Mkanganyiko wa Katiba ya Sasa

Kuna haja ya kuanza upya! .. Tanganyika irudi na itambulike kama nchi yenye Serikali yake ya majimbo. Ikiisharudi ndio huu muungano usanifiwe upya au uvunjwe rasmi.

Badala ya kuwa na muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao umejaa utata usioweza kurekebishwa kwa kuandika katiba ya serikali tatu, ni bora Tanganyika na Zanzibar ziingie kwenye muungano wa Afrika Mashariki ili iundwe Fédération of East African States inayojumuisha DRC,Burundi,Rwanda, Uganda South Soudan,Kenya, Tanganyika, Zanzibar na Comoro.
 
Halafu Zanzibar inapewa mashine 5.Mkoa wa Morogoro unapewa mashine 1 wakati una idadi kubwa ya watu kuliko Zanzibar.
Mhuuu! umeliona hilo, basi na ndege pia zile 2 ni za zanzibar kati ya 10. hizo 8 mutagawana nyie Mil. 50 na hizi mbili sisi Mil 1.5.
Ukisema Muungano wa Zanzibar na Tanganyika unakusudia Nchi mbili zilizokuwa huru na siyo idadi ya watu au ukubwa wa Ardhi.
Kama tutaona Hatuwezi kuendelea na MUUNGANO kwa sababu Mzanzibari kawa Raisi wa Muungano bora tuelekeee kwenye BREXIT mapeema kabla hatuja ingizana vilipuzi vya kuviziana na kusababisha hujuma na umwagaji damu.

Maana Mama 2025 tunaye na baada ya hapo tunawaletea Husein mwinyi awe Mrithi wake. naye angalau apewe miaka 10.
Maana na Tanganyika alipotoka Mkapa kafuatia Kikwete kisha Magufuli wote watanganyika. na wazanzibari wlisema kisha wakanyamaza.
 
Hili la Zanzibar linahitaji majadiliano murua. Kwa sasa Rais amewapa kama Rais wa Tanzania je mipango ya Zanzibar katika mkopo huo ilikuwa ipi, iliingiaje? Ilikuwa in separation kwenye proposal au generalized, kwanini? Je kama wao hawataki CT Scan wanataka kingine? Ndiyo mikanganyiko kama hiyo.

Sipendi Kusema sana kwakua naupenda Muungano naipenda Zanzibar kama navyoipenda Tanzania bara, hafai Zanzibar ipewe vitu kama hisani. Ilitakiwa na yenyewe iwe inajipangia kwa mahitaji yake na isiwe tu kwakua leo Rais anatoka huko basi ionekane anapendelea je akiwa si wa huko?

Zanzibar inahitaji kuheshimika either Rais akitokea huko au akitokea huku. Hii ingekuwa rahisi tu, tatizo kubwa ni letu individuals tunaochukua nafasi hizi, mipango yetu mingi ni very general wala hazipo specific na inclusive let alone kwa nchi hata kwa raia wenyewe tunapenda kuwaaamulia watu wetu kwa utashi wetu individuals, hatujazoea kuenda kwa raia japo mifumo hiyo ipo mpaka ngazi ya kaya; ndiyo sababu kila mara tunarudia rudia makosa yale yale...
 
Wakati wa kusainiwa mkataba wa Muungano, yalikuwa mambo 17. Baadaye yakaongezwa mpaka kufikia 24.

Misaada na mikopo ya nje, ni kweli ni jambo la Muungano. Zanzibar inastahili kupewa asilimia fulani (sina uhakika, lakini nadhani ni asilimia 4). Lakini pesa hiyo hukabidhiwa kwa Serikali ya Zanzibar kwaajili ya kugharamia mambo yasiyo ya Muungano, afya ni mojawapo. Pesa hiyo ikipelekwa Zanzibar, inatumika kwa kadiri ya maamuzi ya Serikali ya Zanzibar na Baraza la wawakilishi. Kwenye hilo msemaji haiwezi kuwa serikali ya JMT wala Rais wa serikali ya JMT. Hili la CT scan, kwa nini maamuzi na msemaji awe serikali ya JMT?
 
Hapo ndipo utata ulipo, which means Mh. Rais ata set precedence mbaya kwa Zanzibar, kesho akiwa siyo mzanzibar naye ataamua awape kingine kwa utashi wake bila kujali Zanzibar ina maamuzi yake inapokuja kwenye maswala yake ya ndani
 
Haikutamkwa kuwa kuna pesa inapelekwa Zanzibar. Imetamkwa kuwa Seikali ya JMT inanunua CT scan machines zitakazosambazwa kwa mikoa yote ya bara na visiwani. Zanzibar ina haki ya kupata gawio la misaada na mikopo ya nje, lakini matumizi ya hiyo pesa hupitishwa na baraza la wawakilishi na Serikali ya Zanzibar, siyo serikali ya JMT.
 
Reactions: Ame
kipi bora, turekebishe twende sawa kabisa au tuishi tuu na donda ndugu?
 
Sisi wengine, hatuna fikra ya kuwa marais wala wabunge au mawaziri (lakini hata tukitaka ni haki yetu), tunataka nchi yetu iongozwe kwa haki, uhuru na demokrasia. Kukiwa na katiba inayolinda haki, uhuru na demokrasia, kuna watu wengi tu, tena bila ya mbeleko ya chama chochote cha siasa, watasimama na kutetea mambo yenye maslahi ya Taifa letu, bila ya kufikiriwa kuwa wanafanya hayo kwaajili ya tamaa ya madaraka.

Sahizi hata ukinyanyuka wewe, ukahoji masuala mbalimbali yahusuyo taifa letu, hata kama hufanyi hivyo kwa mtazamo wa imani za kichama, utapigwa virungu, utabambikiwa kesi, utafirisiwa, na kuambiwa wewe ni mpinzani.

Tunataka KATIBA MPYA itakayompa uhuru kila raia, wa kuweza kuhoji na kutenda lolote lisilo kinyume na sheria, huku akilindwa na katiba.

KATIBA MPYA NI HITAJIO YA RAIA YEYOTE MWENYE MAPENZI MEMA NA TAIFA HILI.
 
Malengo ya mkopo zingatia. Huwezi kukopa fedha za maendeleo ya kilimo halafu unaenda kununulia V8.
 
Afya sio suala la muungano, Zanzibar wao wenyewe wanawajibika kupanga na kuamua kuhusu mambo ya afya na sio kuamuliwa na serikali ya muungano. CT scan ni jambo la afya kwa 100% halikupaswa kufanyiwa maamuzi na Rais Samia, ni makosa makubwa. Ni kujipendekeza kulikovuka mipaka.

Samia alikosea, huenda hajui sheria au hajui mipaka ya maamuzi yake kikatiba, nahisi bado anawaza kijinsia (kike) na Kikanda (mzanzibar) hatambui kama yeye ni Rais wa Tz.
 
Afya sio suala la muungano, Zanzibar wao wenyewe wanawajibika kupanga na kuamua kuhusu mambo ya afya na sio kuamuliwa na serikali ya muungano. CT scan ni jambo la afya kwa 100% halikupaswa kufanyiwa maamuzi na Rais Samia, ni makosa makubwa. Ni kujipendekeza kulikovuka mipaka.

Samia alikosea, huenda hajui sheria au hajui mipaka ya maamuzi yake kikatiba, nahisi bado anawaza kijinsia (kike) na Kikanda (mzanzibar) hatambui kama yeye ni Rais wa Tz.
 
Asante kwa kujadili vema. Ila, Zanzibar inaheshimiwa sana na sisi sote ni Watanzania.

Pili,maelekezo ya hizo mashine si hisani ni sehemu ya kudumisha Muungano wetu.

3. Zingatia malengo ya hizo fedha. Ni afya. Pia hadi Rais anaelekeza anajua hali ya Zanzibar. Rais ni taasisi.
 
Malengo ya mkopo zingatia. Huwezi kukopa fedha za maendeleo ya kilimo halafu unaenda kununulia V8.
Samia yeye ni nani katika serikali ya Zanzibar mpaka awaamulie mambo yao ya Afya?
Je, anajua serikali ya Zanzibar ilikuwa na mipango gani kuhusu kuwa na CT scan?
Je, hilo ndilo hitaji lao la sasa hapo Zanzibar?

Kama pesa za mikopo/misaada zilitolewa kulenga kuboresha mambo ya afya, basi ipewe serikali ya Zanzibar ikazipangie yenyewe, na sio kupangiwa na bara.
 
Ndio maana tulipounga Kuna Mambo yalifanywa kuhusu muungano na mengine siyo ya muungano, afya sio swala la muungano. Mara nyingi Zanzibar amekopa kupitia serikali ya muungano na sio hisani kikatiba Zanzibar anaruhusiwa kupata asilimia 4 ya misaada na mikopo leo iweje pesa za tanganyika ziende Zanzibar
 
Malengo ya fedha za mkopo kutoka Breton woods siyo ya Wizara zetu za afya. Elewa hili.

Msingi wa mkopo kutoka IMF ni afya siyo kununulia majahazi au V8. Zimekuwa allocated ktk maeneo ya kimkakati kiafya.
 
Malengo ya fedha za mkopo kutoka Breton woods siyo ya Wizara zetu za afya. Elewa hili.

Msingi wa mkopo kutoka IMF ni afya siyo kununulia majahazi au V8. Zimekuwa allocated ktk maeneo ya kimkakati kiafya.
Afya haimaanishi CT scan pekee yake. Zanzibar wangeweza kupewa sehemu yao, na kuambiwa kuwa dhumuni la mkopo huu (ambalo najua kuwa wanajua) ni kwenye afya. Huko kwenye afya watafanya nini, ni maamuzi yao na wala siyo jukumu la Samia.
 
Yaani rais wa muungano (bara) anajua zaidi mambo ya wazanzibar kuliko serikali ya Zanzibar yenyewe?

Kwa hiyo hospitali za Zanzibar zinahitaji sana hizo CT scan machine kuliko mambo mengine ya afya?

Kama pesa zimetolewa na mhisani kwa malengo ya kuboresha afya, maana yake kikatiba haziihusu Zanzibar kwa 100% kwa kuwa afya sio jambo la muungano(Huu ni ukweli mchungu).

Hivi unadhani mhisani aliyetoa hizo pesa hajui katiba yetu inasemaje kuhusu mambo ya Afya kikatiba?

Kukumbusha tu, Muungano unadumishwa kwa kufuata katiba kwanza na sio kufanya mambo ya hisani.
 

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…