Basi Moshi iwe republic.Chato itakuwa mkoa soon, mambo yote yanaenda kama yalivyopangwa!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Basi Moshi iwe republic.Chato itakuwa mkoa soon, mambo yote yanaenda kama yalivyopangwa!
Tatizo halipo kwa RCC wala askofu Bangonza; ila tunajaribu ku-mchallenge mwanzisha uzi hakutupa muhitasari wa nini kimeazimiwa na Mkoa wa Kagera, instead kaja na mawazo ya mtu mmoja, jambo ambalo nalo ni sawa.Tatizo liko wapi? Tumejua kwamba RCC ya Kagera wamegoma, na kwamba askofu Bagonza ameunga mkono maamuzi ya RCC ila akaenda mbali kutupa faida ya kuwa na Halmashauri nyingi kuliko wilaya au mikoa. Jamani kuna zaidi ya hapo tena?? Mwisho na mimi nawaunga mkono RCC na baba askofu.
Chato itakuwa mkoa hilo halina ubishi!
Naunga mkono hoja.Anaandika Askofu Bagoza PhD.
TUNAHITAJI HALMASHAURI NYINGI KULIKO MIKOA NA WILAYA MPYA
Kamati ya Maendeleo ya Mkoa wa Kagera (RCC) imemaliza kujadili mapendekezo ya kuundwa kwa Mkoa mpya wa Chato. Wengi wanakataa mapendekezo hayo. Niliwaunga mkono mapema.
Natamani Taifa lihitimishe uundwaji wa MIKOA na Wilaya mpya. Badala yake, jopo la wataalam wa kada mbalimbali, wajikite katika kupendekeza uundwaji wa HALMASHAURI mpya. Kwa Nini tunahitaji zaidi HALMASHAURI kuliko MIKOA na Wilaya?
1. Masuala karibu yote ya Maendeleo yako TAMISEMI.
2. Halmashauri ni kitovu cha mamlaka ya wananchi kujipanga na kusimamia mambo yao.
3. Tuachane na "developmentalism" (U-maendeleo) na kuingia katika "transformation"(Mabadiliko).
4. Maendeleo endelevu hayahitaji "Uimra" (top to down) bali "uasi Mtakatifu" (bottom up). Ma RC na Ma DC ni alama za unyapara. Wanatupeleka mtoni lakini hawawezi kutulazimisha kunywa maji hata kama tuna kiu.
5. Inawezekana kuwa na Halmashauri hata 5 katika Wilaya moja wakati kwa mtindo wa sasa kuna hatari ya Wilaya 2 kugombania Halmashauri Moja.
6. Jopo la wataalam lizame kutafuta namna nyepesi ya wateule wa Rais kufanya kazi na wateule wa wananchi pasipo mgongano wala kutambiana. Siku hizi wateule wa Rais wanawanyanyasa wateule wa wananchi wakati Rais naye ni Mteule wa wananchi.
Ili haya yafanikiwe, semina elekezi zinatakiwa na zisiendeshwe na Rais. Wateule wengi wamejipa haki ya kumdanganya Rais kwa kusifia, kujipendekeza na kumhakikishia Rais kuwa anajua kila kitu.
Hatukuchagua malaika kuwa RAIS wetu. Na hatukuchagua RAIS ili ageuke malaika. Tunamnyima Rais fursa ya kunyenyekea.
KAZI IENDELEE
Sukuma gang ndoto zenu zilizimika tarehe 17/03/2021, sasa hivi chato ni kama kijiji tuChato itakuwa mkoa hilo halina ubishi!
Umekariri!Sukuma gang ndoto zenu zilizimika tarehe 17/03/2021, sasa hivi chato ni kama kijiji tu
Shida ni justification za wasomi hasa wa kagera..ukisoma hata report ya RCC utachecka,, eti utagawanyisha koo na kabila,, harafu eti watapoteza wilaya zenye ardhi nzuri kwa mifugo na kilimo kama hizo wilaya mbili zitakuwa mkoa tofauti.Hoja ya ukabila kuhalalisha mkoa wa CHATO haina mashiko.
Tujiulize faida ya kuanzisha mkoa huo kwa Taifa ni nini?...