Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Rose Mayemba ametoa wito kwa viongozi wa dini nchini kutokuwa waoga na kukemea dhambi zote ikiwemo ufisadi bila kujali imefanywa nani.
Rose ametoa wito huo Februari 16, aliposhiriki ibada ya misa maalum ya kumuombea Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu iliyofanyika kijijini kwao Mahambe, Ikungi huku na kueleza kuwa viongozi wa dini wakiendelea kukaa kimya dhambi zinapotendeka taifa litaingia matatizoni.