Umenikumbusha issue ya mafuta... yalipofikia Tshs 1,350/= (petrol) kila mtu alipiga kelele, serikali kwa usanii mkubwa ikaonekana kuwajali wananchi kupitia EWURA, wakapunguza yakarejea Tshs 1,200/= na watanzania (wadanganyika) wakapoa kabisa na kuchekelea kuwa 'walau yamepungua'... nyuma ya pazia kilichofanyika ni kupandisha 'daily' kwa sh. 10 hivi na mpaka sasa nimefahamishwa kuwa Petrol (ndani ya miezi kama miwili tu...!) imefikia Tshs 1,550/= kwa lita moja.Tutazoea tu!
Hata bei za mafuta ilikua hivyo hivyo.walipandisha kwa ghafla watu wakapiga kelele.wakashusha kisha wakaanza kupandisha kidogokidogo
Leo asubuhi nilikuwa nataka kununua vocha ya vodacom na muuzaji akaniambia bado sh 100. Nikamuuliza kulikoni, akaniambia vodacom wamepandisha gharama kwa sh 100 na hiyo ni kwa vocha za aina zote. Naomba kama kuna mdau yoyote mwenye taarifa zaidi kuhusu hii ishu atusaide tafadhali.
....nilipong'aka nikaambiwa kuwa kuanzia Julai mosi bei za vocha zimepanda bei tangu Julai Mosi. Nikanyong'onyea na kuondoka.
Du hii hali sasa inazingua, jana nilitaka kumpatia vitasa muuza duka pale vijana kinondoni aliponiuzia Tigo ya buku tano kwa buku tano mia tano.
Na watanzania asilimia kubwa huishia hivi...
Unanyong'onyea kisha unaondoka hahahahahaha!
Tanzania inaweza kuongozeka kirahisi nimeamini...
Muuzaji hana kosa, wala usithubutu kumtendea visivyo... lakini haya mekundu ndiyo concern yangu....!Kwi kwi kwi!
Sasa ningefanyaje mkubwa? Options nilizokuwa nazo ni kwa wakati huo (asubuhi ya leo) ni hizi!-
2. Kumshikisha adabu muuzaji na kukutana na mkono wa dola
Kwa sababu nilikuwa nina haraka ya kuwahi kazini.....
Mimi nasema hivi...hii nchi tunakoelekea sio kwenyewe.......ok kampuni zimeamua for whatever reasons kupandisha gharama ya voucher zao...imewazuia nini kuwatangazia wateja kabla hizo rates hazijaanza kutumika? mbona wakiwa wanafanya promotions za kuwaibia maskini hela zao wanatangaza mpaka masikio yanauma?Kwanini ulipie hela zaidi kwa vocha ambayo tayari imeandikwa thamani yake? Sidhani hii inaweza kusimama hata mbele ya sheria....
WIZI MTUPU!
Kama tulisikiliza vizuri bajeti 2009/2010, VAT sasa inatozwa kwenye vocha na siyo Muda wa hewani. Nadhani ndio sababu. Hata hivyo, makampuni ya simu yanatakiwa kubeba lawama hizi kwa kutowafahamisha wateja wao, maana sio watu wote walisikiliza na kufuatilia vizuri marekebisho ya kodi hasa VAT kwenye masuala mbalimbali.