DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Nimefanikiwa kupita kwenye Stendi ya Bukoba ambayo iliezwa na Viongozi wetu wa Serikali kuwa inafanyiwa ukarabati mkubwa, nimekuta kwa sasa ujenzi unaendelea baada ya kusimama kwa zaidi mwaka mzima.
Mnamo Januari 2025 nilileta hoja hapa Jukwaani nikaeleza kwamba ujenzi umesimama na mkandarasi hayupo 'site' licha ya ukarabati huo kutakiwa kuwa umekamilika.
Nilieleza kwamba Mkandarasi alitakiwa kutumia kipindi cha Miezi sita kukamilisha mradi huo tokea ilipotangazwa Mwezi October 2023, hivyo ni kwa mujibu wa taarifa zilizokuwepo rasmi za kiofisi.
Katika maelezo ya awali nilieleza kuwa eneo hilo ni kama lilikuwa limetelekezwa kutokana na kuwa Mkandarasi alikuwa amesawazisha eneo hilo tu bila kujenga miundombinu kama ilivyooneshwa kwenye mchoro.
Itakumbukwa ukarabati huo ulitokana na fedha takribani Bilioni Moja iliyotolewa Serikali kupitia Rais Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kutumika kujenga Stendi ya Kyakairabwa, lakini badae pesa hiyo ilibadilishiwa matumizi baada ya vikao vya makubaliano ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba.
Hata hivyo nilitoa wito kwa kwa mamlaka kufuatilia, kutokana na kuonesha wasiwasi wa fedha hizo kupigwa kama ambavyo awali kabla ya pesa kubadilishiwa matumizi, ambapo Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa alidai kuwa pesa hizo zilikuwa zimeshaanza kutengenezewa mazingira ya upigaji.
Pia soma ~ Ukarabati wa Kituo cha Mabasi Bukoba kwa "Bilioni Moja ya Rais Samia" hakuna kinachoendelea, Je, Watumishi wamepiga dili tena?