Mjumbe wa China atoa mwito wa kuboresha hali ya usalama na kibinadamu nchini Somalia

Mjumbe wa China atoa mwito wa kuboresha hali ya usalama na kibinadamu nchini Somalia

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
Mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Dai Bing jana alitoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa kuunga mkono juhudi za kuimarisha hali ya usalama na kibinadamu nchini Somalia wakati nchi hiyo ikifanikisha uchaguzi wa rais na wabunge.

Bw. Dai Bing amesema China inatarajia kuwa Somalia itaunda serikali mpya na kutumai kuwa itatumiafursa hii kuharakisha ujenzi wa taifa na kutimiza utulivu na usalama wa muda mrefu mapema iwezekanavyo.

Ameongeza kuwa, amani na utulivu nchini Somalia bado ni masuala yanayokabiliwa na changamoto nyingi, na kusisitiza kuwa jambo muhimu kwa Somalia katika kukabidhi majukumu ya usalama ni kutekeleza mpango wa mpito nchini, kuharakisha uundaji na ujumuishaji wa jeshi lake, na kuboresha uwezo wake wa usalama kwa ufanisi.
 
... ameongea hivyo kwa kuwa Marekani inatuma kikosi Somalia. Mbona miaka yote hawajawahi kuongea hivyo kuhusu hiyo Somalia?

China ni manafiki wa kutupwa hawajawahi kuwa na huruma yoyote kwa Afrika zaidi ya dili zao za kifisadi.
 
Back
Top Bottom