Adidja Palmer, maarufu kama "Vybz Kartel," alihukumiwa kifungo cha maisha Machi 13, 2014, baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya Clive "Lizard" Williams pamoja na wenzake watatu, Shawn, Andre St. John, na Kahira.
Aidha, Mahakama ya Rufaa ya Jamaica imeamua kutokusikiliza tena kesi hiyo kutokana na hali mbaya ya kiafya ya Vybz Kartel, anayesumbuliwa na ugonjwa wa "Graves Diseases".
Licha ya kuwa jela, Vybz Kartel aliendelea na kazi zake za muziki ambapo mwaka 2016 alitoa wimbo wake wa "Fever" ambao una (views) milioni 62 YouTube.
Ni nyimbo gani ya mkali huyu unaikubali sana?