Mkanganyiko ndani ya rasimu ya katiba

Mkanganyiko ndani ya rasimu ya katiba

OSHABU

Senior Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
111
Reaction score
47
Ndugu wana JF,
Nimekuwa nikufuatilia mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya na niakagundua kwa watanzania wengi na pia vyombo vingi vya habari kama si vyote vimejikata sana katika masuala ya Muungano tu, yani serikali mbili au tatu na mambo mengine kutoguswa kabisa.Si kwamba naona hawafanyi kazi nzuri, hapana ila pia sehem zingine pia ziangaliwe kwa makini.
Mfano kwenye rasimu ya katiba
  1. ibara ya 105(3) inasema kila mkoa kwa upande wa Tanzania bara na wilaya kwa upande wa Tanzania Zanzibar vitakuwa ni jmbo la uchaguzi, Papo hapo jukumu la ugawaji wa mikoa na wilaya liko chini ya serkali za washirika, utata unakuja, kwani hakuna mchakato ulioainishwa wa uanzishwaji wa mikoa au wilaya, kwani upande mmoja wa muungano ukianzisha mkoa au wilaya automatically unaathiri majimbo ya uchaguzi na uwiano wa wabunge ndani ya bunge la JMT
  2. Ibara ya 72(5) inasema "Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu,kupoteza sifa za uchaguzi, kutomudu kazi zake ktukana na maradhi ya akili, mwili au kusindwa kutekeleza kazi na shughuli za Rais basi Makamu wa Rais ataapishwa na kushika madara ya Rais kwa muda uliobaki ktk kipindi cha miaka mitano na kwa masharti yaliyoelezwa ktk ibbara ya 76. Kwa maoni yangu ni kwamba , ikitokea Rais na Makamu wake hawapatani ni rahisi kwa makamu kutengengeza mazingira ya kumwondoa madarakani Rais kwan katiba imesema wazi yeye ndiye atakye kuwa Rais kwa kipindi kilicho baki hata kama Rais aliyekuwepo alihudumu kwa mwezi mmojatu. Pia mara nyingi kwa hapa Tz makamu wa Rais huwa ni kama political figure, na watznzania humchagua Rais na kuingia mkata na Rais na si makamu wake,iweje makamu aje kuwa Rais kirahis hv bila kuchaguliwa?
Wadau naombeni muongeze mengine ambayo mnayaona ni tata kwenye rasimu hii ya katiba ili kwa pamoja tuijenge nchi yetu. Pia ni rai yangu kuwa vyombo vya habari, wanaharakati, wanasiasa na wananchi wote kwa ujumla tutaanza kunagalia pia na vipengele vingine vilivyoko kwenye katiba na kuvijadili vzuri
 
binafsi mimi niko na hoja nyingi sana juu ya hii rasimu ya katiba lakin leo naomba niweke hizi hoja mbili ambazo zimekuwa mentioned ndani ya RASIMU HII.

  1. HIVI kuna ulazima gani wa kuwalazimisha watu wote kuimba wimbo wa Taifa ndani ya Katiba?? JE kwa kufanya hivyo hatuoni kwamba tunawalazimisha hata wale wasiomwamini Mungu kuimba ama kukiri kitu wasichokitaka/ kikubali?
  2. pia tusemapo Tanzania Bara, Tanzania visiwani sion kama tuko sahihi kabisa. sababu zangu ni kwamba je Kigamboni iko bara ama kisiwani?? pia kuna maeneo ya bara amabayo yako pwani mfani pwani ya mtwara, tanga, dsm, je kusema huku ni bara tu hatukosei. Kwann tusibaki na jina la Tanganyika kama ilivyokuwa awali??
naomba kusahihishwa hapa.
cc Nguruvi3. Mchambuzi Zinedine
 
Last edited by a moderator:

gfsonwin kuhusu wimbo wa taifa hiyo ni alama tu ya utambulisho na sidhani kama kuna kushikiwa mtutu. Labda unieleze ni kwa jinsi gani umeona rasimu inalazimisha watu kuhusu kipengele hicho. Hapo tutaweza kuwa na mjadala zaidi.

Pili, kuhusu Tanzania bara, hili jina lilitokuja baada ya kuvunja Tanganyika na Zanzibar.
Tukawa na Tanzania bara na Tanzania visiwani. Zanzibar wakaamua kurudi katika jina lao.

Kinachofanyika sasa hivi ni kujaribu kukwepa jina Tanganyika kwasababu kurudi kwa Tanganyika kunaweza kuwa na nguvu zaidi ya jina kuliko Tanzania na hivyo kupunguza nguvu za Tanzania ambayo ni supreme kaliko washirika.

Kwahiyo maelezo yako kuhusu visiwa na sehemu za pwani ni sawa na mkanganyiko unatokana na huko kulazimishwa. Muhimu hapa ni kuwaambia wajumbe wa mabaraza kuwa sisi tunahitaji Tanganyika kwanza.

Kama itakuwepo Tanzania bara, na visiwani iwepo kinyume chake ni Tanganyika na Zanzibar.
 
mkuu wangu Nguruvi3 swala la wimbo wa taifa liko bayana kabaisa kwenye katiba na ndio maana hata huu wimbo waliosema kwamba ni alama ya taifa ikawepo.

hebu soma maneno haya ambayo nimenukuu ndani ya katiba

2

HIVYO BASI, KATIBA HII YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

ILIYOPENDEKEZWA NA BUNGE MAALUM LA KATIBA

imetungwa naSISI WANANCHI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

kupitia kura YA MAONI kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo, na kuhakikisha kuwa Jamhuri

ya Muungano wa Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia na utawala wa sheria, kujitegemea na isiyokuwa na dini..

Halafu njoo usome hapa chini tena
Alama na Siku
Kuu za Taifa

3.
-(1) Alama za Taifa ni:
(a)

Bendera ya Taifa;
(b)

Wimbo wa Taifa; na
(c)

Nembo ya Taifa,
sasa kabla sijaenda mbali zaid kaka yangu waweza kuniambia hapa wanamaanisha nn?? je huon kwamba kuna sababu ya kubadili hata huu wimbo wa taifa??
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3 sioni sababu ya kuwa na jina la Tanzania bara manake ndio kuna bara lkn Tanzania hii inayoitwa bara bado imecontain na eneo la pwani na kisiwa na huoni kwamba kwa kusema tanzania visiwani basi hata kigamboni tunaipa Zanzibar??

Binafsi ningependekeza kwamba jina LETU LA TANGANYIKA NA VISIWAN WABAKI NA ZANZIBAR. MBONA NCHI KAMA ZAIRE ILIGAWANYIKA WALIRUDI KWENYE MAJINA YAO YA ASILI??
 
Last edited by a moderator:
neo la Jamhuri ya
Muungano

2.
Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara
ikijumuisha sehemu yake ya bahari na eneo lote la Zanzibar ikijumuisha
sehemu yake ya bahari.

HEBU SOMA HII SEHEMU YA 1 IBARA KUU YA 2 UONE JINSI AMBAVYO JINA HILI LA TANZANIA BARA HALIFIT IN. KAMA ZANZIBAR WAMEBAKI NA ZANZIBAR YAO BASI NA SISI TUNATAKA TUBAKI NA TANGANYIKA YETU.
 
HEBU SMA TENA KIEPNGELE HIKI HAPA CHINI

Utumishi wa
Umma

15.
-(1) Zawadi au kitu chochote kitakachotolewa kwa mtumishi wa umma katika shug

huli za kiserikali ni zawadi kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na itawasilishwa kwa Katibu

Mkuu Kiongozi kupitia kwa Katibu Mkuu wa Wizara au taasisi ya Serikali inayohusika, akiainisha:

(a)aina ya zawadi;

(b)thamani ya zawadi;

(c)sababu ya kupewa zawadi; na

(d)mtu au mamlaka iliyotoa zawadi hiyo.

SASA HAPA MIMI SIJAELEWA JAMBO MOJA JE ZAWADI AMBAZO WATUMISH WA UMMA HUPEWA HADI SIKU ZA MEIMOSI KAMA ZAO INABIDI ZIWE ZINARUDISHWA KWENYE OFISI??

MATHALAN TUZO AMBAZO WATU HUPOKEA NYINGINE HUANDIKWA MAJINA YAO JE KUNASABABU YYTE YA TUZO HIZI KUZIPELEKA OFISINI??

mimi nilikuwa nafikiri hivi zaadi ambazo mtu hupewa nje ama ndani ya nchi basi zawadi hizi ziorodheshwe na hapo iangaliwe zawadi hii kapewa yeye kama yeyey ama yeye kama ofisi?? ikumbukwe kwamba kuna wanaoapewa zawadi kwasababu ya utendaji wao mzuri lk nje ya ofic wanayofanyia utendaji wao usingalionekana na mbaya zaid watendaji hawa baadhi yao zawadi zao huandikwa majina yao.

nafikiri inahitajika more clarification hapa.

ni mtazamo wangu tu wandugu, naomba kusahihishwa.

turudi kwenye kipengele ha haki za binadamu.

ndugu mtoa mada na wachangiaji wengine wote kuna jambo ambalo naliona kama ni tofauti kabisa.

Kwanza nianze hivi je rasimu hii ni rasimu ya katiba ya JMT na sio ya Tanganyika sio?? sasa je hatuoni kwamba sisi wa Tanganyika tumenyimwa aki yetu hapa??

turudi kwanza kwenye katiba ya Zanzibar katiba hii watalaam wake waliiandika vizuri sana kwenye katiba yao wamebainisha haki za binadamu/mtu yyte yule wakiwa na maana ya mzanzibar, mtanganyika na hata mgeni kutoka nje, lkn pia wakawa na kipengele cha haki za raia ( mtanzania) hawakuishia hapo wakawa na haki za raia wa zanzibar.............

sisi kwenye rasmu hii tunataja haki za binadamu/ mtu na haki za raia je Mtanganyika nayeye hana haki zake humu??

unless kuwe na fairness lkwenye haya maswala vinginevyo hiki kipengele ni batili kabisa.

cc Nguruvi3, Mchambuzi
 
Last edited by a moderator:
Nami nadhani hapa suala la mchakato wa katiba ya Bara ungeanza. Lakini kwa hali inavyokwenda ni wazi kwamba serikali tatu itakuwa ni ndoto. Tume ya Warioba baada ya kuona Zanzibar wana katiba yao nao wakaona si vibaya na Bara kuwa na katiba yake. Hapa automatically serikali ya tatu ya Muungano inazaliwa. Sasa kwa bahati mbaya hii serikali ya tatu itakufa ingali mimba, hivyo kufanya rasimu iliyoandaliwa kuwa mfu nayo
 
mkuu wangu Nguruvi3 swala la wimbo wa taifa liko bayana kabaisa kwenye katiba na ndio maana hata huu wimbo waliosema kwamba ni alama ya taifa ikawepo.hebu soma maneno haya ambayo nimenukuu ndani ya katibaHIVYO BASI, KATIBA HII YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
LIYOPENDEKEZWA NA BUNGE MAALUM LA KATIBA

imetungwa naSISI WANANCHI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

kupitia kura YA MAONI kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo, na kuhakikisha kuwa Jamhuri

ya Muungano wa Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia na utawala wa sheria, kujitegemea na isiyokuwa na dini..

Halafu njoo usome hapa chini tena Alama na Siku Kuu za Taifa3.
-(1) Alama za Taifa ni:
(a)Bendera ya Taifa;
(b)Wimbo wa Taifa; na
(c)Nembo ya Taifa,
sasa kabla sijaenda mbali zaid kaka yangu waweza kuniambia hapa wanamaanisha nn?? je huon kwamba kuna sababu ya kubadili hata huu wimbo wa taifa??
gfsonwin , kuna mambo ambayo ukiwa kama mwananchi huwezi kuyakwepa. Mfano, huwezi kusema wewe si Mtanzania hata kama hupendi Tanzania kwasababu wewe ni Mtanzania by default. Huwezi kusema hupendi bendera ya taifa kwasababu hiyo ndiyo alama ya taifa lako. Na wimbo wa taifa nao ni kama hivyo.

Endapo tatizo ni kutajwa mungu basi hilo linakuwa tofauti. Labda ungesema wimbo wa taifa usimtaje mungu ningeweza kukubaliana nawe kwa upande fulani hasa tukizingatia kuwa wapo wasioamini uwepo wa mungu na wao wana haki.
Lakini pia lazima tukubali kuwa kuna majority kwa baadhi ya mambo. Katika rasimu kama 40% watakataa na 60% watakubali rasimu itapitishwa na kuwa katiba. Hii haina maana 40% wamedharauliwa hapana, ni utaratibu wa ku move mambo vinginevyo hatutakuwa na katiba.

Kwa mtazamo huo kama 60% watasema wimbo wa taifa uwe na neno mungu basi hiyo ndiyo majority na lazima tukubaliane nayo. Vingenevyo tukimsikiliza kila mmoja kwa matakwa yake tunaweza kuishia kupata kundi la 20% linalosema wimbo wa taifa utaje shetani, je, utakuabaliana na kundi hilo? Nadhani jibu ni hapana, sasa kama yupo asiye na dini na bado hakubaliani na neno mungu au shetani lazima tuwe na modality ya kuhakikisha kuwa kuna muafaka.
Modality hiyo ni majority consensus ambayo inatokana majority
 
kwangu mimi hiki ndicho nilicho maanisha kwamba wimbo wa taifa uandikwe upya ama neno Mungu litolewe uwe unaibwa ukiwa neutral usimtaje Mungu wala shetani.

lakin hoja hii ni ndogo sana ukiangalia kwa makini kuna hoja nzito kam vile za kuwanyima waTanganyika haki yao kwenye ardhi yao. ukisoma katiba utaskia kila raia anahaki ya kumiliki ardhi, lkn ukienda kwa katiba ya Zanzibar wao wamesema bayana kwamba kila mzaznibar anahaki ya kumiliki ardhi. sasa sisi hata ardhi yetu wao wanaweza kuimili lkn sisi hatuwez mbona haya ni mapungufu ya wazi?
 
gfsonwin ukiisoma rasimu vizuri kuna kipengele kinachosema sheria zozote zitakazokuwa upande mmoja wa washirika zitahusika katika usawa kwa upande mwingine. Kwa mfano, kama zanzibar watakuwa na sheri zinazozuia ajira kwa Watangayika, basi sheria hiyo itakuwa kwa Tanganyika. Kimeandikwa kifundi sana nitakitafuta ukisome.

Kuhusu suala la ardhi hilo nalo kama mambo mengine limepatiwa ufumbuzi. Ardhi haipo katika mambo 7 yaliyopendekezwa katika serikali ya muungano. Kwahiyo hakuna shaka kuwa limekuwa addressed kulingana na concern zako.
 
hiko kipengele nimekisoma lkn pia natatizika na huu msemo wake kwamba kitakuwa na usawa na mshirika mwingine. kwani nilichojiuliza kama zaznibar wameweza kukiandika basi ni wazi hata sisi tulipaswa kuwa na kipengele chetu. binafsi nimeona kama hapa ni njia moja ya kupooza machungu ya watanganyika .

unless kama itakuwepo serikali 3 basi ni dhahiri kwamba haya yatapatiwa ufunguzi.
 
Na kwa hakika rasimu imeandikwa kwa kulenga serikali 3 na hiyo ndio maana iliyokusudiwa.

Tatizo ni kuwa hiyo Tanganyika imeandikiwa taratibu ikiwa tumboni, siku itakapozaliwa itakuta sheria hiyo (kama rasimu itabaki kama ilivyo). Hapo kuna kuwanyima haki Watanganyika.
Ni kwa mukatadha huo Tanganyika irudi sasa hivi na tunaomba watu waunge mkono hoja.

Hakuna Tanzania bara tunataka Tanganyika. Kama itakuweo bara tutauliza visiwani ipo wapi?
Hakuna tatizo la kurudia jina letu zuri, Kongo wamefanya hivyo kama Burma, Zimbabwe, Msumbiji n.k. sisi hatutakuwa wa kwanza na hilo ni jukumu leyu kuutafuta utaifa wetu.

Tuwasaidie wenezetu wa znz kujitoa katika muungano haraka sana.
 
sasa hapa nashukuru na nafurah kwamba umeunga oja yangu mkono ya kwamba HAKUNA NCHI INAYOITWA TANZANIA BARA BALI IPO TANGANYIKA na kama ndivyo basi wananchi turudishe jina letu la TANGANYIKA.

hALAFU SIJUI KWANN TUMEKUWA WAGUMU KUELEWA KWAMBA HAKI ZA WATANGANYIKA ZIMEWEKWA KAPUNI. TANZANIA ni jina lililotoholewa kutokana na neno Tnganyika= TAN na Zaznibar =ZANIA sasa kuitwa tanzania bara ni wazi kwamba tunakubali akuwa watumwa wa wazanzibar..........................

mbaya zaid iliyo Tanzania visiwani ni ipi??
 
Back
Top Bottom