawe wasafi, na wakiolewa kutwa nzima hawaogi, wanasubiri jioni mubaba anakaribia wanaingia bafuni na kujimwajia maji kama ndoo...
Wanasahau, hata Yanga kuchukua ubingwa mfululu mazoezi yalichangia sana.

Kwenye vitabu vyangu vya maarifa kwa mwanamke nimesisitiza sana uwajibikaji, kwako binafsi na kwa jamii yako.

Kama ni binti uko kwenu, na umezoea kukoga hadi utishiwe kunyimwa ubwabwa, tuna kikao.

Kama ni binti uko kwenu au umeanza maisha ila kufanya usafi mazingira yako ni ugonvi na taifa, Ukae kiti cha tatu kutoka mbele.

Kama ni binti, hutaki kujifunza namna ya kukoga na kuutunza mfumuko wako wa harufu hatarishi kaa nyuma kule.. ehee hapo hapo.

Unaamini kwenye ulozi, unaamini kibuyu chako bila kutiwa makorokoro hakitoi asali tamu.... pole, naomba ukae hapa mbele nikuombee.

Nimekwazika na hili wimbi la mabinti kujivunia madhara baada ya kuweka vitu huko ili wawe watamu. Wanaishia kuoza na wengine kunuka kusikokoma. Mbaya zaidi, hawasemi ukweli wanaficha maradhi, saratani inakuja kuwaumbua, badilikeni.

Mungu alivyokuumba alikupimia ladha kuliko mboga ya mpishi stadi. Alikutia chunvi na kila kiungo ulichohitaji kuwa mwanamke mtamu. Acha kujiloga, acha kujiumiza. Unahitaji tu kuwa msafi na salama, sio kwa ajili ya yoyote, ni kwa ajili yako wewe. Jipende basi!
Mwanaume aliyekuridhia, haitaji uweke shabu huko.
Hahitaji uweke madawa ya mvuto huko.
Hahitaji sijui vipipi, sijui vipapi. Unaweza kuongeza joto na mvuto na ladha yako kwa kuboresha mfumo wako wa maisha na maakuli.

Wewe ni wa muhimu sana.
Wewe ni wa thamani sana.
Usalama wako ni jukumu lako wewe.
Afya yako ni faida yako wewe.
Jilinde sana.
Jitunze pia.

Haya malalamiko kuhusu mabinti kuwa wachafu/ pengine si uchafu, ni madhara ya hekaheka za kuusaka utamu wa ziada.

Kama mwanamke unatakiwa kutambua tu,
"UNATOSHA HIVYO ULIVYO"
Jiboreshe tu kwa kujiongezea maarifa.
Soma vitabu vyangu vya maarifa kwa mwanamke. Na kwenye ishu ya usafi na utunzaji wa hazina yako. Soma kitabu cha KUNGWI.

Kuna mengi ya kuhangaikia ya kukupa faida na sio haya yatakayohitaji kula mtaji kuyakabili yakikubadilikia.

HAKIKISHA UNAKUWA SALÀMA.

NOTE:
Yapo magonjwa mengi yanayopelekea hitilafu huko kibuyuni, mengine ya kuambukizwa, mengine hutokana na mfumo mbaya tu wa ulaji. Mengine ni uchafu wa mazingira(vyoo) Mengine ni uchafu wa mwili, mengine ni madhara ya viambata sumu (cream/pombe/sigara) na mengine ndo hayo ya kutia mazaga huko.
Sambamba na hilo, kuna changamoto ya saratani ya mlango wa kizazi... uonapo dalili zisizo sawa, nenda hospitali, onana na dakitari, kuwa muwazi, kuumwa sio kitu cha kuonea aibu. Pata vipimo, Fuatisha matibabu kwa usahihi na mwisho jitunze..

Na kwa wenza wetu.

Uonapo utofauti kwa mkeo, kuwa chachu ya yeye kupata msaada. Wanawake huona noma sana kuwaambia wapenzi wao kuwa wanaumwa ikulu. Msaidie, wewe ni kiongozi wake na sio hakimu wa madhaifu yake. Na kama unampenda, na amekuwa mchafu, au akikupeleka mlimani anakuacha katikati mnunulie vitabu vyangu kuna namna utamsaidia bila kugombana naye.

Wanawake wanapitia vipindi vingi vya kukosa hamu ya kupanda mlima. Sababu zaweza kuwa nyingi na nyingine hata wao hawazijui. Mmotivate mkeo bro.

Kungwi wa kisasa
20240602_180511.jpg
 
Let me tell you Maina...

Uanamke kazi sana. Hata mazingira yakibadilika wewe unatakiwa ubaki vile vile. Shughuli tupu!!

Mimi ndio maana tulipopata tu mtoto nikamwambia babe, nataka wasaidizi wawili wa kazi. mmoja wa kusaidiana malezi ya huyu baby boy, wa pili wa kusaidiana kutunza nyumba na kupika. Nashukuru alinielewa, sasa nina muda wa kujijali mwenyewe, na kumjali na kumfurahisha yeye.
 
Jesus, mtoto mmoja wasaidizi wawili, una umri gan au una kazi gani labda una ulemavu? We ni mvivu na mchafu tusiende mbali
 
Aisee
 
Nafikiri ni jukumu lako wewe kama mwanamke kumtunza mwanao, kumhudumia mwanaume wako na mwisho ni lazima ujitunze wewe mwenyewe sababu huo ndio uanamke.
Yes, kutunza nyumba na usaidizi wa kazi za nyumbani ni vyema ukapata msaidizi, na ikiwa utaanza kwenda kazini yes, pia ni vyema ukapata wasaidizi wawili kwaajili ya mtoto"malezi na usaidizi wa kazi za ndani.
 
Let me tell you Maina...

Uanamke kazi sana. Hata mazingira yakibadilika wewe unatakiwa ubaki vile vile. Shughuli tupu!!

Mimi ndio maana tulipopata tu mtoto nikamwambia babe, nataka wasaidizi wawili wa kazi. mmoja wa kusaidiana malezi ya huyu baby boy, wa pili wa kusaidiana kutunza nyumba na kupika. Nashukuru alinielewa, sasa nina muda wa kujijali mwenyewe, na kumjali na kumfurahisha yeye.
Kwamba wewe binafsi huwezi hivyo vishughuli maana kujibalancena usafi ni mtihani hivyo unahisi utanuka?
 
Naweza ila mwisho wa siku nitakuwa nimechoka kama mbwa, jambo ambalo siliwezi na silitaki!

Life inatakiwa iwe “Minimum effort, Maximum Enjoyment”
 
Let me tell you Maina...

Uanamke kazi sana. Hata mazingira yakibadilika wewe unatakiwa ubaki vile vile. Shughuli tupu!!

Mimi ndio maana tulipopata tu mtoto nikamwambia babe, nataka wasaidizi wawili wa kazi. mmoja wa kusaidiana malezi ya huyu baby boy, wa pili wa kusaidiana kutunza nyumba na kupika. Nashukuru alinielewa, sasa nina muda wa kujijali mwenyewe, na kumjali na kumfurahisha yeye.
Tushajua wewe n Mwanamke wa dizain gani kama mtoto mmoja wasaidizi wawili...Mwamba kaingia cha kike
 
Mademu siku zihi hamuogi mnamaliza kutiwa mnajifuta tu na tshrt au Lesso mnavaa, Mbwa nyie bora Babycare inanukia bana dronedrake ni shahidi.

Zamani walikua wakimaliza wanatuomba hela za sabuni na lotion, siku hizi nyie ni bando, nauli na chips tu hovyo kweli.
Mademu gn we sema demu wako haogi usijumlishe kila mtu.
 
Let me tell you Maina...

Uanamke kazi sana. Hata mazingira yakibadilika wewe unatakiwa ubaki vile vile. Shughuli tupu!!

Mimi ndio maana tulipopata tu mtoto nikamwambia babe, nataka wasaidizi wawili wa kazi. mmoja wa kusaidiana malezi ya huyu baby boy, wa pili wa kusaidiana kutunza nyumba na kupika. Nashukuru alinielewa, sasa nina muda wa kujijali mwenyewe, na kumjali na kumfurahisha yeye.
Point aisee.
 
Jesus, mtoto mmoja wasaidizi wawili, una umri gan au una kazi gani labda una ulemavu? We ni mvivu na mchafu tusiende mbali
Hapana, chukua point yake kwamba mazingira inabidi umuwekee yawe bora ili awe mzuri na safi kama ulivyomkuta. Unakuta mtoto wa watu umemtoa anakaa kwenye nyumba nzuri ina maji ina kila kitu, unaenda kumuweka mpiji, maji ya kuchota kwa kichwa na huweki mazingira safi ya kufanya apate maji ya uhakika nyumbani na hapo bado una expect chumba chenu kimoja cha kupanga kidekiwe kila siku, ni sawa kweli wewe unaona..??
Wanaume tunawafubaza sana hawa watoto
 
Don't generalise, kuna wanawake wanajua kubalance, pamoja na kuwepo watoto lakini usafi wao na mazingira yao ni wa kiwango cha juu sana. Uchafu ni asili tu na hulka ya mtu, inawezekana hukumchunguza ila hata alivyokuwa mwenyewe bado alikuwa mchafu.
 
Hapana, chukua point yake kwamba mazingira inabidi umuwekee yawe bora ili awe mzuri na safi kama ulivyomkuta. Unakuta mtoto wa watu umemtoa anakaa kwenye nyumba nzuri ina maji ina kila kitu, unaenda kumuweka mpiji, maji ya kuchota kwa kichwa na huweki mazingira safi ya kufanya apate maji ya uhakika nyumbani na hapo bado una expect chumba chenu kimoja cha kupanga kidekiwe kila siku, ni sawa kweli wewe unaona..??
Wanaume tunawafubaza sana hawa watoto
Asante. Unajua nimegundua Wanaume wengi hawako na wanawake wanaowapenda. Maana mtu your queen kweli unataka apigike, huku mtoto, huku adeki, huku apike, na kitandani aje msafiiiii na hapo hapo na kazi ya kumuingizia kipato afanye msaidiane maisha😹😹😹😹😹
 
Let me tell you Maina...

Uanamke kazi sana. Hata mazingira yakibadilika wewe unatakiwa ubaki vile vile. Shughuli tupu!!

Mimi ndio maana tulipopata tu mtoto nikamwambia babe, nataka wasaidizi wawili wa kazi. mmoja wa kusaidiana malezi ya huyu baby boy, wa pili wa kusaidiana kutunza nyumba na kupika. Nashukuru alinielewa, sasa nina muda wa kujijali mwenyewe, na kumjali na kumfurahisha yeye.
Siku akipata uterezi kwa mfanyakaz ndo utajua
 
Back
Top Bottom