Imalamawazo
JF-Expert Member
- Jul 27, 2021
- 1,343
- 3,269
Kumbe hata hujafuatilia. Mbona kila siku wanaeleza anayetoa pesa ni nani na nani? Kwa kifupi, mradi anajenga mchina, anasimamia mchina, ila sehemu ya pesa katoa Oman ambaye anaikumbuka Bagamoyo kama moja ya himaya yake. Jiulize je mchina kashindwa kutoa pesa yote mpaka akamtafute wa kushirikiana naye? Kwa kifupi ni mahesabu ya kumfanya sultan ajaribu tena bahati yake kupitia Bagamoyo na baadae Zanzibar.Sasa nani alikwambia kuwa oman watajenga hiyo bandari?
Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
Watazitapika wakiwa juu au chini ya ardhi?Hiyo bandari kuna watu watasaga meno baadae penye uhai,acha wazile kwa sasa ila huko mbele watazitapika tu
Wa mjini wanapenda sana white elephantHuu mkanganyiko wa kauli za hawa viongozi waandamizi wa chama na serikali kuhusu bandari ya Bagamoyo inaonyesha kuna madudu sana ndani ya terms of contract,na hii inatokana na baadhi ya viongozi wachache waliolenga kujinufaisha na mradi huo .
Rejea jinsi dharura iliyotumika kupitisha miswaada hiyo na idadi ya wabunge waliotumika kufanya ufedhuli huu,idadi walikuwa ni sitini tu kati ya wabunge mia tatu.
Mzee Mangula anasema bandari haimo kwenye ilani ,bali ilani inataja ujenzi wa gati tu. je nini tofauti ya gati na bandari?
Wanaopanga kujinufaisha na huu mradi kwa kuliingizia Taifa hasara kama ni kweli, wajue kwamba tutawadai wao pia tutakidai kizazi chao kwa gharama yoyote ile warudishe walichopora
Watazitapika kwa utaratibu gani?.Mkiambiwa kuwe na katiba mpya itakayo wawajibisha watu mnajifanya hamnazo leo unaongelea habari za kutapisha watu wakati unajua chini ya utaratibu uliopo hakuna kitakacho fanyika.watakula hadi wasaze na hutawafanya kitu sana sana utaishia kulalamika uku mitandaoni.Hiyo bandari kuna watu watasaga meno baadae penye uhai,acha wazile kwa sasa ila huko mbele watazitapika tu
Na hawatakaa hata siku moja waweke terms zitakazoifaidisha Tanzania sawa na wao. Hapo ndipo lilipo tatizo. Bado kuna mengine mengi tu ya kuwazua.Suala sio kujenga au kutokujenga bandari, kwa mkataba au makubaliano yapi? Kama nchi, maslahi yetu yameangaziwa ipasavyo?
Nna imani tungekua na uwezo tungeijenga wenyewe hiyo bandari kwa pesa zetu. Tatizo ni hapo kwenye terms and condition ( pakiwekwa sawa, ijengwe tu hata kesho).
Na hawatakaa hata siku moja waweke terms zitakazoifaidisha Tanzania sawa na wao. Hapo ndipo lilipo tatizo. Bado kuna mengine mengi tu ya kuwazua.
Huyo mzee kachemsha, thanks to Nape kamjibu vizuri tuu kwamba wamefanya mengi tuu ambayo hayakuwa kwenye ilani. Ajifunze kwa wazee wenzake wanaozeeka na misimamo imara kama akina Pius Msekwa, Warioba etcTwo wrongs dont make another wrong thing becomes right. Kuna kitu hakiko sawa. Tunalazimisha sana huu mradi kwa sababu zipi?
Wewe ambaye hujakurupuka si uweke hapa?Kaisome ilani ,inaonekana unakurupuka Sana
Daah kuna watu mna mawazo ya kindezi aisee!! Yaani karne hii unawaza mkoloni arudi kukutawala wakati ukoloni mpya ni wa kiuchumi?? Mchina karibia yuko kila kona ya dunia na anavuna mabilioni kupitia mikataba yenu wenyewe (umesikia ya uwanja wa Entebbe??) kalagabaho...Waambieni ukweli wa Oman, hata kama hiyo bandari itajengwa na hata kama tukishindwa kulipa deni lao, huyo mtu wao Sultan wa Zanzibar hatarejea Zanzibar kamwe.
Kwa fasili yako, ni nini maana ya kutawala?Daah kuna watu mna mawazo ya kindezi aisee!! Yaani karne hii unawaza mkoloni arudi kukutawala wakati ukoloni mpya ni wa kiuchumi?? Mchina karibia yuko kila kona ya dunia na anavuna mabilioni kupitia mikataba yenu wenyewe (umesikia ya uwanja wa Entebbe??) kalagabaho...
Pipe dream. Za EPA, rada, Tegeta Escrow hadi leo hata kichefuchefu tu hawajakihisi ndio waje watapike za Bagamoyo? Unaijua CCM wewe?Hiyo bandari kuna watu watasaga meno baadae penye uhai,acha wazile kwa sasa ila huko mbele watazitapika tu
Kiitukadi Mangula na Magu wanafanana hivo naamin Mangura hakujutia kufanya kazi na Magufuli ila naamini amejutia kuwah kufanyakazi na Jakaya Mbepari.Mangula anajua kabisa Chama kilikosea kumpitisha Mrundi kushika hatamu!Toa mifano ya awamu nyingine ya uongozi wa nchi yetu!sio hii iliopita ya Mrundi!!!
Mambo mengine soma tu uachane nayo. Dunia inaenda kuwa kijiji kupitia teknolojia, baadhi ya mataifa yameshaanza kufikiria chips kwa ajili ya control ila huku kuna mtu yupo anawaza ukoloni wa sultani kwamba anataka kurudi atawale zanzibar halafu wewe unatumia nguvu kumjibu.Daah kuna watu mna mawazo ya kindezi aisee!! Yaani karne hii unawaza mkoloni arudi kukutawala wakati ukoloni mpya ni wa kiuchumi?? Mchina karibia yuko kila kona ya dunia na anavuna mabilioni kupitia mikataba yenu wenyewe (umesikia ya uwanja wa Entebbe??) kalagabaho...
Ni kweli. Kila wakitowa maelezo ndivyo wanavyozidi kuleta mashaka. Dalali Zitto kile kipindi cha mwanzo mwanzo mwa utawala wa Magufuli alikuwa anasema tusipowakubalia haraka tutakuwa tumepoteza bahati kubwa kwani wataenda sehemu nyingine, na kila nchi inawataka. Mpaka leo imepita miaka zaidi ya sita hawajaenda popote na wanahaha kushawishi ili wakubaliwe. Najua wanatumia fedha nyingi sana na kuna watu wameahidiwa mshiko mrefu iwapo mradi utapita.Na ndio uharaka unapoleta shaka, kwanini tukimbilie kujenga wakati kuna kila dalili kwamba terms haziko sawa?
Unaona hadi inafika mahali wengine wanasema hakujawahi kuwa na mkataba wakati jiwe la msingi liliwekwa na mheshimiwa awamu ya nne.
Mbona Magufuli kawatapisha sana tuWatazitapika kwa utaratibu gani?.Mkiambiwa kuwe na katiba mpya itakayo wawajibisha watu mnajifanya hamnazo leo unaongelea habari za kutapisha watu wakati unajua chini ya utaratibu uliopo hakuna kitakacho fanyika.watakula hadi wasaze na hutawafanya kitu sana sana utaishia kulalamika uku mitandaoni.