Mjumbe wa kamati tendaji Yanga awatakia kila la Kheri Al Ahly

Akihojiwa na EATV mjumbe wa kamati tendaji Yanga bwana Alex Ngai amesema Yanga wanatamani siku moja na wao wapate fursa ya kushiriki African football league, lakini amewatakia kila la Kheri Al Ahly katika michezo yake dhidi ya Simba.
Sasa kama yeye ni shabiki la AL ahly je?
 
Enyimba ina ubora gani? Klabu ubingwa imeshatolewa preliminary stage.
Hiyo michuano ni ya kuwavimbisha kichwa Al Ahaly tu.
Imetolewa na timu ya Libya. Ingetolewa na ASAS au Zalan ningeshangaa.
 
ila inaumiza sana. Yaani unafika fainali ya kombe la shirikisho halafu unaambiwa haustahili kushiriki ligi yenye vilabu bora nane?
Inaumiza kitu gani sasa! Mbona hata USM Alger waliochukua huo ubingwa hawapo!! Kubali hayo mashindano kwa mwaka huu hayana tofauti na bonanza!! Labda kwa siku zijazo ndiyo yatakuwa na tija iwapo vigezo na masharti vitazingatiwa.

Maana Enyimba haina mafanikio yoyote yale ndani ya hii miaka michache! Na sidhani hata ipo kwenye timu 20 bora Barani Afrika kwa sasa. Lakini na yenyewe imejumuishwa.
 
Vigezo ndio hivyo, ubora wa timu sambamba na uwakilishi wa region. Hata World Cup wasingeweka utaratibu wa region, huenda Africa tungekuwa tuna nafasi 3 labda badala ya 5 za sasa. Enyimba anatoka ile region ya West Africa, na ndiye walau anayetisha kule kwa hii miaka 5 ya mwisho
 
Kwenye hicho kipengele cha uwakilishi wa Kikanda (Regions) kwa ajili ya kutanua soko la hayo mashindano, naona itakuwa ndiyo hoja yenye mashiko zaidi. Ila ukija kwenye ubora, siamini kama timu kama Enyimba ina ubora wowote ule kwa sasa.
 
Al Ahly ataenda hadi fainali. Ni suala la muda tu
Al Ahaly wakiweza kuwatowa Mamelodi Sundowns wanachukuwa ndoo.

Ila hao Mamelodi Sundowns kwa hao Waangola Petro huwa ni mbinde haswa mechi haitabiriki mshindi wa jumla nani atakwenda nusu fainali, Al Ahaly tayari wameshaingia nusu fainali hili wala halina mjadala, huwezi kutegemea mazingaombwe kwenye Mpira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…