Ntemi Kazwile
JF-Expert Member
- May 14, 2010
- 2,182
- 308
Best huielewi hii TV? Ni kama tawi la ccm ndo maana wanakuwa biased. Kumbuka huyo mkurugenzi wao aliletwa na mgonjwa wetu toka alikokuwa, so anatetea meza mkuu na ndo maana hata waloko chini yake wanafanya atakavyo. Kubwa ni kuwapiga chini na tuendelee kuwasubiri hadi 31st Okt mtaona kama hawatajiunga nasi kuimba nyimbo za ukombozi wa nchi yetu!
Suala la-uprofeshno katika vitu vingi hapa kwetu bado ni ndoto..!
TBC1 wanaboa kuliko maelezo. Ukiangalia unaona wazi kabisa wanapendelea CCM na ni aibu kwa chombo cha umma kufanya mambo anayofanya Tido Mhando. Wakifanya Clouds, Channel 10, Uhuru, n.k unaweza usishituke kwa sababu tunajua mafisadi wamewekeza kuhakikisha CCM inaendelea kuwa madarakani kwa sababu hilo ndilo chaka lao.
Mwisho wao hata hivyo unakuja
Jamani CCM ndio wanaowaweka hapa mjini mnadhani watafanyaje kama si kupendelea aliyekuwa madarakani?Hata chama cha upinzani kikichukua nchi itakuwa vivo hivyo kwa kupendelewa hasa wakati wa uchaguzi kama huu.Cha msingi ni kuangalia namna ajira zao zinavyopatikana si kwa style hii ya uswahiba mnapeana chombo cha umma kinacholipiwa na wananchi wote huku mkitaka kupendelewa wakati fulani mkiwa na shida
TBC hawana aibu hebu fikiria kila siku asubuhi kwenye uchambuzi wa magazeti lazima kila mchambuzi(msoma magazeti) aanze na gazeti la Uhuru. Sasa hapo utasema ni chombo cha uma , tumeingiliwa.
mimi niliona channel ten sikuamini macho yangu kwa umati hule!!ccm mnayokazi inabidi mjiweketayari kwani hata mkiiba vibaya tutawakamata mwisho wasiku tunacho waomba msije mkaiweka hii nchi kwenye machafuko kwani watu wameamka mkiwanyima haki yao hawatakubali ni bora busara ikatumika kam alivyofanya mh.kenneth kaunda wa zambia.
TV stations karibia zote zina upendeleo wa ajbu sana kwa CCM.
Hakuna hata yenye afadhali, wasipo'chakachua' kwenye taharifa ya habari 'watachakachua' kwenye makala.
Mimi siangalii TBC1, kwani kwangu hata chaneli yake namba saba nimeichakachua, na ni marafuku kwa yeyeto kuisearch.
na TBC 1 wamekuaja na gia nyingine, siku ya pili leo hawarushi kampeni za DR. Slaa siku hiyo hiyo, wanarusha siku inayofuata asubuhi muda ambao wengi wanachakarika kwenda makazini
Dahhh wanachakachua mpaka picha
na TBC 1 wamekuaja na gia nyingine, siku ya pili leo hawarushi kampeni za DR. Slaa siku hiyo hiyo, wanarusha siku inayofuata asubuhi muda ambao wengi wanachakarika kwenda makazini
Leo mchana wamerusha wakionyesha kichwa tu cha Dr Slaa.
Mafisadi TBC wasio na haya wala soni.