Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa Bw. Daniel Chonchorio Nyamohanga, Mkazi wa Nyakato Jijini Mwanza anadaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha majira ya asubuhi siku ya jana.
Kwa mujibu wa Familia wanasema aliondoka Nyumbani kwake tarehe 23 majira ya Saa 2 Asubuhi akiwa anaenda mazoezini lakini tangu hapo hawakumpata hata kwa simu zake za mkononi nazo hazipatikani.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Familia imesema imetoa taarifa kituo Kikuu cha Polisi na tunaendelea kumtafuta RPC Mwanza kupata undani wa taarifa hii.
Aidha Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linaendelea na uchunguzi juu ya kutoweka kwa Ndugu Daniel Chonchorio Nyamhanga, ambaye ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa ambapo hadi sasa, hajapatikana, na juhudi za kumsaka zinaendelea.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, SACP Audax C. Majaliwa, familia, ndugu, jamaa na marafiki wa Nyamhanga wameeleza wasiwasi wao kuhusu kutoweka kwake.