Mkanganyiko wa Katiba ya Sasa

Mkanganyiko wa Katiba ya Sasa

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
3,197
Reaction score
7,677
Ukiingalia katiba ya Tanzania, ni kama vile ilifikiriwa kuwa wakati wote Rais atakuwa Mtanganyika.

Tanganyika iliungana na Zanzibar kwenye mambo machache, nadhani wakati ule yalikuwa 17 tu.

Hayo mambo 17 pekee ndiyo yalikuwa chini ya Serikali ya JMT. Mambo hayo yalikuwa ni pamoja na Ulinzi, Mambo ya ndani, Uhusiano wa Kimataifa, Sarafu, Elimu ya juu, n.k.

Mambo yaliyobakia kama vile Afya, Elimu, Utamaduni, Kilimo, Biashara, yalibakia kuwa chini serikali za maeneo (Tanganyika na Zanzibar). Mambo haya kwa upande wa Zanzibar yangesimamiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya Rais wa Zanzibar. Na kwa upande wa Tanganyika, yangesimamiwa na Serikali ya JMT chini ya Rais wa JMT. Kwa mantiki hiyo, ni kwamba kuna wakati Rais wa JMT anakuwa Rais wa nchi ya Tanzania (anaposimamia utekelezaji wa yale mambo ya Muungano), na kuna wakati anakuwa Rais wa Tanganyika (anapotekeleza mambo yale ya Tanganyika yasiyo chini ya Muungano).

Mambo ya Kufikirisha:

1) Kila raia wa Zanzibar ni raia wa Tanzania

2) Siyo kila raia wa Tanzania ni raia wa Zanzibar.

3) Kila raia wa Zanzibar na Tanganyika ana haki ya kushika uongozi au kuwa mtumishi kwenye taasisi zinazosimamia mambo yale ya Muungano.

?? Jana nimesikia kuwa eti Rais wa JMT ameagiza serikali ya JMT inunue CT scan machines kwaajili ya hospitali zote za mikoa ya bara na visiwani. Ina maana suala la Afya, nalo limeingizwa kwenye mambo ya muungano? Au mkanganyiko wa katiba unamfanya Rais akose kutambua mipaka ya mamlaka ya Rais wa JMT kwenye mambo yasiyo ya muungano?

JUMUISHO
Kuna wakati Rais wa JMT anafanya kazi kama Mkuu wa nchi ya JMT (wakati huo anasimamia yale mambo ya Muungano tu) na kuna wakati anafanya kazi kama Rais wa Tanganyika (anasimamia mambo yale yasiyo ya Muungano).

SWALI
Raia wa Zanzibar, ambaye siyo raia wa Tanganyika, anakuwa na uhalali gani kuwa Rais wa Tanganyika (ili kusimamia mambo yale yasiyo ya muungano)? Au Mwalimu Nyerere alidhani wakati wote, Rais wa JMT atatoka bara tu?

Waliosema katiba ina mkanganyiko, naona wapo sahihi sana. Na aliyesema Tanganyika imejivika koti la muungano, naye yupo sahihi.

KATIBA MPYA YENYE UFAFANUZI SAHIHI NA WENYE MANTIKI HAIIEPUKIKI.
 
Halafu Zanzibar inapewa mashine 5.Mkoa wa Morogoro unapewa mashine 1 wakati una idadi kubwa ya watu kuliko Zanzibar.
Rais kama hafahamu mipaka yake katika masuala yasiyo ya muungano, washauri wake waache unafiki, wamwambie ukweli juu ya kipi ni sahihi na kipi siyo sahihi. Hawa hawa, siku za mbeleni watamgeuka, na kusema alitumia madaraka vibaya.

Rais kwa vile ni Mzanzibari (kama alivyotamka mwenyewe), akitumia nafasi yake ya kuwa Rais wa JMT, kutumia pesa za Tanganyika kuhudumia Zanzibar, atasababisha chuki dhidi yake na dhidi ya Zanzibar, jambo ambalo siyo jema kwa utengamano wa muungano.

Kama pesa itakayonunua hizo CT scan machines ni mkopo au msaada, basi sehemu ya pesa hiyo ipelekewe Zanzibar (kwa kadiri ya mkataba wa muungano), na atakayekuwa na uwezo wa kuisemea pesa hiyo ifanye nini ni Rais wa Zanzibar, siyo Rais wa JMT.
 
Kama fedha za kununulia CT scan machines ni za mkopo nafuu yaani concessional loan ambapo Zanzibar ni beneficiary sababu ni sehemu ya JMT, ni sawa! Ila kinachochanganya ni kwa nini agizo litoke kwa Kiongozi mkuu. Zanzibar wana wizara ya afya, Raisi, baraza lao la mawaziri, haikuwa busara wao wenyewe waamue?
 
Wakati unataja mambo ya muungano umesema yalikuws 17 si sahihi. Ukayataja baadhi. Mikopo ya nje ni katika hayo ya muungano.

Fedha zimepatikana kwa mkopo ambazo ndo zitanunua hizo city scan. Zanzibar haziwahusu? Ndio nikasema uisome vizuri katiba.

Kimsingi katiba ina mikanganyiko mingi. No vyema kuisemea kwa ujumla (in totality) badala ya kunyofoa kidogokidogo. Zanzibar imekuwa ikinyimwa haki nyingi na watu hawasemi kwa kisingizio cha kulinda muungano
 
Wakati unataja mambo ya muungano umesema yalikuws 17 si sahihi. Ukayataja baadhi. Mikopo ya nje ni katika hayo ya muungano. Fedha zimepatikana kwa mkopo ambazo ndo zitanunua hizo city scan. Zanzibar haziwahusu? Ndio nikasema uisome vizuri katiba. Kimsingi katiba ina mikanganyiko mingi. No vyema kuisemea kwa ujumla (in totality) badala ya kunyofoa kidogokidogo. Zanzibar imekuwa ikinyimwa haki nyingi na watu hawasemi kwa kisingizio cha kulinda muungano
Malipo ya hiyo mikopo yanatokana na fedha zipi? sio madini ya Shinyanga yalipe mkopo wa CT scan iliyonunuliwa Zanzibar
 
Sidhani na sioni mkanganyiko wowote kuhusu Katiba na Tunu yetu ya Muungano, ikiwemo uongozi na mgawanyo wa fedha za mikopo ya Kimataifa. Muungano wetu ni unique na Katiba yetu ndiyo imelifikisha taifa hapa .

Pili, rejea hizo fedha Rais alizoagiza ziende Zanzibar. Kama ni za IMF huo ni mkopo wa Kimataifa kwa Tanzania. Zanzibar haikopi ktk taasisi za Breton woods kama IMF na WB. Hivyo mkopo huo ni wa nchi yetu na Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, ina haki ya kunufaika.

NB: Sisi wajukuu wa Mwalimu Nyerere tunachukizwa mno na maneno madogo madogo kuhusu Muungano na Tunu nyingine za Taifa. Tuko ktk kumbukizi ya miaka 22 ya Mwalimu: Piga vita ukabila, ukanda na udini. #SISI NI TAIFA.
 
Malipo ya hiyo mikopo yanatokana na fedha zipi? sio madini ya Shinyanga yalipe mkopo wa CT scan iliyonunuliwa Zanzibar
Yatatokana na makusanyo ya kodi ya mapato na ushuru ambayo ni mambo ya muungano.
 
Huu muungano unauumiza zaidi Tanganyika kuliko Zanzibar, wazanzibar waliondoa kinyemela swala la mafuta na gesi kuwa la muungano lakini Leo hii tunapata rais mzanzibar anakimbilia kusaini mikataba ya gesi ya Tanganyika.

Kama wao hawakuamini kuwa serikali ya muungano haiwezi kupinda maslahi ya gesi yao kwanini raia wa kwao aje asimamie gesi ya tanganyika.

Wakati muungano unaanzishwa katiba ilisema Jambo lolote la muungano ili libadilishwe linatakiwa lipate ridhaa ya theruthi mbili za Baraza la wawakilishi na bunge la jamhuri ya muungano lakini Sasa hivi tunaambiwa Kuna Keri za muungano ambazo hazitajwi zimerekebishwa.

Isitoshe Kama Kuna kero Basi muungano huu ni kero bora uvunjwe
 
Hadi Samia amalize urais wake tutaona mengi sana. Wale wanaoipinga katiba mpya wataikubali tu. Ni kama vile kwa sasa Bara na Visiwani tupo chini ya Tiptip
Mimi ni mmoja ambaye sikuwa napenda katiba mpya haswa wakati huu na sababu kuu ni kuwa wanaoitaka kwa nguvu wana nia moja tu ya kutaka madaraka huku wakiwa na ushirika na watu ambao wamekuwa mwiba kwa miaka mingi kwenye maslahi ya nchi yetu; na vijana wetu kutumiwa kwa faida ya maadui zetu wa ndani na nje kama nchi, kwakua tu wapo kwenye desparate state hasa ya kukosa ajira.

Lakini kwa dhati ya moyo, jinsi inavyozidi kusogea siku kuna mambo naona hata mimi kwamba bila katiba mpya nchi yetu hii itaendelea kuendeshwa kwa mawazo ya watu ambao hawafikirii maslahi ya wengi. Na kisha madaraka yanajionyesha kuwa ndiyo tamaa ya wengi bila kujali madaraka hayo yatasaidia nini watu wa nchi yetu.

Mungu isaidie nchi yangu Tanzania.

Naona kama hii transition Mungu mwenyewe kaisababisha ili atupeleke kunapohitajika kwa faida ya watu wake.

Over to you my God in Jesus name, AMEN!
 
Back
Top Bottom