MKUU SWALA LA KUJIAJIRI AU KUAJIRIWA HAPA TANZANIA LINA HISTORIA NDEFU SANA, HAPA KUNA MAMBO MENGI SANA.
1. TATIZO LA KUAJIRIWA HAPA TANZANIA.
tatizo la ajira hapa tanzania lina mlolongo mkubwa sana na lina sababishwa na vitu mbalimbali. MFANO
a. UCHUMI WA TAIFA LETU
Uchumi wa Tanzania kwa sasa ni mbaya sana na kama unavyo jua nchi yetu ni masikini sana ingawa tuna rasilimali za kutosha. Tumeshindwa kujenga uchumi imara ambao utavutia investors wakubwa wa ndani na nje walete mitaji yao ili ajira zipatikane kwa wingi.
2. TRIENDS YA UWEKEZAJI TANZANIA
kama ukifuatilia uwekezaji wa tanzania umejikita katika secta ya utalii kwa wingi sana, secta ya habari, madini kwa wingi sana, kilimo, na viwanda kwa uchache
TATIZO LA AJIRA TANZANIA LINGEWEZA KUPUNGUZWA NA UWEKEZAJI KATIKA VIWANDA NA SI KATIKA CHOCHOTE KILE
Vi wanda ndo suluhisho pekee la ajira Tanzania, Na Wawekezaji wengi hawawekezi kwenye viwanda, wanawekeza kwenye utalii ambao un ajiri watu wachache sana,
- Nchi nyingi sana duniani hupunguza tatizo la ajira kupitia viwanda,
- Mfano kiwanda kama cha A to Z arusha kimeajiri watu zaidi ya 4000, pamoja na kwamba masilai si mazuri ila inasaidia sana hebu fikilia tungekuwa na viwanda aina ya A to Z kama 10,000 hapa tanzania ingekuwaje?
3. KUFA KWA VIWANDA VILIVYO KUWEPO
Viwanda vyote vimekufa na yamebaki magofu baada ya hata mashine kuchuliwa na kwenda kuuzwa kama chuma chakavu
Hivi viwanda kama vyote vingekuwa hai vingeweza kutupunguzi tatizo kwa kiasi fulani
4. MABADILIKO YA SAYANSI DUNIANI
Kwa sasa Computa zinachukua nafasi ya binadamu, chukulia mfano benk zamani na sasa, zamani benki moja ilikuwa na si chini ya wafanyakazi 20 ila kwa sasa benk moja inawafanyakazi 8 hadi 10
makampuni mengi sana yanatumia komputa badala ya binadamu ili kupunguza cost na kuongeza ufanisi, chukulia mfano kwa sasa TBL walikuwa na mpango wa kufungu ROBOT ZA KUPANGA CRETI ZA BIA, HAPO UNATEGEMEA NINI?
5. USHINDANI WA BIASHARA
Ushindani huu unapelekea makampuni mengi kupunguza ghalama za uendeshi ili kuweza kupambana, na wanapunguza kupitia kuajiri wafanya kazi wa chache sana
6. MFUMO WETU WA KIJAMAA
Tulizoea kila kitu ni serikali, ajira serikali, biashara serikali, huu mfumo wa kinjamaa ungali upo vichwani mwetu, hatutaki kubadilika.
7. WAZAZI WETU
Wazazi wetu nao wanachangia sana walitulea vibaya sana, tulizoeshwa kila kitu, tuliambiwa kwamba tunasoma ili tuje kupata kazi nzuri, tunasoma tuje kuwa mameneja, tunasoma ili tuje kufanya kazi TRA, BANDARINI, NSSF, BENKI NA KAZALIKA
TUMEKUWA TUKIAMINI TUKO SHULENI AU VYUONI ILI TUJE KUPATA KAZI NZURI SANA, HILI NI KOSA KUBWA SANA LA KUWALALUMU WAZAZI WETU, LEO HII KIJANA YUKO MTAANI AMEMALIZA CHUO ANASUBILI AJIRA, DEGREE YAKE HAOWEZI HATA MSAIDIA KUANZISHA BUSTANI YA MBOGA
KWA KIFUPI KUNA MASWALA MENGI SANA YANAFANYA AJIRA ZIWE NGUMU, NA ZINAKUWA NGUMU KUTOKANA NA WAHITIMU WOTE KWENDA KUBANANA KWENYE KUAJIRIWA.
KATIKA SWALA LA KUJIAJIRI HAPA KUNA UNAFIKI WA HALI YA JUU MNO, NA HAPA MIMI SI ILAUMU SERIKALI HATA KIDOGO.
1. Hivi serikali ndo inajukumu la kutuanzishia biashara?
2. Ni wangapi tuna culture ya kujiajiri tangia mwanzo?
3. Ni wangapi wamemaliza chuo na kujairibu hata kuanzisha bustani? utazungumziaje kupewa mikopo ya kilimo wakati unaona aibu kuanzisha bustani eti utachekwa na ngudu, jamaa, rafiki, mchumba na kazalika?
TUNA ILAUMU SERIKALI LAKINI SISI WENYEWE NDO TATIZO KATIKA KUJIAJIRI.
1. MFUMO WA KIJAMAA TENA HAPA NI TATIZO
Ndo kama hivyo tunasubiria serikali ituanzishie biashara, ituambie sasa vijana fanyeni biashara
2. WAZAZI WETU
walitufundisha kwamba tunasoma ili tuajiriwe na tumejijengea hivyo, hadi leo hii wanafunzi wa shule za misingi ukiwauliza wazazi wao huwa wana washauri nini kuhusu elimu utasikia haya. TUNAAMBIWA TUSOME ILI TUJE KUWA MAMENEJA, TUJE KUWA MARUBANI, TUJE KUAPATA KAZI NZURI
Hakuna hata mazazi mmoja anaye mwambia kijana wake asome aje kuwa mjasirimali mzuri, Wale watoto tiyali wameisha haribiwa, wao wako shuleni ili waje kuajiriwa na si vinginevyo
3. WALIMU WETU NAO WANACHANGIA SANA
Hawa nao story wanazo wapatia wanafunzi shuleni ni kama za wazazi tu, SOMENI SANA MJE KUWA MAMENEJA
4. EXTENDED FAMILLY
Huu mfumo wa extended familly kwa huku kwetu naona nao ni kikwazo sana, tena sana
LEO HII KIJANA ANAMALIZA CHUO/SHULE NA KAZALIKA ANAKAA KWA DAD, KWA SHENEJI, KWA MJOMBA, KWA SHANGAZI, KWA BIBI, KWA BABU, KWA MDOGO WAKE NA SHEMEJI, KWA BINAMU, KWA BABA WA UBATIZO, KWA MAMA WA UBATIZO.
Leo hii huyi kijana ukimwambia jiajiri hawezi kukuelewa wakati huko kwa ndugu zake anaishi kwa raha sana ANAPEWA HELA YA VOCHA, AMENUNULIWA SIMU KARI SANA, ANAKULA VIZURI SANA MILO MINNE KWA SIKU, HIVI HUYI KIJANA UKIMWAMBIA TUKASHIKE POLI TUANZE UJASIRIAMLI ATAKUELEWA? ANASHIDA GANI?
Ndugu wanachangia sana kufanya vijana wasiwe na ari ya kujijiri kwa sababau wanakuwa wanawatoa fedha, sheneji atampa, mjomba atampa na mama atampa,
HUYU KIJANA HAWEZI KUWA NA MAWAZO YA KUJIAJIRI HATA SIKU MOJA.
4. VIJANA WENGI KUAMNI KWAMBA NYUMBANI KUNA MALI ZA KUTOSHA
Kama kijana anaamuka na anaona home kuna magari, kuna nyumba za kutosha kuna fedha za kutosha ya nini akajiangaishe na biashara? si bora akae nyumbani? Je anaweza anisha biashara ya Baba lishe?
Hapa husubiri wazazi wafe ili wahike usukani
5. UNAFIKI WA GRADUATE.
Haya mambo ya kujiajiri huwa yanazungumzwa na graduate wakisha ingia mtaani na kuona mambo yote yamefeli ndo huanza kukurupuka.
VYUONI HAKUNA UNDERGRADUATE WANAO PIGA STORY ZA KUJIAJIRI, PALE WATU WANAPEANA MATUMAINI YALIYO PITILIZA, WANAWAZA JINSI WATAKAVYO AJILIWA TRA, NSSF, BANDALINI, BENKI NA KAZALIKA
Na ushajiuriza ni kwa nini wanawake/wnaume wengi sana wanapapatikia Undergaduates? au Graduate? Wanafahamu huyu akimaliza chuo tu atakuwa na kazi nzuri sana, atakuwa meneja, so kila mwanamke/mwanaume anataka awe na mchumba alie chuo kikuu kwa matumaini kwamba maisha kwake yatakuwa mteremko.
HUYU KIJANA ALIOKO CHUONI NA ANAE MPA MATUMAINI MCHUMBA WAKE KWAMBA NIKIMALIZA CHUO TU NA NASA KAZI, HAWEZI MALIZA CHUO HALAFU AKAANZISHA BUSTANI YA MBOGA, MCHUMBA ATAMZARAU SANA NA MCHUMBA TANGIA MWANZO ALISHA JUA MCHUMBA WAKE AKIMALIZA CHUO ATAKUWA MENEJA, LEO HII AMUONE ANA KIBANDA CHA KUUZIA VOCHA,
NATOA MFANO HAI.
NIKIWA CHUONI, TULIVYO KUWA TUNAKARIBIA KUMALIZA CHUO, TULIKUWA TUSHA SOMA ALAMA ZA NYAKATI KWAMBA MTAANI SI SALAMA, NA TULIANZA MIKAKATI IFUATAYO.
Tuliamua kutafuta tasisi za serikali zinazojihusisha na maswara ya biashara ili zije zituelimishe maswala mbalambali yahusuyo kujiajiri, tuliita
-TRA
- BRELA
- TIC
- SIDO
- NA BAADHI YA BENKI
WAKUU TULIBEZWA SANA, UNDERGRADUATE WENZETU WA KOZI ZINGINE TULIKUWA TUKIWAALIKA NA WALIVYO KUWA WAKIINGIA UKUMBINI KWELI WALIKUWA WAKISILIKIZA KWA UMAKINI SANA, ILA KWENYE KUULIZA MASWALI SASA, WAKATI WENGINE TUKIULIZA WATUPE MAUJANJA YA KUJIAJIRI WENZETU WALIKUWA WANAULIZA MASWALI KAMA WANAWEZA PATA CHANSI ZA KUAJIRIWA KWENYE HAYO MASHIRIKA
Wakuu nazani mmepata picha, Undergraduate wengi sana wakiwa vyuoni wanawaza kuajiriwa wala hakuna wano panga mikakati ya kujiajiri. Ila wazo la kujijiri huja baada ya mtaani kuwa kugumu,
7. MAWAZO POTOFU/ NAITA NI UJINGA
Eti graduate ailiyesomea kilimo, hawezi anzisha hata busatni, eti atakuwa najiaibisha,
Geaduate aliye somea mapishi hawezi anzisha biashara ya Mama lishe/ Baba lishe, kisa aibu, atachekwa na jamaa zake pamoja na mchumba wake
KWA STAILI HII AJIRA ZITAENDELEA KUWA NGUMU, TUTABAKIA KUSEMA TUNAMAWAZO YA BAISHARA ILA TUMEKOSA MITAJI
7. OVER EXPECTATIONS
hii inatusumbua sana, na ni moja ya sababu ya graduate kushindwa kujijiri
SO TUACHE KULAUMU SERIKALI WAKATI C C HATUJAONYESHA NJIA.
1, Je tumeonyesha njia ya kujiajiri?
2. Je tunaspirti ya ujasiriamali?
3. Tusha anagalau anza? ili basi serikali ikija ikute tumefanya somthing?
4. Je bado tuna story za kwamba tuna aidia nzuri sana ila tumekosa mitaji?
5. Je hatuna unafiki?
6. Je kama tumepenga kujiajiri na tulisha anza mikakati baadae tukaitiwa kazi tutaenda? au tutaendele na mikakati ya kijiajiri?
LAZIMA TUBADILIKE VYUONI
- KULE INDIA, KUNA CHUO KIMOJA CHA MASWALA YA AGRICULTURE NILIKUWA NA FUATILIA STORY ZAKE, NIKAKUTANA NA KITU CHA AJABU ASILIMI 45% YA GRADUATE HUANZISHA MAKAMPUNI YAHO/ HUJIAJIRI WENYEWE.
- Turudi huku bongo
- Je SUA ni asilimia ngapi wanajiajiri
- Je UD
- MZUMBE
- DIT
- UDOM
- TUMAINI
- SAINT AGASTINI
Fanya research utakuta ni hakuna,
Cha kusikitisha hata vyuo vya VETA badala ya walimu kuwandaa wanafunzi wajiajiri wao wanawapigia story za kuajiriwa
TUACHE KULIALIA, TUBADILIKE KWANZA. TUONYESHE NJIA,