Mkakati mwingine wa kuendeleza mpunga waja

Mkakati mwingine wa kuendeleza mpunga waja

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
1576649595390.png

Serikali imezindua mkakati wa taifa wa awamu ya pili wa miaka 10, wa kuendeleza zao la mpunga nchini ili kuhakikisha wanafikia hekta milioni moja ifikapo mwaka 2025.

Hayo yalibainishwa jana na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, ambapo alisema lengo ni kuona wanaongeza uzalishaji wa zao la mpunga ifikapo 2030, kusiwe na njaa pamoja na kuongezeka kwa biashara ya zao hilo.

Alisema amefarijika kusikia Tanzania imeshika nafasi ya nne kuzalisha mpunga, lakini atafarijika zaidi kusikia imeshika nafasi ya kwanza au ya pili.

"Sijafurahi sana kuona tunapitwa na Misri na Madagascar wakati wao hufanya kilimo cha mpunga cha umwagiliaji, nahitaji kuona tunakuwa juu yao hapo baadaye," alisema Hasunga.

Alisema kuna kila sababu ya kusonga mbele katika zao hilo hasa ukizingatia ni zao pendwa na kila mtu, na kwamba nchi inaweza kutoa mchele safi na bora ambao utauzwa nje.

Alisema mkakati huu wa miaka 10 wa awamu ya pili unaonza 2019 -2030, ukawe chachu ya maendeleo ya wakulima wa zao hilo nchini.

Alisema wizara yake itatekeleza uongezekaji wa mbegu bora, kuongeza eneo toka milioni 1.1 hadi 2.2 ifikapo 2030, kuongeza thamani ya mpunga.

Aidha, alisema bado sekta za fedha hazijawekeza katika kilimo, pia uwekezaji bado haukidhi mahitaji ya kilimo.

Kadhalika, Hasunga alisema bado kuna uhaba wa mbegu nchini, ambapo mahitaji ni taji 186,000 wakati zinazopatikana kwa sasa ni tani 57,000.

Alisema wakulima wamekuwa wakilima kilimo cha hasara, na kuwa kwa sasa mikakati ni kuhakikisha wengi wanalima kilimo cha biashara.

Alisema bado kuna uhaba wa mbegu nchini ambapo mahitaji ni taji 186,000 wakati zinazopatikana kwa sasa ni tani, 57,000 pekee.

Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Methew Mtigumwe, alisema mkakati huo uliozinduliwa ni mwendelezo wa matokeo ya utekelezaji wa mkakati wa awali wa kuendeleza zao la mpunga NDRS 1 ambapo ili kuongeza kiwango cha uzalishaji uliowekwa, ni lazima kupanua maeneo yanayofaa kwa kilimo cha mpunga kwa umwagiliaji na yanayotegemea mvua.

"Tanzania tumedhamiria kuongeza uzalishaji wa mpunga mara mbili zaidi kutoka tani 2.2 kwa sasa hadi tani 4.5 ifikapo 2030, na hili litafanikiwa kwa kutumia kilimo cha umwagiliaji, mbegu bora, mbolea, dawa zinazofaa na zana bora za kilimo ikiwamo kupunguza upotevu kabla na baada ya mavuno," alisema Mtigumwe.

Chanzo: IPP Media
 
Back
Top Bottom