KERO Mkanganyiko pesa ya Kujikimu Kada ya Ualimu Shinyanga DC

KERO Mkanganyiko pesa ya Kujikimu Kada ya Ualimu Shinyanga DC

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mahmud20

New Member
Joined
Jul 22, 2024
Posts
1
Reaction score
0
Baada ya Serikali kutoa fedha kwa ajiri ya malipo ya posho za kujikimu kwa waajiriwa wapya wa mwaka 2026.

Hali imekuwa tofauti katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Ambapo watumishi wapya walio chini ya Idara ya Elimu kata wamelipwa pesa pungufu tofauti na miongozo ya serikali inavyotaka.

Baada ya malipo hayo kufanyika tarehe 01/07/2026, watumishi wengi walishangaa kukuta pesa iliyowekwa kwenye account zao ni tofauti na muongozo wa fedha za kujikimu.

Wengi wamelipwa kati ya tsh 590, 000 hadi tsh 680,000. Haijarishi Elimu yako ni shahada, stashahada au cheti.

Hali hii ni tofauti na halmashauri nyingine ambapo wengi wamelipwa kati ya shilingi 900,000 na 1, 000,000tsh.

Viongozi wa idara ya Elimu walipoombwa kutoa ufafanuzi walikwepa kwa kuwaambia watumishi waandike kutoa majibu.

Hii imeonekana ni njia ya kuwafanya watumishi hawa wakate tamaa kufuatilia fedha zao.

Kwani barua zinaweza kuchukua muda mrefu sana kujibiwa.

Tunaomba Serikali itusaidie sisi watumishi tuweze kupata fedha zetu zote kama inavyotakiwa.

Tunaomba pia serikali ichunguze halmashauri hii ya Ushetu kwani kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu hasahasa kwenye fedha za kujikimu.

Na watumishi wanapolalamika wanapokoea vitisho kuwa watahamishiwa kwenye maeneo ya vijijini.

TUNASHUKURU.
 
Back
Top Bottom