Mkanda wa jeshi (Herpes zoster/ shingles) fahamu kuhusu dalili na tiba yake

Shine

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2011
Posts
11,481
Reaction score
1,368


BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU KUHUSU TATIZO HILI
Wakuu muu hali gani naomba kujua kinachosababisha mkanda wa jeshi na indicator zake pia madhara yake na kami huu ugongwa una tiba
Nawakilisha
---
swali la nyongeza: mkanda wa jeshi unaitwaje kwa lugha ya kiingereza/medical language?nataka ni google ili nijielimishe zaidi juu ya hili gonjwa au sijui ni dalili ya ugonjwa?
UFAFNUZI WA KINA WA UGONJWA WA MKANDA WA JESHI
Kwa takribani miongo mitatu sasa, tumeshuhudia ongezeko kubwa la mlipuko wa ugonjwa wa mkanda wa jeshi linaloendana na ongezeko la hususani ugonjwa wa UKIMWI. Hali hii imefanya baadhi ya watu kuamini kuwa, ugonjwa huu ni dalili ya wazi kabisa ya mtu kuwa na VVU, imani ambayo kwa kiasi kikubwa ina ukweli ndani yake ingawa si kwa wote wanaopatwa nao.Mkanda wa jeshi au shingles au herpes zoster kwa majina ya

kitabibu ni ugonjwa unaosababishwa na virus wa aina ya Varicella-zoster ambao pia husababisha ugonjwa wa tetekuwanga au chickenpox. Ugonjwa huu huathiri ngozi ambapo huambatana na vipele na michubuko kama ya kuungua yenye kuambatana na maumivu makali.

Visababishi
Kama tulivyokwisha tangulia kueleza hapo juu, ugonjwa huu husababishwa na virus aina ya Varicella-zoster ambao pia husababisha ugonjwa wa

tetekuwanga. Baada ya mtu kupatwa na tetekuwanga, virus hawa hubaki katika hali ya kupooza/kutokuwa na madhara (dormant) katika neva fulani za mwili. Baada ya miaka kadhaa, iwapo itatokea kinga ya mwili ikashuka kwa sababu yoyote ile, virus hawa hupata tena nguvu/kuwa na madhara (active), kuibuka na kusababisha ugonjwa wa mkanda wa jeshi.Kwa kawaida shambulio la mkanda wa jeshi hutokea mara moja maishani ingawa laweza kujirudia.

Vihatarishi
Mkanda wa jeshi unaweza kumpata mtu wa umri wowote ule ingawa watu walio katika makundi haya wapo katika hatari kubwa zaidi:
Wenye umri wa zaidi ya miaka 60.

Mtu aliyewahi kuugua ugonjwa wa tetekuwanga kabla ya umri wa mwaka mmoja. Watu ambao kinga yao ya mwili imepungua kwa sababu mbalimbali kama vile matumizi ya aina fulan za dawa, magonjwa kama vile maambukizi ya VVU (HIV/AIDS), saratani na utapiamlo.

Je, mkanda wa jeshi huambukizwa?
Hapana ugonjwa huu hauambukizwi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine! Lakini iwapo itatokea mtoto au mtu mzima ambaye hajawahi kupatwa na ugonjwa wa tetekuwanga maishani mwake na ambaye pia hajawahi kupata chanjo dhidi ya ugonjwa huo akakutana na mtu mwenye ugonjwa wa mkanda wa jeshi, mtoto au mtu huyo atapatwa na ugonjwa tetekuwanga na siyo mkanda wa jeshi.

Dalili
- Dalili ya awali kabisa ya mkanda wa jeshi ni maumivu makali sehemu fulani/ upande mmoja wa mwili yakiambatana na hali ya ganzi na hisia za kuungua kwenye ngozi. Maumivu pamoja na hisia za kuungua huwa makali sana na hutokea kabla ya vipele/michubuko kutokea kwenye ngozi.

- Kawaida, vipele au michubuko huusisha eneo fulani la mwili kuanzia kwenye uti wa mgongo kuzunguka kuelekea eneo la tumbo au kifua.

- Michubuko pia inaweza kutokea kwenye maeneo yanayozunguka uso, macho, mdomo au masikio.Dalili nyingine ni pamoja na:

- Maumivu ya tumbo

  • Homa
  • Maumivu ya mwili mzima
  • Vidonda sehemu za siri
  • Maumivu ya kichwa
  • Maumivu ya viungo
  • Kuvimba kwa mitoki/ matezi

Iwapo neva za maeneo ya uso zitaathiriwa, mgonjwa anaweza kupatwa na matatizo ya kuona, kuonja, au kusikia.
Vipimo
Ni nadra sana kufanya Vipimo maalum kwa ajili ya utambuzi wa ugonjwa huu, isipokuwa kwa nchi zilizoendelea. Kwa ujumla utambuzi wa ugonjwa huu hufanyika kwa kuchukua historia ya mgonjwa na kuchunguza sehemu ya ngozi iliyoathiriwa.
Vipimo vya damu yaani FBP huonesha ongezeko la chembe nyeupe za damu na antibodies dhidi ya virus wa tetekuwanga.
Matibabu
Matibabu ya mkanda wa jeshi hujumuisha matumizi ya dawa kama vile Acyclovir, Famciclovir na Valacyclovir kwa ajili ya kuua virus wanaosababisha ugonwja huu. Dawa hizi husaidia kupunguza maumivu, kuzuia madhara zaidi ya ugonjwa huu na kupunguza muda wa ugonjwa.

Dawa hizi hutolewa angalau saa 72 baada ya mgonjwa kuanza kuhisi maumivu na hali ya kuungua. Ni vema dawa zianze kutumika kabla ya vipele/michubuko kujitokeza.
Jamii ya dawa za corticosteroids kama vile prednisolone husaidia kupunguza maumivu na uvimbe kwa badhi ya wagonjwa. Dawa nyingine zinazofaa kutumika ni pamoja na jamii ya antihistamines kwa ajili ya kupunguza muwasho, dawa za maumivu, calamine lotion kwa ajili ya kupunguza muwasho. Aidha mgonjwa anashauriwa kupata mapumziko ya kutosha

Matarajio
Mkanda wa jeshi kwa kawaida huchukua kati ya wiki mbili hadi tatu kupona wenyewe. Aidha ni nadra sana kwa ugonjwa huu kujirudia tena. Iwapo neva zinazothibiti mwendo katika mwili zitakuwa zimeathirika, mgonjwa anaweza kupatwa na kupooza kwa muda au kwa kudumu kwa sehemu ya mwili iliyoathiriwa. Wakati mwingine, maumivu yanayosababishwa na mkanda wa jeshi yanaweza kudumu kwa miezi mpaka mwaka hata baada ya mgonjwa kupona kabisa. Maumivu haya yanayojulikana kama postherpetic neuralgia kwa kawaida huwakumba wagonjwa wenye umri wa zaidi ya miaka 60 na husababishwa na uharibifu katika neva za mwili.

Madhara
Madhara ya mkanda wa jeshi ni pamoja na kupatwa na shambulio jingine la ugonjwa huu, maambukizi ya bakteria, upofu iwapo eneo la jicho litahusika, ukiziwi, maambukizi katika utando wa ubongo (encephalitis), uwepo wa vimelea kwenye damu (sepsis) au ugonjwa unaoitwa Ramsay Hunt Syndrome iwapo utahusisha neva za uso.

Kinga
Epuka kabisa kugusa eneo lenye vipele au michubuko kwa mtu mwenye mkanda wa jeshi au tetekuwanga iwapo hujawahi kuugua au kupata chanjo ya tetekuwanga.
Ni vema kupata chanjo dhidi ya virus wa Varicella zoster kama inapatikana katika nchi au eneo ulilopo . Tafiti zimeonesha kuwa, watu wazima wanaopata chanjo hii wana uwezekano mdogo sana wa kupata madhara ya mkanda wa jeshi kuliko wale wasiochanjwa.


BAADHI YA MICHANGO ILIYOTOLWEWA NA WADAU
---
---
---
 
Mmh! in most cases ni HIV!
 
Swali la nyongeza: mkanda wa jeshi unaitwaje kwa lugha ya kiingereza/medical language?nataka ni google ili nijielimishe zaidi juu ya hili gonjwa au sijui ni dalili ya ugonjwa?
 
NgumiJiwe, inaitwa herpeszoster (sina hakika na spellings) . Google.
Mkanda wa jeshi ni shambulio la nerves by virus. Hii inatokana mostly na upungufu wa kinga mwilini either baada ya kuugua muda mrefu au baada ya stress ya muda mrefu. Magonjwa ya virusi hayana tiba zaidi ya kuu-boost mwili ili uweze kupambana zaidi. Hebu google kwa maelezo zaidi
 
shukrani mkuu King'asti na ubarikiwe. Wacha nikajielimishe!
 
Ukipata mkanda wa jeshi, kapime VIH haraka iwezekanavyo.
 
Wakuu muu hali gani naomba kujua kinachosababisha mkanda wa jeshi na indicator zake pia madhara yake na kami huu ugongwa una tiba
Nawakilisha
Ugonjwa wa mkanda wa jeshi (herpes zoster aka shingles) unasababishwa na virus anayeitwa Varecella zoster, huyu huwa anaingia mwilini mapema sana katika umri mdogo, anasababisha ugonjwa wa "chiken pox". Ugonjwa ambao huambatana na homa na vipele, ambayo huisha vyenyewe.

Kuisha kwa chicken pox hakumaanishi kuwa Virus wameisha, bali huwa wanaenda kwenye sehemu za mwisho za mishipa ya fahamu (nerve endings) na huwa wanakaa humo na kuwa dormant, kwa maneno mwngine, kwa kuwa kinga ya mwili ingali juu, basi hawa wadudu hawana madhara, na ndo maana wanakimbilia kule kusikofikiwa kiurahisi na seli za kinga. Ikiwa kinga ya mwili inapungua kwa sababu yeyote ile ama kutokana na HIV/AIDS, advanced cancer, lishe duni, na nyingine,..

basi hawa wadudu wanapata nguvu na kujitokeza from nerve endings walipokuwa. Wanasababisha painful blisters, na wanatambaa na mishipa ya fahamu,..ndio maana hizo blisters ama vidonda vinakuwa kama vinafata mstari, ama eneo husika. Mara nyingi mgongoni, kiunoni, kifuani, ama mabegani,..kwa kiswahili "mkanda wa jeshi" kwa kuwa ipo sehemu ambazo wanajeshi hufungia mkanda.

Matibabu: mkanda wa jeshi hauna dawa,..bali huisha wenyewe ikiwa kinga inarejea, kwa hiyo dawa wanazopewa huwa ni kwa ajili ya maumivu tu,..wakati mwingine kuzuia infections za bacteria ambazo husababisha usaha, ama kupunguza tu idadi ya virusi kuzuia visizaliane zaidi.

Madhara,..zaidi ya mabaka yanayodumu, sifahamu madhara mengine ukiacha maumivu makali. mara chache hushambulia macho na huweza kukufanya kuwa kipofu, ama kushambulia nerves zinazosaidia misuli, na kufanya ushindwe kutuimia kiungo husika.

Kupata mkanda wa jeshi hakuna maana kuwa Una UKIMWI,..ila wengi wanaopata haswa kwa mazingira yetu basi ni kweli wanakuwa na ukimwi, maana hiyo ndio sababu kuu ya kupunguza kinga ya mwili Tanzania

Stun
 

dah kazi nzuri sn brother,kwa upande wangu umenifungua mambo mengi ambayo sikuwa na ufahamu nayo,safi sn.
 
Mimi niliambiwa mtu mwenye mkanda wa jeshi ana ngoma.
 
Mimi niliambiwa mtu mwenye mkanda wa jeshi ana ngoma.
kama by definition ngoma ni upungufu wa kinga mwilini, then yes..mkanda wa jeshi unahusiana na ngoma,..ila hausababishwi na ngoma
 
stun,
Mkuu nashukuru kwa maelezo yako mazuri
 
dah kazi nzuri sn brother,kwa upande wangu umenifungua mambo mengi ambayo sikuwa na ufahamu nayo,safi sn.

Siyo wewe tu hata mimi na naamini tutakuwa wengi tuliyo elimika kutokana na yeye
 
Poleni na majukumu wadau, nina kitu kinanisumbua akili yangu. Iko hivi: kwa muda wa karibia wiki mbili kuna mstari ulijitokeza juu ya kitovu, na unakua kila kunapokucha kukatiza kwenye tumbo. Je wataalamu huu ndio mwanzo wa kuwa na hili tatizo, au niondoe shaka juu ya hili?
 
je una dalili gani zaidi? andika zaidi upate kueleweka! ni tovuni tu? ni vipelevipele au la! au umenenepa kitambi kinakutoka?:thinking:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…