GE2025 Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Mwaswengu awataka Wananchi Songe kudumisha Amani na Utulivu

GE2025 Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Mwaswengu awataka Wananchi Songe kudumisha Amani na Utulivu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (A/INSP) Mwaswengu, ambaye ni Polisi Kata ya Songe, Wilaya ya Kilindi, Mkoa wa Tanga, amewataka wananchi wa kata hiyo kudumisha amani na utulivu katika kipindi hiki cha kampeni na kuelekea Uchaguzi Mkuu.

1761373181739.png
Wito huo umetolewa Oktoba 24, 2025, wakati Mkaguzi huyo alipokutana na wananchi katika eneo la Kijiwe cha Draft Darajani.

Amesema ni muhimu wananchi kuwa walinzi wa amani kwa kutoa taarifa mapema kuhusu viashiria vya uvunjifu wa amani ili hatua zichukuliwe kabla ya madhara kutokea.

1761373247395.png
Aidha, amewasisitiza wananchi kuimarisha ushirikiano na Jeshi la Polisi kupitia vikundi vya ulinzi shirikishi, kwa lengo la kudhibiti matukio ya uhalifu na kuhakikisha jamii inabaki salama.

1761373263265.png
 
Nchi ina amani na imetulia kama kawaida na wananchi wanaendelea na shughuli zao ila polisi wanafanya ionekane kuna taharuki. Wamekazana kuimba amani amani amani wakati amani ipo. Mbona wanahubiri hofu kwa kitisho cha uwepo wa maandamano yasiyojulikana?
 
Back
Top Bottom