Tetesi: Mkakati wa kuvifuta CHADEMA, CUF waiva

Tetesi: Mkakati wa kuvifuta CHADEMA, CUF waiva

eden kimario

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2015
Posts
10,356
Reaction score
16,379
SIRI imefichuka, kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinashirikiana na baadhi ya viongozi serikalini, kumtumia msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Sales Katabazi Mutungi, ili kuvifuta vyama viwili vikubwa vya upinzani nchini.
aarifa zinasema, vyama ambavyo viko kwenye mkakati wa kuvifuta, ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Chama cha Wananchi (CUF).
Vyama vya Chadema na CUF, kwa sasa ndivyo vyama vikuu vya upinzani nchini.

Wakati CUF ikitikisa Zanzibar, Chadema kimeshika usukani Tanzania Bara; ni miongoni mwa vyama vinne vinavyounda jumuiko la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

“Ndio kuna mkakati wa kutaka kuvifuta vyama viwili vikubwa vya upinzani nchini. Mkakati huu, unaratibiwa na baadhi ya viongozi wa CCM, wanaoshirikiana na wale wa serikali,” ameeleza mfanyakazi mmoja wa ofisi ya msajili kwa sharti la kutotajwa gazetini.

Amesema, “lengo la mpango huu, ni kwamba hadi kufikia mwaka 2020, tunapokwenda kwenye uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani, hakuna chama kikubwa cha upinzani nchini.”

Kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja wiki moja baada ya msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Mutungi, kuitaka Chadema kujieleza ndani ya siku tano, kwa nini kisifutwe kwenye daftari la usajili wa vyama siasa nchini.

Jaji Mutungi ameituhumu Chadema kuwa imekiuka kifungu cha 9(2) cha sheria ya vyama vya siasa na kanuni ya 6(1)(b) ya maadili ya vyama hivyo.

Katika barua yake kwa katibu mkuu wa Chadema, Jaji Mutungi anadai kuwa chama hicho kilifanya maandamano, tarehe 16 Februari 2018 na kusababisha vurugu na baadaye kifo cha Akwilina Akwiline.

Akwilina alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo cha usafirishaji cha taifa (NIT). Alipigwa risasi inayodaiwa kurushwa na askari wa jeshi la polisi akiwa ndani ya daladala, tarehe 16 Februari.

Aidha, kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja wiki moja baada ya jeshi la polisi Visiwani, kuvamia makao makuu ya CUF yaliyopo Mtendeni, Unguja kwa lengo la kufanya upekuzi.

Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui, ameita upekuzi huo, kuwa “ni dhamira ovu sana kwa chama” chake.

Upekuzi kwenye makao makuu ya CUF ulifanyika tarehe 20 Februari 2018. Ulianza saa 12:20 jioni hadi saa 1:30 usiku.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mjini Magharibi, Hassan Nassir Ali, amekiri kufanyika kwa upekuzi huo.

Alisema, jeshi lake limelazimika kuzipekua ofisi za chama hicho, baada ya kupokea taarifa kuwa “ndani ya ofisi hizo kumehifadhiwa silaha, jambo ambalo ni kinyume cha sheria ya vyama vya siasa.”

Alisema, “…baada ya kufanya ukaguzi na kubaini hakuna kitu, tulisaini kuwa tumefanya ukaguzi na hatujagundua kitu chochote cha hatari kinyume cha tulivyopata taarifa. Askari wote waliokuwa wakifanya ulinzi katika eneo hilo tuliwaondoa.”

John Mnyika, naibu katibu mkuu wa Chadema ameliambia gazeti hili kuwa chama chake kimepata taarifa hizo, lakini akaonya kuwa “mkakati huo, hauwezi kufanikiwa.”

Anasema, “tunaelewa. Msajili anasukumwa na serikali kufanikisha dhamira yao ni kukifuta Chadema. Nawaambia hivi, jambo hilo hawaliwezi.”

Juhudi za kumpata Jaji Mutungi kuzungumzia madaia hayo, hazikuweza kufanikiwa. Mara mbili, mwandishi alipiga simu yake, lakini haikuweza kupokelewa.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, mpango wa kuvifuta vyama hivi, utaanzia Chadema na baadaye kufutwa kwa CUF; vyama hivyo vitafutwa kabla ya kumalizika kwa mwaka huu.

Chanzo: Mwanahalisi online
 
Mbona hawa jamaa wanahangaika sana? Japikuwa kubenea sio Wa kuaminiwa ssna lakini hali halisi tunaiona hakuna Baja ya kuambiwa...

.
.
.
.
26/4 is loading.......
 
Hakuna anayevifuta bali vinajifuta vyenyewe. Huwezi kushiriki uchaguzi ukaambulia kata moja kati ya 43 then ukasema chama kinafutwa
ficha umbulula wako basi, hivi hizi chaguzi za marudio unaweza kusema nazo ni chaguzi ? yalitokea yote hukuona ? watu wanapigwa, wasimamizi wanazuiliwa pamoja na hila nyingi bado mnajitia kuwa mlishinda kata 42 ? je kilichotokea hapa juzi kinondoni na siha hukuona ? mabazazi mkamuua mpendwa wetu akwilina(r.i.p), alafu unajinasibu kwamba mnashinda kihalali ?

ipo siku kibao kitawageukia punda nyie, damu ya mtu haimwagiki bure, haki haidhulumiwi. hata kama sio leo, au mwaka huu, vyeo vina mwisho.
kuna mbegu mbaya sana inamea kwenye kizazi cha sasa, siku ikilipuka hapatakuwa salama, rev ni kitu kitacho-take time, years over years, ila ipo siku.
 
Hakuna anayevifuta bali vinajifuta vyenyewe. Huwezi kushiriki uchaguzi ukaambulia kata moja kati ya 43 then ukasema chama kinafutwa
Mkuu piga nyundo taratibu ukijua chadema kuna watu wana presha.Hoja kama hii itasababisha chadema wengi kulazwa kwa presha .Hurumia wagonjwa wa presha walioko chadema
 
Kufa kwa vyama vya upinzan sio mwisho wa upinzan zaidi ccm wanatengeneza makundi ya m23.
Mabadiliko ni fikra za mwanadamu ambazo zipo ktk hisia zao ccm wanahamisha maji kwa kutumia net kupeleka kwenye ndoo.
 
Hakuna anayevifuta bali vinajifuta vyenyewe. Huwezi kushiriki uchaguzi ukaambulia kata moja kati ya 43 then ukasema chama kinafutwa
Ule uchaguzi au uchafuzi hata hiyo kata moja sijui mkurugenz alikuwa mlokole hapendi dhuluma na ujambazi.

"Magufuli nakulipa mshahara,posho na gari halafu unatangaza mpinzan kashinda"
 
Mkuu piga nyundo taratibu ukijua chadema kuna watu wana presha.Hoja kama hii itasababisha chadema wengi kulazwa kwa presha .Hurumia wagonjwa wa presha walioko chadema
Mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe,mtaji wa CCM ni watu waliozaliwa kwa njia zisozahalalishwa na Bwana Mungu ,kama wewe.
 
Mleta mada eden kimario mchaga umechambua hasa sisi huku kijijini kwa mbowe tumefurahi sana yaani wote akina mushi,mosha,akina mtui,manka,munisi,lema,mrema,ukoo wa mtei yaani wote wamefurahi na mchango wako koko
Acha Ukabila wewe

Ova
 
ficha umbulula wako basi, hivi hizi chaguzi za marudio unaweza kusema nazo ni chaguzi ? yalitokea yote hukuona ? watu wanapigwa, wasimamizi wanazuiliwa pamoja na hila nyingi bado mnajitia kuwa mlishinda kata 42 ? je kilichotokea hapa juzi kinondoni na siha hukuona ? mabazazi mkamuua mpendwa wetu akwilina(r.i.p), alafu unajinasibu kwamba mnashinda kihalali ?

ipo siku kibao kitawageukia punda nyie, damu ya mtu haimwagiki bure, haki haidhulumiwi. hata kama sio leo, au mwaka huu, vyeo vina mwisho.
kuna mbegu mbaya sana inamea kwenye kizazi cha sasa, siku ikilipuka hapatakuwa salama, rev ni kitu kitacho-take time, years over years, ila ipo siku.
Hapa Tanzania ni kazi kubwa kuwaelemisha wafuasi wa kakobe na wachaga wa chadema hawa kuwaelemisha mpk mtu Mohammed afufuke
 
Back
Top Bottom