PreGE2025 Mjumbe wa BAKWATA: Tushiriki uchaguzi 2025 kwa amani, tusiige mataifa mengine

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Watanzania wamehimizwa kuhakikisha wanashiriki uchaguzi Mkuu ujao ifikapo mwaka 2025 Oktoba huku wakiaswa kushiriki uchaguzi huo kwa amani na kutoiga mataifa mengine ambayo yanaingia kwenye vurugu kipindi cha uchaguzi.

Hayo yamesemwa na Mjumbe wa Halmashauri Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Ahmed Misanga katika la kongamano la waislam ambalo lilikuwa na washiriki 1800 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Kongamano hilo limeandaliwa na Taasisi ya Islamic Propation Center (IPC) Singida, ambalo lilianza Juni 13.2025 na kumalizika Juni 20.2025 katika Kata ya Ihanji Kijiji cha chungu,Wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida.

Huyo mjumbe wa BAKWA TA ni mwendelezo wa wapumbavu wanaoogopa mabadiliko,tukisema No Reforms no election Ina maana tunataka mabadiliko kwanza Ili twende kwenye uchaguzi huru na wa haki bila kuvunja amani
 
Watanzania wamehimizwa kuhakikisha wanashiriki uchaguzi Mkuu ujao ifikapo mwaka 2025 Oktoba huku wakiaswa kushiriki uchaguzi huo kwa amani na kutoiga mataifa mengine ambayo yanaingia kwenye vurugu kipindi cha uchaguzi.

Hayo yamesemwa na Mjumbe wa Halmashauri Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Ahmed Misanga katika la kongamano la waislam ambalo lilikuwa na washiriki 1800 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Kongamano hilo limeandaliwa na Taasisi ya Islamic Propation Center (IPC) Singida, ambalo lilianza Juni 13.2025 na kumalizika Juni 20.2025 katika Kata ya Ihanji Kijiji cha chungu,Wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida.

Mataifa gani hayo
 
"Tushiriki uchaguzi kwa amani"

Hii ni kauli ninayoisikia Tanzania tu kwanini uchaguzi uhusishwe na amani hawajiulizi?

Kwahiyo wanataka waibe halafu wakupoze kuwa utulie?

Mbona sijawahi kusikia US wanatuma wachungaji & mashekhe kusema uchaguzi uwe wa amani?
 
BAKWATA ni UWT ya siri, ndiyo maana siku zote, jumumu lao kubwa walilopewa na CCM ni kuupamba uovu wa CCM
 
Back
Top Bottom