Mkakati wa Chato kuwa mkoa wapingwa rasmi na RCC ya mkoa wa Kagera

Tatizo halipo kwa RCC wala askofu Bangonza; ila tunajaribu ku-mchallenge mwanzisha uzi hakutupa muhitasari wa nini kimeazimiwa na Mkoa wa Kagera, instead kaja na mawazo ya mtu mmoja, jambo ambalo nalo ni sawa.

Henry Ford anasema, kila mmoja yuko sawa maadam anachofikiri ni sawa. Japo kwa mtazamo matokeo baadae huwa yanawatofautisha hao wawili kwa misingi ya fikra zao.
 
Chato inakwenda kuwa Mkoa,wenye wivu jiandaeni kujinyonga.
 
Naunga mkono hoja.
Mimi binafsi nilimuona Magufuli kama mtu mkatili na mbinafsi sana ambaye Tanzania hajawahi kutokea.

Akiwa Waziri wa Ujenzi wakati wa B Mkapa alibasidili ramani ya barabara isipite Biharamulo ila ikapita Chato. Alipokuwa Rais ametumia madaraka yake makubwa kupeleka Kijijini kwao Chato miundombinu mikubwa kama Airport, Referral hospital, TRA, CRDB na Mbuga ya Burigi kwa kutumia raslimali za taifa.

Chochote kinachofanyika kuhalalisha UBADHIRIFU wa Magufuli kwa kuifanya Chato kuwa Mkoa nakiita ni UHAYAWANI.

Ile miundombinu inabidi ibakie hivyo hivyo katika ngazi ya wilaya kama ilivyobakia Gbadolite ya Mobutu Seseseko. Tunataka watu wakibisha kuwa tulikuwa na Rais kichaa na mwizi tuwaonyeshe mfano halisi
 
Hoja ya ukabila kuhalalisha mkoa wa CHATO haina mashiko.

Tujiulize faida ya kuanzisha mkoa huo kwa Taifa ni nini?

Tusikurupukeee! Tujenge uchumi kwanza hayo ya mikoa na wilaya yatafuata.

Kuanzisha mkoa ni gharama kubwa sana! Mpaka leo tuna mikoa mipya kadhaa iliyoanzishwa kwa JAZBA za kisiasa haijaweza kusimama kikamilifu kuwa mikoa, mfano mingi bado ofisi za wakuu wa mikoa zimejiegesha kwenye majengo ya watu.

Nyumba za watumishi SHIDA! Huko hatujakamilisha mnataka kuanzisha mikoa mingine! Ni nani aliturogaaaaa?
 
Uwanja wa Chato vijana wa Subaru kutoka kaskazini wauchamgamkie, wautumia kwny 0-60, piga Sana ma-drift etc
 
Hoja ya ukabila kuhalalisha mkoa wa CHATO haina mashiko.
Tujiulize faida ya kuanzisha mkoa huo kwa Taifa ni nini?...
Shida ni justification za wasomi hasa wa kagera..ukisoma hata report ya RCC utachecka,, eti utagawanyisha koo na kabila,, harafu eti watapoteza wilaya zenye ardhi nzuri kwa mifugo na kilimo kama hizo wilaya mbili zitakuwa mkoa tofauti.

Lakini hoja nyingine ikasemwa kwa sbb huko Biharamulo na Ngara kunamadi nayaosaidia kuiedneleza Bukoba na kusema chato kama chato haijaendele kuwa mkoa kwani bado wilaya changa.

Ndo nikajiuliza je serikali ikisema iweke mkoa nyakanazi..Bukoba watashangilia ? wanaposema masuala ya ardhi..je haoa tanzania kunamtua anakatazwa kwenda kuchunga au kulima mkoa mwingine?

Suala la madini...je Geita ilupoundwa na kumegwa kutoka Mwanza..walo mbona walikubali kwanini hawa waone madini kuwa mkoa mwingine mpya ni shida..inamaana basi hata geita ivunjwe ili mkoa mama wa Mwanza ufaidi mapato ya madini kutoka wilayani Geita..Shida ni hoja zinazojengwa zinaonekana hazina mqshiko ..angalu wewe umeleta hoja ya msingi
 
Nyumbs za watumishi mbona huwa zinauzwa,wacha tuwe tunapanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…