Harrisonngowo
New Member
- Sep 11, 2022
- 1
- 2
Kwanza natoa shukurani zangu nyingi sana kwa kupata nafursa ya kutoa mawazo yangu kuhusu kilimo Tanzania.
Wakulima wamelima kwa muda mrefu sana kwa lengo la kuuza mazao yao na kupata chakula na ziada kidogo ya mazao inayopatikana huuzwa kwa kupata fedha za matumizi ya kilasiku. Uhalisia ni kwamba kilimo kinyachofanywa na wakulima wengi wa Tanzania hakipo kibiashara, kwani wakulima wengi wa Tanzania wanalima kimazoea na sio kimkakati.
Kama tunataka kupata mafanikio katika kilimo, lazima tuzingatie mipango na kuweka mikakati madhubuti ya uzalishajiKwanza kabisa lazima tupange mbinu za uzalishaji na malengo mahususi ya kutanua wigo wa kilimo chetu. kilimo cha kutegemea mvua hakiwezi kukidhi haja ya uzalishaji.
Ni lazima mbinu ya umwagiliaji zitumike kwa kuzingatia hali na uchumi wa nchi yetu. Mojawapo ya mbinu hiyo ni kujenga mabwawa makubwa ili kukinga maji msimu wa mvua nyingi kisha yatumike msimu wa kiangazi.
Maeneo mbali mbali yamekuwa yakipata neema ya mvua nyingi na zakutosha, lakini mvua hizo zimekuwa zikitumika vyema kwa umwagiliaji wakati wa masika. Hakuna sababu ya kuacha maji ya mvua yatiririke bure na kupotea wakati wa masika. Mabwawa makubwa yatasaidia pia mifugo yetu ipate maji wakati wa kiangazi. Wakulima wanaweza kulima mara mbili kwa mwaka kama watawekewa mabwawa. Kuna mabonde mazuri sana yanayopitisha maji ambayo yanaweza kutumika endapo maji hayo yatakingwa. Pili kulima mazao ya chakula na biashara.
Mazao ya chakula hulimwa na wakulima wadogo wadogo, kwakuwa wanafanya kilimo kwa kipimo kidogo na maeneo madogo madogo. Hivyo Kuna haja sasa ya kuwapa mtaji mkubwa matajiri ili wafanye kilimo kwa kipimo kikubwa na wazalishe kwaajili ya biashara.
Mfano matajiri miamoja wataweza kuzalisha mazao ya alizeti kwa kupewa mikopo na maeneo makubwa, jambo hili litawezekana kama watahamasishwa na kupewa ardhi zile sehemu zinazofaa kwa mazao husika. Matajiri hao wakipata vifaa bora na wataalamu wanaweza kuzalisha mazao bora na mengi. Hali inayoweza kuondoa changamoto ya ajira na kuleta maendeleo makubwa kutokana na kuuza mazao nje ya nchi.
Tatu vikosi vya majeshi yetu viboreshwe kwa kufundishwa ili vizalishe mazao bora na mengi. Kufundisha ukakamavu peke yake bila kuwa na taaluma ya uzalishaji wa aina yeyote ni moja ya sababu ya kukosa uzalishaji. vikosi vya JKT Magereza ni moja ya nguvu kazi kubwa ya taifa endapo vitatumika vizuri.
Mabwawa yakijengwa kila sehemu panapofaa, ingependeza kama wataanzisha kikosi cha JKT Magereza waweze kutumia maji hayo na kufanya kilimo cha umwagiliaji na chenye tija. Vilevile vijana wengi wanapenda kufanya kazi ila hawajui waanzie wapi, jambo hili lichukuliwe kama fursa kwa serikali. Hivyo serikali ianzishe makambi maalumu ya JKT kwaajili ya uzalishaji kupitia secta hii nyeti ya kilimo.Wataalamu wetu wa kilimo hawatumiki vizuri.
Kukaa darasani, kusoma na baadae kupata cheti peke yake haitoshi hivyo ni bora wasomi waliomaliza vyuo vikuu wapelekwe nje ya nchi (hasa nchi zinafanya vizuri kwenye kilimo) wakaone kwa vitendo kwa wenzetu ni mbinu gani na utaalamu wa aina gani wanatumia katika kilimo, kisha wakirudi wapewe vituo katika kila mkoa. Vituo hivyo ndivyo vitakavyo fundisha wakulima wote waliobaki hapa nchini.
Wakijifunza kilimo cha umwagiliaji na kuja kufundisha kwa wengine.Ili mambo haya ya kilimo yafanikiwe ni lazima elimu itolewe kwa wakulima wote. Endapo wataalamu watapewa nafasi za kwenda kujifunza elimu yao ije itolewe kitaifa kwanza, kikanda, kimkoa, kiwilaya,na kikata kisha vijiji. Vyombo vya habari virushe vipindi maalumu vya kilimo.
Pia ni vizuri serikali ianzishe stesheni ya televisheni ya kilimo. Halmashauri zetu za miji waanzishe tovuti zao za kushauri na kufundisha mbinu mbali mbali za kilimo. Wakulima wetu wasilime kwa kubahatisha tu, wapewe elimu.Halkadhalka kuwe na mashindano ya wakulima. Matajiri (Watu wenye pesa lakini hawajihushi na kilimo) na wakulima wadogo washindanishwe, wale wote watakaofanya vizuri wape tuzo mbalimbali, ikiwemo kupelekwa nchi za nje ili kujifunza na kuona namna mbalimbali za kilimo zinazofanywa na nchi mbalimbali zinazofanya vizuri katika kilimo.Haya yote yatafanikiwa endapo mipango mizuri itapangwa kwa ajili ya utekelezaji wa kilimo.
Mfano mwaka huu mpango wa kutekeleza utengenezaji wa mabwawa unapangwa, mwaka unaofuata elimu kwa wakulima inatolewa ikienda sambamba na utoaji wa vifaa na pembejeo.Mwaka wa tatu ni utekelezaji wa kilimo chenyewe, nguvu kubwa itaelekezwa kwenye kilimo. mwaka wa nne ni upimaji wa mafanikio na dosari zilizojitokeza, ili kuboresha Zaidi na kuondoa ama kupunguza dosari zilizojitokeza.Utaratibu huu utafanya kilimo kipendwe na wananchi wote na pia vijana wata hamasika kujiingiza kwenye kilimo.
Miaka inayofuata ni kutengeneza maghala kwaajili ya kuhifadhi mazao na kuongeza elimu Zaidi kwa wakulima. Pia kuboresha uzalishaji wa mawazao mbalimbali yanayokidhi masoko ya ndani na kimataifa. Hii itaenda sambamba na utafutaji wa masoko.Kwa mpango huu utafanya Tanzania kuwa mstari wa mbele, pengine kinara katika kuzalisha mazao mbalimbali ndani nan je ya Africa.
Halkadhalika mpango huu unaweza kutumika kwa mifugo na samaki.Lazima tuelewe kuwa uzalishaji wa jambo lolote la maendeleo ni vizuri malengo na mipango madhubuti iwekwe kwa utashi na namna nzuri inayoeleweka kwa elimu na usimamizi mzuri utakao pelekea utekelezaji uwepo wa utekelezaji wa kudumu.

Attachments
Upvote
2