Jamii Opportunities
JF-Expert Member
- Feb 10, 2014
- 4,876
- 1,549
Chama Kikuu cha Ushirika Kagera (1990) Ltd kinaundwa na vyama vya msingi 134 kutoka katika wilaya tatu za Muleba, Bukoba na Misenyi. KCU (1990) LTD yenye makao makuu katika manispaa ya Bukoba, inaendesha shughuli zake chini ya Sheria ya Ushirika namba 6 ya mwaka 2013, Ili kutekeleza kwa ufanisi shughuli zake, KCU{1990)Ltd inatangaza nafasi ifuatayo:-
MKAGUZI MKUU WA NDANI (NAFASI 01)
Mkaguzi Mkuu wa ndani atakuwa Mkuu wa ldara ya Ukaguzi wa ndani na atawajibika kwa Bodi ya KCU (1990)Ltd. Atakuwa na jukumu la kutathmini utoshelevu wa udhibiti wa ndani, uendeshaji wa shughuli kwa kufuata miongozo, Kanuni na Sheria.
MAJUKUMU
VIGEZO NA UZOEFU
Kwa ambaye ana sifa na vigezo vilivyotajwa hapo juu, anaweza kutuma maombi kwa barua iliyoandikwa kwa mkono na kusainiwa kwa njia ya Posta, ikiambatana na maelezo binafsi (CV)
yenye anuani, namba ya simu na barua pepe, picha ndogo mbili, nakala za vyeti na wadhamini watatu wenye mali zisizo hamishika (Fxed assets) au watumishi wenye mikataba ya kazi ya kudumu kwa anuani liyopo hapa chini.
Waliokwisha kutuma maombi wasitume tena. Aidha, ambao hawatapata wito wa kuhudhuria usahili wajue kuwa hawakukidhi vigezo vinavyohitajika.
Mwisho wa kupokea maombi ni Ijumaa, tarehe 26/04/2022 saa 10.00 ioni.
MENEJA MKUU, KCU (1990) LTD
S.LP 5, BUKOBA

- Kupima na kutoa taarifa juu ya utoshelevu wa udhibiti katika makusanyo, uhifadhi na matumizi ya rasilimali za KCU (1990)Ltd
- Kupima na kutoa taarifa juu ya utekelezaji wa Sheria Kanuni, Nyaraka za Mrajis pamoja na maamuzi ya Mkutano Mkuu kupita taarifa za mapato na matumizi ili kubaini kama zimetayarishwa kwa usahihi
- Kupitia na kutoa taarifa juu ya mifumo inayotumika na matumizi ya rasilimali
- Kupitia na kutoa taarifa juu ya maamuzi na hatua mbali mbali zinazochukuliwa na Menejimenti
- Kupima thamani ya fedha (value for money) kwenye miradi mbali mbali inayotekelezwa na KCU (1990)Ltd
- Kupitia na kutoa taarifa juu ya mfumo wa ukusanyaji kodi za majengo, upangaji wa bei na ukusanyaj wa madeni
- Kupitia na kutoa taarifa juu ya mfumo wa uendeshaji wa hoteli, udhibiti wa mapato na matumizi
- Kupitia na kutoa taarifa juu ya mfumo wa manunuzi na mauzo ya kahawa ndani na nje ya nchi
- Kufana kazizinqine atakazoagizwa na Bodi
VIGEZO NA UZOEFU
- Shahada ya kwanza au Stashahada va uu kaika nnasomo ya Uhasibu, Fedha au Utawala wa Biashara
- Lazima awe amesajiliwa na Bodi ya Wanasibu na Wakaguzi Tanzania walau katika daraja la ACPA
- Awe na walau uzoefu wamiaka mitatu katika kazi za Ukaguzi
- Awe wezo wa kuandik ana kuongea lugha ya Kiswahili na Kingereza kwa ufasaha
- Awe na uwezo wa kushirikiana na wenzake katika kutimiza malengo ya taasisi
- Awe na uwezo wa kutumia kompyuta
- Asiwe na umri zaidi ya miaka 45
- Awe Raia wa Tanzania
- Awe hajawahi kuhukumiwa kwa kosa la jinai