MJUSI KAFIRI

MJUSI KAFIRI

Mahmood

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2008
Posts
7,908
Reaction score
2,478
Napenda kuuliza kuhusu jambo hili (Labda linaweza kuwachekesha wengine lakini mimi limenishangaza), katika siku moja kuna mjusi watatu walibanwa na milango 3 tofauti za nyumbani, wote walibanwa katika siku hiyo hiyo moja (Haya hayajawahi kutokea tokea tuanze kuishi katika nyumba hii sasa ni miaka 24).

Milango iliyo wabana mjusi hao ni yajikoni (mlango wa kuingilia jikoni kutokea inje, uwani), na mlango wa kuingilia ndani (Main door) na mlango wa choo cha chumba chetu (master bedroom).

Je hili tukio lina maana yeyote ?
 
Mjusi Kafiri (Lugha)??????????????????????????????
 
Mjusi ni kiumbe kama viumbe wengine inaonyesha humu ndani ya nyumba yenu kuna hao viumbe wengi haina maana mbaya mbona mimi ninae Mjusi na kila siku analia na kunipa News kulia kwake nikiangalia saa najuwa amesema kitu gani mjusi huwa halii ovyovyo tu ndani ya nyumba. mimi nawependa hao viumbe.

lizard-8433.jpg
 
Du umeshaniwahi na atavar hiyo Big up Mashaa allah!
 
Nitarudi watu wakishatoa maana na tafsiri
 
Lakini kitu cha kushangaza mjusi watatu wamebanwa na milango mitatu tofauti katika nyumba moja na siku moja ?

I have been living in this house for 24 years now, this has never happened before.

Pia katika nyumba hii hakuna mjusi wengi..
 
Mjusi ni kiumbe kama viumbe wengine inaonyesha humu ndani ya nyumba yenu kuna hao viumbe wengi haina maana mbaya mbona mimi ninae Mjusi na kila siku analia na kunipa News kulia kwake nikiangalia saa najuwa amesema kitu gani mjusi huwa halii ovyovyo tu ndani ya nyumba. mimi nawependa hao viumbe.

lizard-8433.jpg

Acha bwana wee, anakupa News gani ?

Naomba utufahamishe.
 
Sasa hilo swali na jukwaa la lugha, wapi na wapi jamani? haya bwana...
 
Napenda kuuliza kuhusu jambo hili (Labda linaweza kuwachekesha wengine lakini mimi limenishangaza), katika siku moja kuna mjusi watatu walibanwa na milango 3 tofauti za nyumbani, wote walibanwa katika siku hiyo hiyo moja (Haya hayajawahi kutokea tokea tuanze kuishi katika nyumba hii sasa ni miaka 24).

Milango iliyo wabana mjusi hao ni yajikoni (mlango wa kuingilia jikoni kutokea inje, uwani), na mlango wa kuingilia ndani (Main door) na mlango wa choo cha chumba chetu (master bedroom).

Je hili tukio lina maana yeyote ?

unachezewa na majirani zako, lete mbuzi nikutengenezee kinga fasta. Usisahau pia kuwaletea mizimu LED tv ya nchi 42
 
Na kwanini waitwe Kafiri?
Nachojua ukafiri unahusiana na dini,
Sasa mijusi na dini wapi na wapi?
Au ni jina tu?
 
Mkuu, kwa wiki unaweza kabana mijusi mingapi? Tufanye hiyo project ya mijusi
 
Mijusi wanasogelea maeneo hayo ya jamaa kwani inaelekea kuna wadudu wengi sana anga hizo wapulizie sumu ya kuua wadudu farmigation
hicho kitawafanya mijusi kukosa wadudu na watajikaa sorry wataondoka zao
 
Acha imani za giza. Kama umewaona wachomoe uwatupe. Jaribu kufanyia usafi nyumba yako, inaonekana umchafu sana.
 
Back
Top Bottom