SoC02 Mkakati wa kupunguza uhalifu kupitia Polisi Jamii

SoC02 Mkakati wa kupunguza uhalifu kupitia Polisi Jamii

Stories of Change - 2022 Competition

Junior Lecturer

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
913
Reaction score
582
Jukumu la kupunguza uhalifu na wahalifu ni jukumu la jamii nzima. Mkuu wa Jeshi la polisi aliye maliza muda wake CPF (CHIEF OF POLISI FORCE) marufu kama IGP (INSP GERAL OF POLICE), SIMON NYANKORO SIRRO, ALIPELEKA WAKAGUZI WA SAIDIZI WA POLISI kwa kila kata katika kata zote nchini Tanzania. Ili wakawe viungo wazuri baina ya Jamii na polisi. Kwa maana ya kuwa Wakaguzi wasaidizi wa polisi maarufu kama polisi kata wata kwenda kuhuburi DHANA YA POLISI JAMII.

NINI MAANA YA POLISI JAMII?
Huu ni muunganiko chanya baina ya jeshi la polisi na wananchi katika masuala mazima ya kupambana na uhuhalifu na wahalifu.

Falsafa ya jeshi la polisi Tanzania ni "usalama wa raia na Mali zao." Ili kuweza kutekeleza falsafa hii ndipo jeshi la polisi sasa lika amua kuanzisha KAMISHENI YA POLISI JAMII ,ndani ya jeshi hilo.

MIRADI YA POLISI JAMII.
Wakaguzi wasaidizi wa Jeshi la polisi walioko katika kila kata nchini wanatakiwa kufanya kazi kwa kushirikiana na ,watendaji wa kata, madiwani, wenyeviti wa mitaa pamoja na watendaji wa mitaa, na ofisi zao zitakuwa kwenye jengo la ofisi ya kata husika na siyo kwenye vituo vya polisi. Hivyo wananchi wamesogezewa huduma zakipolisi katika ofisi za watendaji. Majukumu yao ni kuelimisha jamii juu ya MIRADI YA POLISI JAMII ,ambayo ni kama ifuatayo:-

ULINZI SHIRIKISHI.
Polisi kata anatakiwa kushirikiana na wenyeviti wa mitaa pamoja na watendaji kuanzisha vikundi vya ulinzi shirikishi kwa kila mtaa ndani ya kata na kutoa elimu ya kufanya kazi kwa weledi pasipo kumwonea mtu na kwa kufuta misingi ya sheria. Polisi kata ndiye atakuwa mlezi wa vikundi hivyo vya ulinzi shirikishi ili kuhakisha mitaa inakuwa salama na uhalifu unapungua.

DAWATI LA JINSIA.
Kila kituo cha polisi kina dawati la jinsia wanawake na watoto,. Kesi zote za ukatili na unyanyasaji wa kijinsia zinazo ripotiwa kwenye kata ,polisi kata anatakiwa amwelekeze muhusika au ampeleke mwathirika dawati la jinsia la polisi kwa kushirikiana na afisa ustawi wa jamii ngazi ya kata pamoja na afisa maendeleo nasiyo kuzimaliza kesi hizo mezani mathalani kesi za ulawiti zinazo letwa katani. Tumesema polisi kata ni kiungo baina ya jamii na polisi hivyo anapaswa kuisaidia jamii akiwa kama daraja baina ya jamii na polisi.
Swali, Je,ndugu mwananchi katika kata uliyopo polisi kata anafanya hivyo? Je anapatikana kwenye kata muda wote? Kama hapatikani katani muda wote toa taarifa kwa kiongozi yeyote serikalini,na polisi.

MAJUKUMU YA DAWATI LA JINSIA.
●Kuripoti kesi zote za ukatili na unyaanyasaji wa kijinsia mahakamani na kuhakikisha haki inatendeka kwa kukusanya ushahidi madhubuti.
● Kutoa elimu mashuleni na kwenye mikutano. Polisi kata anatakiwa kuambatana na wahisika wa dawati la jinsia katika mikutano ya mitaa au vijiji na kutoa elimu ya ukatili mashuleni kama itakwavyo ratibiwa na shule husika.
● Kushirikiana na taasisi binafsi zinazo pinga masula ya ukatili katika jamii, kama vile WADADA GENDER BASED VIOLENCE SOLUTION, MTAKUWA, MTOTO KWANZA N.K. polisi kata anatakiwa kuhakisha jamii ina elimika kuhusu masuala ya ukatili na wanapata pa kukimbilia pale wapatapo maswaibu ya ukatili katika jamii.

MRADI MWINGINE NI , UVUVI SALAMA.
Polisi kata anapaswa kutoa elimu kwa wavuvi mathalani kwa yale maeneo ya maziwa,bahari na mito juu ya athari za uvuvi haramu na siyo kukimbilia kukamata tu.

HUDUMA BORA KWA MTEJA WA JESHI LA POLISI.
Huyu polisi kata anawajibu wa kuwasidia wananchi kupata huduma bora pindi wa patapo matatizo,mathalani kuonewa na Askari polisi ambao siyo waaminifu katika kazi yao. Hii itasaidia kujenga na kurudisha imani ya jeshi la polisi.

Mradi mwingine: SAFIRI SALAMA
Askari wa usalama barabarani ni sehemu ya polisi jami. Hivyo polisi kata anapaswa anapo toa elimu kwa wanafunzi , bodaboda ,madereva wa mabasi na hiace sharti askari wa usalama barabarani atoe elimu hiyo.

Mradi wa ULINZI JIRANI
Kupitia polisi jamii wananchi wanapaswa kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzake. Siyo jirani yako anaomba msaada wewe ndo kwanza unabana mlango ,huu siyo.ujirani mwema.

Mradi wa MAZIZI SALAMA
Wananchi hawatakiwi kuwaachia watoto wadogo mifugo yao wakachunge kwani hii inachochea kuongezeka kwa wimbi la wizi wa mifugo.

Mradi wa MUONGO RIKA
Ili kupunguza uhalifu na wahalifu katika jamii kupitia polisi jamii 'matamasha mbalimbali ya michezo kama vile polisi jamii cup yata anzishwa ili kuwaleta vijana pomoja na kuwapa elimu ya masuala mbalimbali mbali ikiwemo, athari za matumizi ya madwa ya kulevya na kutojihusisha na vitendo vya kiuhalifu.

UUSALAMA WETU KWANZA
Jamii inapaswa kuelimishwa umuhimu wa kujilinda wenyewe na kulinda wengine.
Kwa kuitaja miradi hii michache.

MAJUKUMU/WAJIBU WA JAMII KATIKA KUTOKOMEZA UHALIFU.
● Kutoa taarifa fiche za uhalifu na wahalifu.
● Kutambua wageni wote wanao ingia na kutoka katika mtaa kwa kusajili kwenye madaftari maalumu wenyenyumba na wapangaji wao.
● kutojihusisha na vitendo vya kiuhalifu.
● kupunguza matamanio ya uhalifu kwa kufanya yafuatayo:'
_kupeleka pesa banki au kwenye mitandaonya simu.
_ kuweka mageiti imara kwenye milango yao.
_ kuvaa kwa staha.
_ kuacha kuweka mzigo mkubwa dukani.
● kuzingatia malezi bora kwa watoto.
● Kuwa na utayari wa utandawazi hususani mabadiliko ya sayansi nateknolijia ili kuepuka wizi wa mitandaoni.
● Kupinga ukatili na unyanyasaji wa kijinsi katika jamii.
○Kupinga ukatili wa kiuchumi.
Baba na mama wanalima pamoja lakini wakati wa mavuno na mauzo baba ana uza na kuchukua pesa zote huu ni ukatili wa kiuchumi, hivyo polisi jamii lazima isimamie.
○ kupinga ukatili wa kimwili mathalani vipigo.
○Kupinga ukatili wa kingono, mfano ubakaji ,wanawake wengi waliopo kwenye ndoa wana bakwa na waume zao ,na vijana wengi wavivu wanabakwa na majimama marufu kama mashuga mami.
○ kupinga ukatili wa kiakiki,watoto wengi wanajiingiza kwenye vitendo vya kiuhalifu kutokana na kunyanya paliwa kisaikolojia mfano ,mwalimu ana mwambia mwanafunzi " kichwa chako hicho kimejaa sisimizi wametafuna ubongo wako huwezi kufaulu ng'o."

WAJIBU WA POLISI KATA.
● KUTUNZA SIRI
● KUTOA ELIMU KWA JAMII
● KUWA KIUNGO MUHIMU BAINA YA POLISI NA JAMII.
● KUSHIRIKIANA NA WADAU MBALIMBALI KUTOKOMEZA NA KUBAINISHANISHA WAHALIFU KATIKA JAMII.

MWANGA WA MAFANIKIO KATIKA POLISI JAMII.
● Jamii kuwa karibu na polisi na kuwasilisha matitizo yao kwa polisi kata ,na kupatiwa elimu juu ya mambo mbalimbali yahusuyo polisi na jamii pamoja na elimu ya ukatili mashuleni,, Mfano kuna baadhi ya kata kama ,kata ya mhandu,gamboshi,mkolani,mwaisome, mirongo , na nyinginezo nyingi nchini Tanzania matunda yameanza kuonekana.

WAJIBU WA SERIKALI KATIKA POLISI JAMII.
Serikali iendelee kusambaza Waguzi kata wajeshi la polisi kwenye kata ambazo hakuna polisi kata iki kuboresha muunganiko mzuri baina ya jamii na polisi.

Pia polisi katanwengi wanasafiri umbali mrefu kwenda kwenye kata zao,hali itakayo pelekea kuwa katisha tamaa polisi kata wetu, serikali kupitia Ilani ya chama tawala sura ya tano ibara ya 104 kama sikosei imebainisha uwepo wa polisi kata ,hivyo iwape hata usafiri wa pikipiki iki kuwafikia wananchi wengi zaidi.
Hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza na kutokomeza uhalifu katika jamii.

Vilevile serikali ikachunguze wale wote wanao kwenda kinyume na matakwa ya polisi jamii mathalani Vitendo vya Rishwa kwenye kata.

MWISHO POLISI JAMII INAENDA KUWA NGUZO IMARA YA KUTOKOMEZA UHALIFU KATIKA JAMII HIVYO SERIKALI ITOE KIPAUMBELE KWA JESHI LA POLISI.

POLISI ASIWE ADUI WA MWANANCHI BADALA YAKE AWE KIMBILIO LA MWANANCHI.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom