Ndugu wana JF,
Nimekuwa nikufuatilia mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya na niakagundua kwa watanzania wengi na pia vyombo vingi vya habari kama si vyote vimejikata sana katika masuala ya Muungano tu, yani serikali mbili au tatu na mambo mengine kutoguswa kabisa.Si kwamba naona hawafanyi kazi nzuri, hapana ila pia sehem zingine pia ziangaliwe kwa makini.
Mfano kwenye rasimu ya katiba

- ibara ya 105(3) inasema kila mkoa kwa upande wa Tanzania bara na wilaya kwa upande wa Tanzania Zanzibar vitakuwa ni jmbo la uchaguzi, Papo hapo jukumu la ugawaji wa mikoa na wilaya liko chini ya serkali za washirika, utata unakuja, kwani hakuna mchakato ulioainishwa wa uanzishwaji wa mikoa au wilaya, kwani upande mmoja wa muungano ukianzisha mkoa au wilaya automatically unaathiri majimbo ya uchaguzi na uwiano wa wabunge ndani ya bunge la JMT
- Ibara ya 72(5) inasema "Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu,kupoteza sifa za uchaguzi, kutomudu kazi zake ktukana na maradhi ya akili, mwili au kusindwa kutekeleza kazi na shughuli za Rais basi Makamu wa Rais ataapishwa na kushika madara ya Rais kwa muda uliobaki ktk kipindi cha miaka mitano na kwa masharti yaliyoelezwa ktk ibbara ya 76. Kwa maoni yangu ni kwamba , ikitokea Rais na Makamu wake hawapatani ni rahisi kwa makamu kutengengeza mazingira ya kumwondoa madarakani Rais kwan katiba imesema wazi yeye ndiye atakye kuwa Rais kwa kipindi kilicho baki hata kama Rais aliyekuwepo alihudumu kwa mwezi mmojatu. Pia mara nyingi kwa hapa Tz makamu wa Rais huwa ni kama political figure, na watznzania humchagua Rais na kuingia mkata na Rais na si makamu wake,iweje makamu aje kuwa Rais kirahis hv bila kuchaguliwa?