KERO Mkaa una thamani kuliko uhai wa mtu? Maliasili Tabora mjitafakari

KERO Mkaa una thamani kuliko uhai wa mtu? Maliasili Tabora mjitafakari

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

McRobert Manoeuvres

New Member
Joined
Apr 22, 2024
Posts
2
Reaction score
1
Maliasili wako tayari kudhulumu uhai wa mtu kisa Mkaa, Mamlaka zichukue hatua stahiki kinachoendelea Tabora sio haki, sio utaratibu. Mtu yupo Main Road kabeba gunia moja la mkaa na magunia mengine matatu ya mazao, Gari la Maliasili lina Overtake kwa kumgonga pembezoni ili kuchukua gunia moja la mkaa, Seriously Mkaa una thamani kuliko uhai wa Mtu?

Hili lmetokea leo mchana.
 
Hao jamaa wapumbavu sana, wameua na wametia watu ulemavu wengi tu...Mlandizi, Kosarawe hayo matukio yanatokea sana tu.
 
Huenda alikaidi ndio maana nguvu ikatumika.

Ila pamoja na hayo, maliasili hawakufanya sawa.
Hata kama alikaidi hawakupaswa kuchukua sheria mikononi mwao.hakuna ambaye yuko juu ya sheria hivyo ni lazima watu hao wafikishwe kwenye vyombo vya sheria
 
Ni Amri kutoka juu

Hasa kwny Maliasili zikiwepo Mkaa na Wanyama pori

Kule Same na Mwanga Tembo mmoja ana thamani kuliko Wanakijiji wa kijiji kizima japo Tembo wamekuwa wengi sana lakini Ole wako uue mmoja au umdhuru
 
Gesi bei juu, umeme bei juu, wakijitafutia namna ya kupika mnawafanyia ubaya.
Kama mna uchungu na nchi katazeni wanaouza rasilimali za nchi
 
Back
Top Bottom