Hao ANC walipokuwa wanapambana na makaburu walipata support mpaka nje ya nchi, na bado waliteswa zaidi ya miaka 50, na hakuna chochote waliwafanya wazungu, mpaka alipotokea mzungu mlokole akaona ni siasa outdated, kama hao weusi wa kusini waliogopwa na wazungu, mbona Mandela alikaa jela 27yrs mpaka alipotolewa kwa huruma ya De Clerk? Ww unatolea mfano wa miaka chini ya 10 kwa cdm!
Inaonekana ushawishi kwako ni njia ya mapigano tu, bila kujua njia ni nyingi ikiwemo kususia. Kwa taarifa yako hii tabia ya kususia inazidi kuleta njia ya kukaa mezani, kuliko hiyo ya mapambano ambapo tayari watu ni waoga. Kitendo cha CDM kususia chaguzi ni njia nzuri na salama kwa wanachama na wafuasi wake, kwani haiwaachi na vifo au vilema vya maisha. Hii inasaidia kuwa na viongozi wasio na uhalali wa umma, ambapo kadiri muda unavyokwenda ni rahisi kushawishi wananchi kuutoa uongozi wa kihuni kwa public disiobidiance.