Nafuatilia bunge live saa hii. Ninachokiona ni mkanganyiko mkubwa wa hoja juu ya suala la bandari na "mkataba" na kampuni ya Dubai ya DPW.
Nimegungua kuwa upo mkanganyiko mkubwa kati ya wabunge, huku wengine wakisema haya ni makubaliano ya awali kuhusu mikataba itakayofuata.
Wapo wanaosema kuwa huu sio uwekezaji, wala ubia bali ni makubaliano ya ushirikiano kati ya Tz na Dubai.
Wengine wanasema document hii ni kuhusu mambo makuu matatu; uendeshaji, endelezaji na uboreshaji na sio uwekezaji.
Wengine wanasema huu ni mkataba msingi, juu yake itafuata mikataba katika specific areas. Tusiwe na hofu mikataba itakuja.
Wabunge wengine wanasema "makubaliano" haya yana kikomo cha muda, wengine wanasema hakuna haja ya kuwa na ukomo wa muda kwani mikataba itakayofuata ndio itaonesha ukomo wa mikataba.
Naogopa kuwa wabunge wetu bado hawajui vizuri kinachoendelea kuhusu suala la bandari. Kama "mkataba mama" hautakuwa na misingi mizuri basi tujue kuwa mikataba yote itakayofuata ambayo itajengwa juu wa mkataba msingi wa sasa, haitakuwa na msingi sahihi na kuna uwezekano mkubwa kuwa tukapigwa.
Kwa bahati mbaya leo nimegundua kuwa wabunge wetu walio wengi hawana uelewa mzuri wa mambo na kuna uwezekano mkubwa wa kuisaliti nchi bila hata kujua kutokana na ujinga wa wawakilishi wetu.
TUSISAHAU KUWA IWE NI MKATABA, MAKUBALIANO, MARIDHIANO, ETC, YOTE YANA NGUVU YA KUFUNGA (BINDING FORCE) NA NI HATARI KWETU ENDAPO KUNA VIFUNGU VISIVYOELEWEKA VIZURI.
Wataalamu wetu fafanueni na wekeni wazi mambo haya kwa watanzania.