Mkanganyiko wa Katiba ya Sasa

Hoja ya kusema Wazanzibari ni wachache au ardhi yao ni ndogo ndiyo maana Watanganyika hawatakiwi kuwa na access na kilichipo Zanzibar, siyo sahihi. Kama kilichopo huko ni kidogo, si wanaruhusiwa kuja bara ambako kuna vingi, na hawabaguliwi wala kuzuiwa kama ilivyo kwa wenzao wa bara.
 
Siri wanayo CCM kwanini muungano wa aina hii ni wa pekee na wauonevu kwa upande mmoja.
Wanaofaidika zaidi Muungano huu ni Zanzibar. Mzanzibari anapokuwa rais wa muungano anatawala na Tanganyika na mambo ya muungano, anasimamia bajeti ya Tanganyika na kuteua mawaziri wake, lakini mtawala akitoka Tanganyika hatawali Zanzibar kwa kuwa kiongozi wao yupo. Mfano sasa hivi Tanganyika haina kiongozi mkuu Mtanganyika anayesimamia masuala ya Tanganyika. Waziri Mkuu ni mteule wa Rais wala si wa wananchi wa Tanganyika
Katiba ya Tanzania ni ya ajabu haijawahi kutokea ko kote.
 
Watanganyika ni malofa.
Samahani.
Kama kuna mtanganyika anabisha aende Zanzibar akagombee hata uenyekiti wa mtaa au Ushea atarudi na jibu
 
Tukubali kwanza kuwa watangulizi wetu walifanya makosa kuunda huu muungano lakini sasa tuamue ku - uunda upya au kuuvunja.

Dhambi ya mapinduzi tumeiirithi kwa lengo la kuutetea umajinuni wa Afrika.

Chakushangaza hapa; unamfukuza mwarabu ambaye ndie mtawala halali lakini unaamua kuoa binti yake na kubaki nae kama mke?

Ulaghai gani huu ulioigharimu Tanganyika ?.... Wakati wa ku - urekebisha nadhani umefika.
 
Kuna mda muungano wetu unatufanya tujue utu na ubinadamu wetu.

Ukiangalia kwa sasa huwezi jua jambo la muungano ni lipi na lisilo la Muungano ni lipi.
 
Wewe ndo pia hutaki kujua mamlaka ya Rais kikatiba
 
Asante kwa kunirekebisha. Nadhani upo sahihi. Mwanzoni yalikuwa 11, baadaye 17.

Sasa kama Rais Samia na mwenzie Mwinyi wameamua kuongeza na Afya liwe suala la Muungano, wapeleke kwenye bunge la JMT na Baraza la Wawakilishi, ili ikapitishwe kikatiba.
Hakuna kilichoongezwa wala kupunguzwa kwenye hoja ya mkopo tunayoijadili. Kuna kutokufahamu au kutokufahamiana kwenye hii hoja.
 
M
Maswali yote yaliyo ulizwa chanzo chake ni kuchanganyikiwa kwa mleta mada; kwani kikatiba, raia wote wa Zanzibar ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT), hivyo suala la kuwa Rais na uraia hakuna mkanganyiko wowote bali kilichopo ni madhanio (assumptions) tu ya kinadharia kwa nia na lengo la kuwachanganya Watanzania!

Kuhusu ununuzi na mgawanyo wa hizo mashine aidha za afya au za aina nyingine yoyote kwa pande zote za JMT ni hivi - huu mkopo wa IMF kwa JMT ni kwa Zanzibar na Tanganyika au Tanzania Bara (ukipenda) yaani hilo ni moja ya masharti yake kwani, kama uliwasikia viongozi wetu vizuri katika maelezo yao, ni kuwa mkopo huu unalenga kupambana na UVIKO - 19 na athari zake kwa JAMII. Hivyo Serikali yetu ikaishawishi IMF kuwa mkopo huu ushughulikie mambo yote, ambayo ni CROSSCUTTING as far as UVIKO - 19 is concerned; siyo kununua chanjo tu kama walivyo kuwa wanataka na kushauri IMF. Huo ndio msingi wa huu mkopo kwenda Tanzania nzima, siyo eti kuwa sasa suala la afya ni suala la Muungano, HAPANA. Sijui nimeeleweka?!
 
Wewe nadhani hujaelewa chochote. Soma tena. Kuna mahali, nimeeleza kuwa raia wa Zanzibar siyo raia wa Tanzania?

Hata kwenye ununuzi wa hizo CT scan, hujaelewa chochote. Soma tena.
 
Wewe ndo pia hutaki kujua mamlaka ya Rais kikatiba
Eleza mamlaka ya Rais wa JMT kwa mambo ya Zanzibar yasiyo ya muungano, lakini nina uhakika wewe ndiye usiyeelewa mipaja ya mamlaka ya Rais wa JMT kwa Zanzibar kwa mambo yasiyo ya muungano.
 
Eleza mamlaka ya Rais wa JMT kwa mambo ya Zanzibar yasiyo ya muungano, lakini nina uhakika wewe ndiye usiyeelewa mipaja ya mamlaka ya Rais wa JMT kwa Zanzibar kwa mambo yasiyo ya muungano.
Pengine unapaswa kuelewa tunapozungumzia kazi/majukumu ya Rais. Hapa tunazumgumzia mikopo ya nje ambayo yapo kwenye mamlaka ya Jamhuri ya Muungano ambayo msimamizi wake mkuu ni Rais. Kwenye fedha za mikopo Rais anayo mamlaka ya kutoa miongozo ya matumizi yake kama alivyofanya.
 
Hizo ni fikra na matakwa yako lakini kikatiba, ni kwamba mgawanyo wa pesa yote ya nje (mikopo au misaada), mgao wa Zanzibar unapelekwa SMZ. Na serikali ya SMZ ndiyo yenye mamlaka kisheria kupanga matumizi ya pesa waliyopewa kwa kuzingitia madhumuni ya mkopo au msaada.

Ifahamike kuwa serikali ya JMT inapoomba mkopo au msaada wa nje, SMZ hushirikishwa. Kwenye suala la manunuzi ya CT scan, hakuna mahali popote ilipoelezwa kuwa Rais na Seirikali ya JMT, imetoa pesa kuwapa SMZ bali wanazungumzia kuwapelekea Zanzibar machine za CT scan. Hii ina maana CT scan machines zimenunuliwa na serikali ya JMT. Na hakuna uhakika kqma hizo machines ndiyo mgao wa fedha kwa SMZ au wanapewa CT scan machines, huku mgao wao wa fedha za mkopo ukiwa upo pale pale.

Note: Taarifa imesema kuwa serikali ya JMT imeagiza machines za CT scan kwaajili ya hospitali zote za Tanzania bara na visiwani. Hiyo ya kusema Rais amezielekeza serikali ya JMT na SMZ kuwa pesa hizo za mkopo, pamoja na mambo mengine, zitumike kununulia CT scan machines, umeisikia wapi?
 
Hili bandiko ni kuhusu mkanganyiko ktk katiba ya sasa. Maelezo yakaja kuhusu CT Scan kupelekwa Zanzibar wakati afya sio swala la muungano. Hoja yangu ikawa fedha hizo ni mkopo wa nje ambao ni swala la muungano. Kikatiba uendeshaji wa nchi (administration) ni mamlaka ya Rais na anaweza kuagiza uendeshaji wake kwa mawaziri na ndivyo alivyofanya.

Kuhusu mgao kwa asilimia haijazungumzwa kwenye katiba na kinachofanyika ni ama utekelezaji wa sheria - kama ipo - makubaliano au vyovyote itakavyokuwa. Kwa vyovyote vile, kwa maoni yangu, hayamzuii Rais kutekeleza wajibu wake

Moja ya mambo yanayoweza kuleta utata kwenye katiba yetu n kuingiza mambo bila kuangalia athari zake za muda mrefu kama hili la mikopo, kodi ya mapato ambayo utekelezaji wake unafanywa na wizara ambazo sio za muungano. Yaani kutoa fursa upande mmoja, kisha ukaizuia upande mwingine ambapo mimi naona hufanywa makusudi kwa kudhani tunadhubiti upande mwingine.

Bado kwa Rais kutoa miongozo/maelekezo kwenye CT Scan hakuna mkanganyiko wa kikatiba.
 
ZANZIBAR ni kama kupe ana2nyonya 96% Ya pato la taifa ni tanzania bara hao zanzibar hawana export yoyote ya maana yenye bei ya maana kwenye soko la dunia na kama utalii bado bara tupo juu yao maana ndo 2na vivutio vingi sio watalii wote wanapenda kucheki magofu ya watumwa ya akina SULTAN
 
NYIE hamuwezi kutuongoza cc mna bahati sana uyo mama kaupata urais kwa bahati af inaniuma kuona 2nagawana xana akati nyie ni sawa na kamkoa cha Dar.Muungano ukivunjika wazenji mtakiona cha moto maana maisha yatakuwa magumu na kuzamia sauzi mpaka mpande boti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…