Mkanganyiko wa Katiba ya Sasa

Unapaswa kufahamu kwamba utendaji wote kwa Serikali upo chini ya Rais. Mawaziri, kwa mujibu wa katiba,wanafanya kazi kwa niaba ya Rais, hivyo Rais anaweza, kama alivyofanya, kuelekeza
 
Orodha ya asili ilikuwa na mambo 11 tu kwa orodha
 
@Pascal Mayalla mtaalam wananzengo wanakusubiri kwenye numbaga uwafafanulie tafadhali

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Afya haimaanishi CT scan pekee yake. Zanzibar wangeweza kupewa sehemu yao, na kuambiwa kuwa dhumuni la mkopo huu (ambalo najua kuwa wanajua) ni kwenye afya. Huko kwenye afya watafanya nini, niaamuzi yao na wala siyo jukumu la Samia.
Unafahamu mahitaji ya hizo mashine kwa hospital kuu za Zanzibar?
 
Hapo ndipo utata ulipo, which means Mh. Rais ata set precedence mbaya kwa Zanzibar, kesho akiwa siyo mzanzibar naye ataamua awape kingine kwa utashi wake bila kujali Zanzibar ina maamuzi yake inapokuja kwenye maswala yake ya ndani
Ahsante kwa mjadala wa kiustaarabu.

Nami niongezee hili, kweli u Rais ni taasisi lakini inyoongoza watu na kwa mujibu wa sheria, siyo inayojisimamia yenyewe zipo na zingine nisiende huko kwa maslahi mapana ya nchi yetu.

Mfano, mdau amesema Katiba inasema mambo hayo yalitakiwa yajadiliwe na Baraza la Wawakilishi na kisha anayewajibika kulisemea ni Rais wa Zanzibar na siyo wa Tanzania kwakua ni mambo ya ndani ya Zanzibar, je hapo taasisi ya u Rais wa Tanzania inaingiaje?

Lengo liwe ni kukubali kuongozwa na sheria, kanuni na taratibu na iwe consistent isiwe inabadilika badilka kila anapoingia mtu wa tofauti kwenye hizo taasisi.
 
Kila siku nasema ujinga ulifanywa na viongozi wetu wa Tanganyika wakati huo wa kuungana kukubali kuwaachia Zanzibar mambo yao halafu wao ndio wakajiona wajanja kwa kuigeuza Tanganyika kuwa ndio Tanzania matokeo yake ndio haya sasa.
 
Siyo hisani ya fedha za Tanganyika ni haki ya Zanzibar.

Lakini pia, kuna ubaya gani kwa mfano,Zanzibar kuwasaidia ndugu zao wa Bara na Bara kuwassidia Wazanzibari? Kwa nini vitu vizuri tunataka kuviingizia fikra hasi?
 
Siyo hisani ya fedha za Tanganyika ni haki ya Zanzibar.

Lakini pia, kuna ubaya gani kwa mfano,Zanzibar kuwasaidia ndugu zao wa Bara na Bara kuwassidia Wazanzibari? Kwa nini vitu vizuri tunataka kuviingizia fikra hasi?
Wangekuwa na nia ya kusaidiana tusingesikia malalamiko yao ndio maana tunaitaka Tanganyika yetu
 
1) Kila raia wa Zanzibar ni raia wa Tanzania

2) Siyo kila raia wa Tanzania ni raia wa Zanzibar.
hiyo number 2 ina sura ya ubaguzi....

Mwalimu alipoulizwa hili alisema eti wazazibar ni wachache na ardhi yao si kubwa, kwa hili ni lazima katiba iwalinde....

Je haya tuliyajadili kwa pamoja au wachache ndiyo walituamulia wakati wa kutungwa katiba hii? mliokuwepo mwaka 1977 tujuzeni mchakato ulifanyikaje?
 
Tatizo kubwa hapa ni Tanganyika kukosa mtetezi wa kweli.. Imegeuka Shamba la bibi
 
Lkn kuna kanuni ya mgawo wa hizo fedha . Siyo kama anavyonya rais. Ndege zimeletwa mbili, moja inaenda Zanzibar, fedha zimekuja anagawanya bila formula. Mwambieni huyu mama kwamba awakwaza watanganyika.
 
Muungano huu ufe tu, una manufaa kwa watu wachache sana wenye maslahi binafsi.
 
Unapaswa kufahamu kwamba utendaji wote kwa Serikali upo chini ya Rais. Mawaziri, kwa mujibu wa katiba,wanafanya kazi kwa niaba ya Rais, hivyo Rais anaweza, kama alivyofanya, kuelekeza
Nadhani huelewi hoja iliyopo. Waziri wa afya aliye chini ya Rais wa JMT ni Waziri wa Afya wa huku bara na siyo Waziri wa afya wa Zanzibar.

Kwenye suala la afya, Rais wa JMT hana mamlaka juu ya Zanzibar. Na wala waziri wa afya wa huju bara, hana mamlaka juu ya Zanzibar, isipokuwa linapokuwa kwenye kiwango cha kimataifa.
 
Orodha ya asili ilikuwa na mambo 11 tu kwa orodha
Asante kwa kunirekebisha. Nadhani upo sahihi. Mwanzoni yalikuwa 11, baadaye 17.

Sasa kama Rais Samia na mwenzie Mwinyi wameamua kuongeza na Afya liwe suala la Muungano, wapeleke kwenye bunge la JMT na Baraza la Wawakilishi, ili ikapitishwe kikatiba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…