Mkanganyiko katika Gharama za Vocha za Simu

Mkanganyiko katika Gharama za Vocha za Simu

Zain inawatahadharisha wateja wao kutonunua vocha tofauti na bei iliyoandikwa kwenye vocha zenyewe. Usiongeze hata senti... Hii ni kwa mujibu wa taarifa yao kwa vyombo vya habari, naitafuta nikiipata nitaitundika kwenye hii mada...
 
Mi jana jioni nimeenda kununua tiGO nusu sehemu ambayo huwa nanunua 500 tu wakaniambia gharama zimepanda akaniambia muuzaji nichukue ila baadae nimpelekea hamsin yake, mi nkafikri ananizuga! inawezekana ni kweli mtu wangu wmaepandisha!
 
Hii ndio Ilani ya CCM, Sasa hapa lazima tujiulize kuwa hizo vocha zilikuwa tayari katika bei husika kabla ya Mwaka wa Bajeti inakuaje sasa inakuwa hivyo??
 
Muuzaji hana kosa, wala usithubutu kumtendea visivyo... lakini haya mekundu ndiyo concern yangu....!
Jamani jamani jamani jamani jamani jamani! Mimi ni mmoja wapo wa wauza Vocha za simu mitandao yote. Sisi hatuna makosa. Malalamiko yote kuhusu kupanda kwa vocha muwapelekee serikali au makampuni ya simu.
Hivi kama wewe ni mfanyabiashara umenunua bidha kwa sh. 10,000 je utaenda kuiuza kwa sh. 10,000 hiyohiyo? Jibu ni hapana. Ndivyo ilivyo katika vocha za simu kwa bei ya jumla. Baadhi ya sehemu nyingine vocha za jumla kwa mfano 1000 za voda tunauziwa hiyo hiyo 1000, hivi kama wewe utaiuza kwa sh. ngapi? Na wakati huo huo bado hujapigia hesabu matumizi ya nauli uliyoitumia kufuata hizo vocha. Jamani msitulaumu bure.

Hata mimi Vocha za sh. 500 nauza 550, za 1,000 nauza 1,100 n.k.
 
Zain inawatahadharisha wateja wao kutonunua vocha tofauti na bei iliyoandikwa kwenye vocha zenyewe. Usiongeze hata senti... Hii ni kwa mujibu wa taarifa yao kwa vyombo vya habari, naitafuta nikiipata nitaitundika kwenye hii mada...

Its about time tuanze kuwatosa hawa vodacom, hakuna sababu ya kuendelea kubembelezana wakati watoa huduma wanaongezeka kila siku! Sasatel si wameshaanza?
 
Burn!

Hapo umechomekea leo asubuhi nimenunua tigo ya Elfu tano kwa bei hiyo hiyo! ya buku tano muza kadi kakufua tu !!!

Watumiaji wa Voda walishauriwa na Mzee Mwanakijiji waachane na mtandao ambao umeingizwa hapa TZ kwa rushwa ya CCM hamkusikia litakalowafika ni shauri yenu hampaswi kulalamika.

Wewe Burn hata TIGO wangepandisha kwa rate inayotumika ya Tshs.60 kwa dakika Tigo kwa Tigo bado inalipa. Kama uko Zain au Voda ambao inabidi uchague watu kumi au watano kwa bei ya Tshs.60 kwa dakika always ianakula kwako! Hivi nyie watu wa KIJANI hamkujifunza hata Table mlipokuwa bush school now chekechea !!!!

Coming back to the stupid TCRA hivi kukimbilia kusajili simu kwa vile tu watu wezi wachache wametumiwa ujumbe wa matusi inasaidia kitu gani kuleta nafuu ya bei kwa watumiaji wa mitandao ya simu. Huko ulaya wanasajili simu and people have proper ID's LAKINI wizi wa simu na matusi mbele kwa mbele!!! Prof. Mkoma You are really dead and buried!!! Magari yenye ukubwa kama VX yanaibwa na ktokomea hayaonekani kwani si yamesajiliwa na majina ya wabunge!! Unatarajia simu isiibwe simply kwa kusajili acheni upuuzi hata watu wenyewe hawajulikani shit!!!!

Kwa kweli haihitajiki mtu kuwa Profesa kuliona hilo. The challenge brought by TIGO kwa kushusha bei mpaka kufika 60/= per minute ni fundisho tosha kwa wapumbavu wa CCM I mean the JMK aka Matonya GVT kwamba tumekuwa tukiibiwa kichizi na makampuni ya simu!! now to Mkoma kwa nini usitumie Tigo kama Guinea pig na kupanga bei kama anavyofanya Sekirasa kwenye usafiri wa mabasi?? That man is not a Professor lakini take trouble and ask the wananchi on the streets ! Definately he is popular than many of our ministers!!! Na anafuatilia

The bottom line nawashauri mjiunge na TIGO you won't regret tigo can as well expand and take up the influx na kumonopolize the market kama walivyofanya Tanzania Breweries walipoiua Kibo Breweries kule Moshi!! To HELL WITH ZAIN AND VODA kwani wana kiburi cha CCM.

Jana nilikuwa nanunua vocha nikaambiwa Vodacom peke yao ndio wamepandisha bei, nikaikumbuka rai hii. Kwakweli its high time kuachana na mtandao huu wenye kila sura na dalili zote za wizi.
 
Jana nilikuwa nanunua vocha nikaambiwa Vodacom peke yao ndio wamepandisha bei, nikaikumbuka rai hii. Kwakweli its high time kuachana na mtandao huu wenye kila sura na dalili zote za wizi.
Hata mimi leo July 3 nauza vocha za Vodacom kwa sh. 550, 1100, 2200, 3300, 5500. Na zingine zote nauza bei ya kawaida yaani 500, 1000 n.k. kwa sababu bado nina stock ya zamani ila nikienda kuchukua stock mpya kama bei itakuwa juu basi tutauza kama zilivyo za Vodacom
 
kule kwetu bunghwangoko nimepata taarifa kuwa zimepanda toka june, sasa zimefika mjini.

nchi yangu tanzania!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Na watanzania asilimia kubwa huishia hivi...

Unanyong'onyea kisha unaondoka hahahahahaha!

Tanzania inaweza kuongozeka kirahisi nimeamini...

Mkuu si ndo kitu baba yetu wa Taifa alitufanya. Tuwe wapole na wanyonge...au sio? There is a price to everything...hahaha
 
Ukitia bajeti ya Serikali ya 2009/2010 kuwa bei za vinywaji na gharama za simu zimeongezeka.

Sasa kwa utaratibu huo na makampuni ya simu na vinywaji lazima yapandishe huduma zake na hivyo zigo lote kenda kwa mtumiaji wa mwisho (Mlaji)

Sasa kwa kuwa vocha hizo zilitengenezwa toka awali za kiasi cha 500, 1000 n.k sasa zitaongezwa bei kiasi mpaka stock yao iishe ndio watoe tolea maalum la vocha kulingana na bajeti.
 
Of course huu ni wizi na ubabaishaji!! Mimi nina wasiwasi na hawa wauza vocha wa reja reja! Inawezekana wamejipandishia bei wenyewe tu! Hawa Service Providers wanachoweza kufanya ni kupandisha rates zao, basi. Unaweza kujiuliza, je, hizi vocha zitabadilishwa? yaani wataanza kutoa ya 1100, 2200, n.k.? Sitegemei! Bahati nzuri mie asubuhi hii huko kwetu shamba tabata nimenunua vocha za 8,000 bila kutapeliwa!
 
Jamani jamani jamani jamani jamani jamani! Mimi ni mmoja wapo wa wauza Vocha za simu mitandao yote. Sisi hatuna makosa. Malalamiko yote kuhusu kupanda kwa vocha muwapelekee serikali au makampuni ya simu.
Hivi kama wewe ni mfanyabiashara umenunua bidha kwa sh. 10,000 je utaenda kuiuza kwa sh. 10,000 hiyohiyo? Jibu ni hapana. Ndivyo ilivyo katika vocha za simu kwa bei ya jumla. Baadhi ya sehemu nyingine vocha za jumla kwa mfano 1000 za voda tunauziwa hiyo hiyo 1000, hivi kama wewe utaiuza kwa sh. ngapi? Na wakati huo huo bado hujapigia hesabu matumizi ya nauli uliyoitumia kufuata hizo vocha. Jamani msitulaumu bure.

Hata mimi Vocha za sh. 500 nauza 550, za 1,000 nauza 1,100 n.k.
ASANTE KWA TAARIFA TUTAENDA KUNUNU HUKO HUKO MNAKONUNUA. inawezekana kwa ufahamu wenu mnaenda kununua kwa wauzaji wa reja reja badala ya JUMLA, asante kwa TAARIFA, nitakuwa nanunua za wiki 3 kupunguza garama za kusafiri mpaka kwenye huduma

Its about time tuanze kuwatosa hawa vodacom, hakuna sababu ya kuendelea kubembelezana wakati watoa huduma wanaongezeka kila siku! Sasatel si wameshaanza?
KWANI ni kwa VOUCHER za VODACOM peke yake?
 
Last edited:
Hizi mia mia za juu ndo tunalipia gharama za mashangingi, posho za wadosi mjengoni n.k wao hizi mia mia hawalipi ila tunawalipia sisi yaani nchi hii natamani kufa hata kesho.
 
Jamani jamani jamani jamani jamani jamani! Mimi ni mmoja wapo wa wauza Vocha za simu mitandao yote. Sisi hatuna makosa. Malalamiko yote kuhusu kupanda kwa vocha muwapelekee serikali au makampuni ya simu.
Hivi kama wewe ni mfanyabiashara umenunua bidha kwa sh. 10,000 je utaenda kuiuza kwa sh. 10,000 hiyohiyo? Jibu ni hapana. Ndivyo ilivyo katika vocha za simu kwa bei ya jumla. Baadhi ya sehemu nyingine vocha za jumla kwa mfano 1000 za voda tunauziwa hiyo hiyo 1000, hivi kama wewe utaiuza kwa sh. ngapi? Na wakati huo huo bado hujapigia hesabu matumizi ya nauli uliyoitumia kufuata hizo vocha. Jamani msitulaumu bure.

Hata mimi Vocha za sh. 500 nauza 550, za 1,000 nauza 1,100 n.k.
nyie wauzaji ndo mlitakiwa mtoe angalizo kwa hayo makampuni ya simu.....ukinipa vocha imeandikwa 1000 sikupi zaidi ya hiyo ..........habari ndo hiyo...mnataka kuuza 1100 print vouchers with that amount on it(tusaidieni kufikisha ujumbe kwa maboss wenu)
 
Hizi mia mia za juu ndo tunalipia gharama za mashangingi, posho za wadosi mjengoni n.k wao hizi mia mia hawalipi ila tunawalipia sisi yaani nchi hii natamani kufa hata kesho.
weeee fide temea mate chini maana Izraili yuko nyuma yako atasepa na ako karoho kako chacha hivi.
by the way mie nimenunua asubuhi nimwembia muuzaji sina mia mbili ntampelekea lakini navuta muda ili nijue kama kweli au si kweli
 
Hawa ni mafisadi, wanatafuta pesa za takrima kwenye uchaguzi wa 2010. My advice...nunua line nyingine not Vodacom, wateja wengi wakianza kuwahama watapunguza bei tuu...
 
weeee fide temea mate chini maana Izraili yuko nyuma yako atasepa na ako karoho kako chacha hivi.
by the way mie nimenunua asubuhi nimwembia muuzaji sina mia mbili ntampelekea lakini navuta muda ili nijue kama kweli au si kweli

hehehehe natema mate juu kisha nayadaka. Nawahurumia watu wa vijijini maana wkt wa buku wao ilikuwa buku jiti mbili sasa hivi si itakuwa buku jero kama sio gwede kabisa.
 
JAMANI HIYO NI KODI YA ONGEZEKO LA THAMANI VAT nalo linamkuta mnununzi wa mwisho ambae ni mimi na wewe,awali ya hapo serikali ilikuwa inachukua VAT toka kwa muuzaji wa jumla na hawa wauzaji wadogowadogo walikuwa wanapewa kwa bei ya jumla isiyo na VAT lakini sasa nao wanalipa VAT hivyo faida inakuwa ndogo kwao nao wanaangukia kutuumiza sisi watu wa mwisho, MUNGU IBARIKI TANZANIA.! LAKINI ISIWABARIKI VIONGOZI WAKE NA MAFISADI.
 
Serikali imeweka VAT kwenye vocha, sasa kivipi tunataka bei isipande?
Tatizo labda ni mawasiliano mabovu ya kampuni na wateja, na pia vocha zilikuwa zishachapishwa kabla ya sheria hii ya VAT kutangazwa, nadhani vocha zijazo zitasema Bei Excluding VAT au kitu kama hicho.
 
hehehehe natema mate juu kisha nayadaka. Nawahurumia watu wa vijijini maana wkt wa buku wao ilikuwa buku jiti mbili sasa hivi si itakuwa buku jero kama sio gwede kabisa.
hapo chacha........
 
Back
Top Bottom