Mkakati wa kumrejesha Mbowe CHADEMA mlango wa nyuma wasukwa

Kwani Mbowe amewahi kuondoka Chadema?..
 
Aiseee,
Hii ndiyo njia iliyomng'oa Mrema NCCR Mageuzi na ndiyo hiyo iliyomkimbiza Maalim Seif kwenye chama cha CUF alichoshiriki kukiasisi .
Acha tuone namna kete zinavyo sukumwa.
 
Kwani Lipumba alirudishwaje kwenye cheo? Ni kwamba sheria zinafuatwa kwa hivyo hadi uonyeshe kuwa kwa Mbowe haitawezekana?
Lipumba alirejeshwa kwa mwanya wa uzembe uliofanywa na Chama chini ya Maalim Seif kushindwa kuitisha kikao cha chama ili kuiidhinisha na kuibariki barua ya kujiuzuru kwa Proffesa.

Je kwenye Cdm, Mbowe anaweza akajirejeshaje kwenye uenyekiti kama alivyofanya Lipumba kwa kutumia mwanya wa uzembe?
 
Tanzania kuna viwanda vya uwongo-jakaya kikwete
 
Kama chama kimefungiwa kufanya siasa kwa mizengwe, wahuni watashindwa kufanya hilo?
 
Aiseee,
Hii ndiyo njia iliyomng'oa Mrema NCCR Mageuzi na ndiyo hiyo iliyomkimbiza Maalim Seif kwenye chama cha CUF alichoshiriki kukiasisi .
Acha tuone namna kete zinavyo sukumwa.
Seif na mbowe walikula mabilioni ya mamvi Ili watoe nafasi,lipumba na slaa walipinga
 
Kosa atakalojutia Mbowe mpaka anaingia kaburini ni kutoonesha solidality kwa Mwenyekiti Lisu kipindi kigumu anachopitia.

Mbowe hajawahi kutokea mahakamani wala kwenda jela kumuona Lisu, hii ni dosari kubwa sana kiasi kwamba nimemdharau kabisa Mbowe ni mpuuzi na ameshindwa kuficha hisia zake za kushindwa uchaguzi, hakuwa tayari kwa mabadiriko kama anavyoyahubiri, mabadiriko si kuiondowa tu Ccm, mabadiriko ni haya waliyofanya Chadema kupitisha Anti virus.

Yani akili za kina Mbowe na wenzake hawana tofauti na Bob Wine, yani unashiriki uchaguzi ambao matokeo tayari yanajurikana huko ni kuwahadaa watu.

No reforms, no election.
 
Ni kazi moja pekee inayoweza kumrudisha Mbowe ndani ya CHADEMA; kukiua chama hicho. Hakuna zaidi ya hapo.

Sasa sijui kama kuna yeyote ndani ya CHADEMA sasa hivi anayekubali haya yatokee tena ndani ya chama hicho..

Kama ni juhudi toka nje ya chama, hilo ni swala jingine litakalohitaji mbinu sahihi ndani ya chama kulishughulikia.
 
Sikumbuki vizuri, maana ni muda kitambo toka nimekusoma humu JF ukiwa tofauti na haya uliyoweka hapa; ambayo ninayaunga mkono moja kwa moja.
 
Hii serikali chini ya Samia ni wajinga na wapumbavu kwelikweli...

Hivi wanatoa wapi guts za kumtaka Tundu Lissu atokee mlango wa uani wa mahakama kwa sharti la kukubaliana na "maridhiano feki" wakati walimwingiza kwa mlango wa mbele kwa wanachodai ana kesi ya uhaini..?

Hiki ndicho wenye akili timamu wanakikataa na kutoona dhamira yoyote njema kwenye kinachoitwa "maridhiano" huku ukweli ukiwa kinyume chake: Ulaghai na ujanja ujanja tu wa siasa za kizamani wakidhani Tundu Lissu ni mtu wa akili zinazofanana na za kwao...

It's time for Samia and her collegues to accept the truth, kwamba hizi ni NYAKATI na MAJIRA tofauti kabisa na wakati ule..!

Kama kweli wanataka kulileta taifa hili pamoja, THEY MUST DO THE NEEDFUL which are:

1. Wakubali kuwa, CHADEMA na wafuasi wake, mashabiki wake na mamilioni wanaokiunga mkono nchini kote na dunia ndio kiungo muhimu ktk hiki kinachoitwa MARIDHIANO na kwamba bila uwepo wao, NOTHING IS GOING TO HAPPEN..!!

2. Kama watakubaliana na No.1 hapo juu, then wajiulize swali dogo rahisi tu hili, kwamba:
√ Wanataka ku - achieve nini iwapo kiungo muhimu (i.e CHADEMA + kiongozi wake mkuu Tundu Lissu) wa hiki kinachoitwa maridhiano wako under dentetion? Hizi ni akili gani ndani ya serikali hii zinaamua mambo haya...?

3. Hebu CCM, Samia na Serikali wajaribu kutumia akili zao vizuri kujaribu kufikiri tena hili👇🏻

Kwamba, kama wanawataka CHADEMA washiriki kwenye hiki kinachoitwa MARIDHIANO, hivi wanataka washirikije wakati bado serikali hiyo hiyo kwa magumashi tu wamekifungia chama kufanya shughuli yoyote ya kisiasa isivyo halali na kinyume cha sheria huku wakiwa wamesitisha hata kesi kuendelea ili ku fast track maamuzi ya kisheria?

Uamuzi wa kushiriki au kutoshiriki unatolewa kwa watu kukaa kwenge vikao na kuamua. Lakini hao hao wanaotaka ushiriki wa CHADEMA ktk maridhiano ndio haohao wanaendelea kucheza michezo michafu ya kisiasa ili CHADEMA wasiwe na hata uwezo wa kukaa kikao na kujadiliana...!!

Hawa watu (CCM na serikali yao) ni kama vile wanawaza kwa kutumia makalio yao na kisha kuhara utopolo wao hadharani hivi...

Jambo ngumu Lakini wanataka liishe kwa mbinu chafu ambazo actually haziwezi kutatua tatizo hata 0% tu....!!


CCM, SAMIA & Your Illegitimate Government, it's high time to accept that, YOU WERE WRONG IN EACH AND EVERY STEP...

Nendeni mahakamani kupitia mlango wa mbele, semeni hatuna haja ya kuendelea na kesi ya Tundu Lissu, fungulieni wafungwa wote wa kisiasa wa kesi za uongo, drop every charge against CHADEMA kisha waiteni kwenye mazungumzo mkiwa na hoja zenu na wao wakiwa na hoja zao. Kutaneni katikati. GIVE & TAKE PRINCIPLE lazima izingatiwe. CCM acheni ulafi wa kutaka yote yawe yenu...

Ni njia ngumu kupita lakini ni lazima tupite mo kwa kuwa ndiyo njia sahihi yenye majibu ya kudumu ya changamoto za nchi na taifa hili...!!
 
Duru mbalimbali mitandaoni na ndani ya chama hicho, zinaelea kuwa Mbowe anaandaliwa kuunganisha vyama vikubwa vya siasa ikiwamo CHADEMA, ili kupigania hoja ya maridhiano, huku akijitanabaisha kuwa yeye ndiye mkombozi wa chama hicho.
Kwani hana kumbukumbu kwamba alishindwa kwenye uchaguzi wa viongozi wa chama hicho; au bado hatambui kuwa kuna viongozi wapya?

Yeye atarudi kuunganisha vyama akiwa kama nani?
Ni andiko refu, ambalo pengine faida yake ni kukumbushia matukio ndani ya chama hicho; lakini hakuna mahali popote panapoonyesha wala kuashiria tu kuhusu "MBINU" za kumrudisha Mbowe kwa mlango wa nyuma.

Ni uandishi mzuri, lakini uliokosa lengo muhimu lililosababisha mada ianzishwe.
 
Sikumbuki vizuri, maana ni muda kitambo toka nimekusoma humu JF ukiwa tofauti na haya uliyoweka hapa; ambayo ninayaunga mkono moja kwa moja.
Msimamo wangu nilikuwa naunga mkono Mbowe aendelee kuwa mwenyekiti sikuujuwa ukweli wote.

Ukweli uko wazi Mbowe amefanya makubwa Chadema, lakini kwa hili la kutoonesha ubinadamu kwa Tundu Lisu limemuondolea heshima na kuaminika, na kundi lile la kwenda Chauma ndio limezidi kuonesha kumbe ndani ya chama palikuwa na kundi la wapiga dili.

Matokeo yake Lema alifanya maamuzi sahihi kumuunga mkono Lisu na sasa heshima yake imeongezeka.

Sugu ni rafiki wa Mbowe na ameletwa Chadema na Mbowe lakini amesimama na msimamo wa Chama no reforms no election naye pia heshima yake imeongezeka na sambamba na kushuka kwa heshima ya Mbowe.

Mbowe ni Msaliti.
 
"Who're You" = hapo hapo unatoa $45,000.00 kila mwezi kutafuta favor ya hao hao unaowauliza swali!

Mkuu Palm', hivi kweli bado humjui Samia Suluhu Hassan ni mtu wa aina gani?
Nadhani ni wakati sasa tumchukulie hivyo hivyo alivyo; na tushughulike naye kwa misingi hiyo hiyo.
 
Tugange yafuatayo mkuu 'Matola'; ambayo ni makubwa zaidi ya haya tuliyokwisha yashuhudia.

Mbowe hawezi tena kushika uongozi wa CHADEMA na chama kikaendelea kuwa imara. Hili sasa haliwezekani.
 
Tugange yafuatayo mkuu 'Matola'; ambayo ni makubwa zaidi ya haya tuliyokwisha yashuhudia.

Mbowe hawezi tena kushika uongozi wa CHADEMA na chama kikaendelea kuwa imara. Hili sasa haliwezekani.
Nyakati tayari zinamkataa Mbowe, nyakati hizi zinazotawaliwa na Gen-z chaguo lao ni mtu kama Lisu ndio wapo tayari kumuunga mkono.

Na kosa wamefanya Ccm ni kuwauwa kikatili hawana suluhu tena na Ccm.

Vijana unaowaona Ccm ni vijana wavivu, maslahi na uchawa tu ndio vinawaweka hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…